Kiungo mkabaji raia wa Zambia Justine Zulu amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga mabingwa watetezi wa taji la VPL na Azam Sports Federation Cup (FA Cup).
Zulu alikua akiichezea Zesco United ya Zambia ambayo ilikuwa chini ya kocha wa sasa wa Yanga George Lwandamina ana miaka 27 huku akiwa na uzoefu unaotokana na kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika pamoja na Afrika kwenye ligi zenye ushindani ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini.
Zulu amewahi kuvitumikaia vilabu vya National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United.
Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. October 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadae alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa.
Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012.
Wasifu wa Justine Zulu
Date of birth | 11 August 1989 (age 27) | ||
Place of birth | Lusaka, Zambia | ||
Height | 1.82 m (5 ft 11 1⁄2 in) | ||
Playing position | Midfielder | ||
Club information | |||
Current team | ZESCO United | ||
Senior career* | |||
Years | Team | Apps | (Gls) |
2005–2007 | National Assembly | ||
2007–2009 | Hapoel Be’er Sheva | 23 | (1) |
2009–2010 | Hapoel Bnei Lod | 31 | (1) |
2010–2012 | Hapoel Rishon LeZion | 50 | (3) |
2012 | Enosis Neon Paralimni | 11 | (0) |
2012–2013 | Lamontville Golden Arrows | 4 | (0) |
2013 | Kabwe Warriors | ||
2014– | ZESCO United |