Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

AUDIO: Lwandamina amesema kitu alichokiona kwa wachezaji wa Bongo

$
0
0

img_5891

Tayari kocha mpya wa Yanga George Lwandamina ameshawasoma baadhi ya wachezaji wanaocheza Tanzania.

Lwandamina amesema asilimia kubwa ya wachezaji wa Bongo wanacheza huku wanapumzika wakati mchezo wa soka ukitaka mwendelezo wa uchezaji kwa dakika 90 za mchezo.

Kocha huyo ambaye ameshatambulishwa na uongozi wa Yanga ameiambia shaffihdauda.co.tz aina ya soka wanalocheza wachezaji wengi wa Tanzania wakati nilipotaka kujua maendeleo ya mtanzania Juma Luinzio ambaye alikuwa naye Zesco United kabla ya kujiunga na Yanga.

Lwandamina amesema Luinzio ni mchezaji mzuri mwenye kasi lakini kwa sasa uwezo wake umeshuka na huenda ikawa imesababishwa na maisha yake ya nje ya uwanja.

“Alivyokuja alipamaba akawa vizuri hata kwenye upande wa kufunga, lakini labda kutokana na maisha ya nje ya kiwango chake kilishuka lakini bado anajitahidi kupambana kurejesha kiwango chake.”

“Wakati mwingine kiwango kinapoporomoka na ukataka kukirejesha unatakiwa kupambana zaidi ndiyo maana sio jambo zuri kupoteza uwezo wako ukiwa mchezaji ni vizuri kuhakikisha kiwango hakishuki.”

“Ni mchezaji mzuri mwenye kasi, lakini amekuwa anacheza na kupumzika na hicho kitu nimekiona kwa wachezaji wengi wa hapa wanacheza na kupumzika, mchezo wa soka unatakiwa kuwa na mwendelezo hadi dakika 90 huku kukiwa na umakini kila mmoja akishambulia na kulinda.”

“Hakuna beki wa mshambuliaji, kila mchezaji anatakiwa kuwa na akili ya kushambulia na kulinda.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>