Mbwana Samatta amefanikiwa kupiga bao mbili wakati KRC Genk ikipata ushindi wa ugenini wa magoli 3-1 dhidi ya Waasland-Beveren katika mchezo wa kuwania taji la Croky.
Samatta alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 15 kabla ya kurejea tena kambani dakika tatu kabla ya kwenda mapumziko huku bao la tatu la Genk likipachikwa wavuni na Wilfred Ndindi dakika ya 80.
Bao pekee la Waasland-Beveren likifungwa dakika ya 89 kupitia kwa Zinho Gano.