Jana Jumamosi November timu nzima ya shaffihdauda.co.tz iliungana na ile ya Sports Extra ya Clouds FM kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za ligi za Ulaya zilizopigwa kuanzia saa 9:30 alasiri.
Tulikuwa na wadau wetu wa Mbagala tukiangalia soka kwa pamoja ndani ya Sabasaba Classic Bar iliyopo maeneo ya Sabasaba.
Mchezo uliovuta hisia za wadau wengi wa soka ulikuwa ni wa EPL kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Wadau walikuwa ni wengi na tulifahamiana na kupiga stori mbili tatu hususan kuhusu masuala ya soka kuanzia hapa kwetu Tanzania hadi kwa wenzetu barani Ulaya na Dunia kwa ujumla.
Asikwambie mtu kulikuwa na mzuka wa hali ya juu kwa mashabiki wa timu zote mbili waliohudhuria kuangalia game pale Sabasaba Classic Bar hususan yalipofungwa magoli watu walipagwa kwa shangwe na tambo za hapa na pale.