Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

HII NDIO ADA YA UHAMISHO YA KWANZA KABISA YA CRISTIANO RONALDO

$
0
0

IMG_9525.JPG

Historia inatamja kama mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kutokea kwenye mchezo wa mpira wa miguu, akiwa na rekodi kibao mgongoni mwake ikiwemo ya kuwa mwanasoka aliyenunuliwa kwa fedha nyingi zaidi nyuma ya Gareth Bale – lakini umeshawahi kujiuliza Cristiano Ronaldo ada yake ya kwanza uhamisho ilikuwa ya kiasi gani.

  Ronaldo, ambaye alivunja rekodi ya uhamisho aliposaliwa kwa paundi millioni 80 kutoka Manchester United kwenda Real Madrid, akiwa na umri wa miaka 10 alinunuliwa na Nacional kwa jezi seti 2 na mipira ya kuchezea 20 kutoka klabu ya Andorinha.

 
Kwa mujibu wa FIFPRO, dili hili lilimpeleka Ronaldo Nacional, ambao walikuja kupata faida mara nyingi zaidi alipomuuza Ronaldo kwenda Sporting Clube de Portugal kwa Euro 22,500 mwaka 1997.

 

Thamani ya Cristiano kutoka wakati huo imeendelea kupanda kwa kasi-ambapo Man United walilipa kiasi cha 11.6 million euros mwaka 2003, na baada ya hapo wakapokea kiasi cha 94 million euro kutoka Real Madrid mwaka 2009 – na sasa akiwa mfungaji bora wa muda wote wa RealMadrid anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya €150m.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>