Taarifa za kibiashara zinaripoti kuwa kampuni ya Under Armour imepoteza takribani kiasi cha dola za Kimarekani milioni 600 ($600m) ya thamani yake kama kampuni mpaka kufikia Ijumaa, huku stoko yake ikisemekana kushuka kwa aslimia 4 hasa baada ya viatu vipya vya Steph Curry kutokufanya vyema kama ilivyotegemewa.
CEO wa Foot Locker, Dick Johnson alisema Curry 3 “ilianza taratibu sana ukilinganisha na aina zake nyingine zilizopita,” hali inayopelekea kuanguka kimasoko.
Huku bidhaa za Curry zikiwa zinachangia asilimia 5 ($200 million) ya mapato ya bidhaa na biashara ya Under Armour kwa mwaka mzima wa kibiashara bado ndilo jina kubwa la kibiashara kwenye kampuni hiyo.
Johnson alisema kuwa mapato yaliyohesabiwa chini ya kampuni ya Foot Locker mauzo ya viatu ama vifaa vya michezo vya mpira wa kikapu vilikuwa na ushindani ambao ulikuwa laini kiasi katika kipindi cha nyuma ingawa aliongeza kuwa viatu vya Curry 2 na Curry 2.5, pamoja na Nike za Kyrie Irving vilifanikiwa vyema kupenya.
Johnson akaongeza kuwa bado ni mapema sana kusema lolote juu ya Curry 3. Mpaka siku ya Jumanne, Curry 3 itakuwa imefikisha mwezi mmoja sokoni.
“Tuna imani kubwa wao [Under Armour] watafanikiwa kuendelea kukuza biashara [biashara ya viatu] na kuongeza nguvu na ubunifu nyuma ya chochote wanachokifanya,” Johnson alisema.
Msemaji wa Under Armour alisema kampuni haitosema lolote kuhusiana na maneno ya on Johnson kuhusiana na mauzo ya Curry 3.
Kiatu kinakutana na changamoto tatu: Jambo la kwanza ni bei yake. Under Armour ilipandisha bei ya Curry 3 mpaka kufikia $140 ambayo ni zaidi ya laki 3 kwa pea moja. Hilo ni ongezeko la $20 kutoka kwenye Curry 1 na $10 kutoka kwenye Curry 2.