Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Yanga Hans van Pluijm amesema kwake ni poa tu kupewa majukumu hayo ndani ya klabu na atafanya kazi kwa kushirikiana na kocha mpya aliyekuja ili kuendelea kuleta mafanikio zaidi.
Babu amesema hii sio mara ya kwanza kwake kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi kwasababu akiwa Ghana, alishawahi kutumikia nafasi hiyo wakati akiwa kwenye academy moja nchini humo.
“Hii sio mara ya kwanza kwangu kuwa Technical Director, nilishawahi kuwa na dhamana hiyo wakati nikiwa RedBull Academy nilipokuwa Ghana. Lakini wakati huohuo nilikuwa kocha mkuu, nilikuwa na nyadhifa mbili kwa wakati mmoja,” maneno ya Hans wakati nikipiganae story muda mfupi baada ya kumkabidhi ofisi kocha mpya George Lwandamina.
“Nilishazoea kuonekana kwenye uwanjani kilasiku lakina kwa sasa haitakuwa hivyo kutokana na majukumu mapya niliyopewa lakini mimi mwenyewe nimekubali na nitashirikiana na kocha mpya aliyekuja ili kuleta mafanikio kwenye timu yetu.”
“Kitu muhimu ni kwamba, nitajaribu kumsaidia ili kuhakikisha anafanya kazi yake bila matatizo ili aweke umakini kwenye timu na tutafanya kazi kwa kushirikiana kwasababu kwa sasa nitakuwa nahusika na masuala yote ya soka ya kilasiku kwenye klabu.”
“Mashabiki wanatakiwa kumuunga mkono kama walivyofanya kwangu baada ya hapo nadhani kila kitu kitakuwa sawa kwa kocha aliyekuja huku nikitumaini kutakuwa na mafanikio kama kila mtu anavyotarajia.”