Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Siri ya viungo kuwa makocha bora Duniani

$
0
0

screen-shot-2016-11-29-at-8-29-36-pm

Tumeshuhudia makocha wengi wakipata mafanikio makubwa kwenye mchezo wa soka, lakini kikubwa zaidi ni wachezaji wengi ambao walicheza soka katika nafasi ya kiungo wamekuwa wanafanya vizuri katika tasnia ya ukocha.

Hapa nakudondoshea makocha kadhaa ambao enzi zao walicheza katika nafasi za kiungo lakini walipoamua kuwa makocha bado wakaendelea kupata mafanikio makubwa katika nafasi hiyo.

Mwaka 2003 gwiji wa soka duniani Jordi Cruyff alinukuliwa akikiri
kuwa, idadi kubwa ya makocha bora duniani walikuwa ni wachezaji wa nafasi ya kiungo. Bila shaka hakuna anayepinga ukweli huu kwani hata ushahidi wa makocha wanaotawala soka kwa sasa unadhihirisha hilo.

Angalia mafanikio ya muda mfupi ya kiungo wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane akiwa kocha wa Real Madrid achilia mbali utawala wa miaka saba wa kiungo wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola halafu tazama mbinu ngumu zinazotumiwa na kiungo wa zamani wa Juventus Antonio Conte huu ni ushahidi tosha kwamba, wachezaji wa nafasi ya kiungo wananafasi nzuri ya kuwa makocha wazuri baadaye.

Kama bado hujatosheka, hebu ikumbuke AC Milani ya mwaka 1990 wakati inatwaa ubingwa wa Ulaya. Nafasi ya kiungo ilikuwa na majina ya Carlo Ancelotti na Frank Rijkaard ambao wote wamekuwa ni makocha wenye mafanikio, lakini hata Roberto Mancini alikuwa anaufalme mkubwa pale Inter Milan akiwa kama kiungo wa klabu hiyo.

Nani amesahau vurugu za Diego Simone ‘Chollo’ katika eneo la kiungo wakati akiichezea Argentina na hata klabu ya Lazio ya Italia?

Siri kubwa ya mafanikio nyuma ya viungo ni kuwa, mara nyingi mchezo wa soka umekuwa ukiamuliwa kwenye eneo la kiungo. Hata pale mwalimu anapotaka kubadili mbinu, mara nyingi wachezaji wa eneo hili ndio huhusika zaidi.

Mara nyingi timu inayocheza pasi ndefu itakuwa na viungo wenye jukumu la kufanya hivyo hata timu inayocheza pasi fupi itakuwa na viungo wengi wenye sifa ya pasi fupifupi, timu inayocheza kwa kujilinda itakuwa na viungo wa ukabaji zaidi ya mmoja na kushindwa kufanikiwa kwa safu ya kiungo mara nyingi ndiko huamua matokeo ya mchezo.

Lakini wachezaji wa nafasi ya kiungo wanauwezo mkubwa wa kuusoma mchewo, hii ni sifa yao ya pili hata mkongwe Fabiio Capelo nae alikuwa ni mchezaji wa nafasi ya kiungo na sasa mkongwe huyu ni miongoni mwa makocha wenye heshima kubwa katika mchezo wa soka.

Kwa sifa hizi sitoshangaa kuona Andres Iniesta na pacha wake Xavi Hernandez kuwa makocha bora baadaye na hata kwa Steven Gerrard na swahiba wake Frank Lampard kuwa makocha wenye mbinu za kutisha duniani.

Hii ndio siri iliyopo nyuma ya viungo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>