Habari zinazidi kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii kwamba beki wa kati wa Azam Pascal kurejea kwenye timu yake ya zamani ya El Emerreikh ya Sudan kwa mkataba wa miaka miwili.
Raia huyo wa Ivory Coast ameondoka Azam baada ya kuhudumu kwa miaka miwili tangu alipojiunga mwishoni mwa mwaka 2014.
Wawa hajaonekana kwenye mechi za ligi msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu ambayo alipata wakati Azam ikicheza na Esparance Sportive de Tunis katika kombe la shirikisho.
Wawa amefata nyayo za raia mwenzake wa Ivory Coast Kipre Tchetche ambaye yeye alitimkia zake Oman.