
Freestyle Football Tanzania kwa kushirikiana na kipindi cha Sports Bar cha Clouds TV wamezindua rasmi sindano la kumtafuta bingwa wa kuchezea mpira wa miguu kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Mchakato wa kumpata bingwa wa Freestyle Football utafanyika katika wilaya tatu za Dar es Salaam (Temeke, Ilala na Kinondoni) kisha fainali itafanyikia Coco Beach.
Temeke itakuwa wilaya ya kwanza ambapo washindi watano watatafutwa tarehe 19 November kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, ikifuatiwa na Ilala November 26 kisha Kinondoni watahitimisha Disemba 3 kabla ya fainali inayotarajiwa kufanyika Disemba 11 mwaka huu.
“Malengo ya shindano hili ni kuibua vipaji na kutoa fursa kwa vijana. Tumeanza na mkoa wa Dar es Slaam, panapo majaaliwa tunatarajia tufanye shindano hili kwenye mikoa mingine ili kupata bingwa atakaye tuwakilisha katika mashindano ya kimataifa,” amesema Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Bw. Pascal Chang’a.

Amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo linalodhaminiwa na RedBull na kuratibiwa na Shadaka Sports Management, vilevile amefungua milango kwa kampuni nyingine kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo lina malengo chanya kwa jamii.