Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Dogo aliyezaliwa mwaka 2000 ameweka rekodi Serie A

$
0
0

moise-kean

Moise Kean amekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2000 kucheza kwenye moja ya ligi nne bora barani Ulaya baada ya kuingia kwenye mchezo wa Juventus dhidi ya Pescara.

Kinda huyo wa miaka 16 anayekipiga timu ya taifa ya Under-17 ya Italy alitokea benchi kuchukua nafasi ya Mario Mandzukic zikiwa zimesalia dakika sita pambano kumalizika.

Kijana huyo aliyezaliwa February 28, 2000, anafanishwa na Mario Balotelli kutokana na uwezo wake uwanjani ameshatajwa mara tano kukaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba na kocha Massimiliano Allegri katika mechi za Serie A na mara mbili katika mechi za Champions League.

Juventus sasa wako mbele kwa pointi saba dhidi ya AS Roma walio nafasi ya pili ambao watacheza na Atalanta Jumapili hii.

Sami Khedira, Mandzukic pamoja na Hernanes walifunga magoli ya Juve na kuifanya timu hiyo kuufukuzia ubingwa wa Serie A kwa mara ya sita mfululizo.

Wachezaji wengine waliozaliwa miaka karne hii ambao tayari wamecheza mechi za ligi kuu…

Vincent Thill alikuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2000 kucheza ndani ya Ligue 1 nchini Ufaransa. Kijana huyo mwenye miaka 16 ambaye ameshacheza mechi saba na kufunga goli moja dhidi ya Luxembourg alicheza kwa dakika nane wakati Metz ilipocheza dhidi ya Bordeaux mwezi September.

Jack Aitchison, pia ni mchezaji aliyezaliwa mwaka 2000 ambaye alifunga kwenye mchezo wake wa kwanza akiitumikia Celtic huku ikiwa ni mpira wa kwanza kugusa tangu alipoingia uwanjani kwenye mechi ya mwisho ya msimu uliopita dhidi ya Motherwell.

Msimu uliopita, Callum Styles alikuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa karne hii kucheza ligi ya mpira wa miguu. Lakini kwa bahati mbaya usajili wake haukuwa umekamilika vizuri na ilipelekea Bury kunyang’anywa pointi tatu.

Mwezi April, mchezaji wa West Brom Jonathan Leko alikuwa ni mchezaji wa kwanza kucheza Premier League akiwa amezaliwa mwaka 1999. Hakuna mchezaji mwingine aliyezaliwa baada ya hapo amewahi kucheza ligi hiyo.

Hakuna mchezaji aliyezaliwa mwaka 2000 au baada ya hapo ambaye amepata nafasi ya kucheza kwenye Premier League, Bundesliga au La Liga.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>