Umaarufu mkubwa aliopata Cristiano Ronaldo akiwa Manchester united labda usingekuwepo tena kama mambo ambayo anazungumza Rais wa zamani wa Barcelona yangetimia.
Leo hii Ronaldo ni mchezaji hatari kwenye mechi za Real Madrid Vs Barcelona, lakini Rais wa zamani wa Barcelona Joan Laporta anasema kwamba Ronaldo ilibidi aje Barcelona.
Akielezea ishu hiyo Laporta alisema,“Wakati uongozi mpya tulivyoingia madarakani tulimsaini Ronaldinho,Marquez na Quaresma. Pia tulikua kwenye utaratibu wa kutaka kumsaini Cristiano kutoka Sporting. Agent wa mchezaji alikua ana wasiamia Marquez na Quaresma pia, alituambia pia ana mchezaji mzuri anaitwa Cristiano Ronaldo.”
“Yeye alituambia tutoe Euro milioni 2 kabla Manchester hawajatoa Euro milioni 19. Kabla hatujakamilisha kitu chochote walimaliza biashara na Manchester”.
Mechi ya El Classico inafuatia na Ronaldo amekua icon wa Real Madrid. Ingekuaje kama angekua nyota wa Barcelona leo hii ambayo ina Messi, Neymar na Suarez.?
