Wengi hasa mashabiki wa Arsenal wanaweza kuwa na kumbukumbu juu ya hali ngumu ambazo wamekutana nazo baada ya kuhama kutoka katika viwanja vyao vya awali, kumbukumbu ikiwa kutoka Highbury kwenda Emirates.
Mwezi Mei mwaka huu klabu ya West Ham nao walihama kutoka uwanja wao wa nyumbani kwenda kwenye uwanja wa Olympic uliopo Stratford na kuacha nyuma historia yao ya miaka 112 wakiwa na uwanja huo. Na sasa wapo kwenye uwanja mpya wenye kubeba idadi ya watu 60,000.
Tayari upande mdogo zaidi wa mashabiki kwenye uwanja wa Upton Park maarufu kama East Stand, ambao ulikuwa mdogo kuliko pande zote nne, tayari umevunjwa na shughuli ya uvunjaji ikiendelea kuhakikisha kuwa eneo linabadilishwa kwa ajili ya majengo ya makazi ya watu na biashara.
West Ham iliyokuwa chini ya Slaven Bilic ipo katika nafasi ya 17 ikiwa na msimu mbaya tangu kuhamia katika uwanja huo wa Olympic. Mpaka sasa wameshinda mara mbili tu katika uwanja wao huo wa nyumbani.
Uhamiaji katika uwanja huo pia umeambatana na matatizo mengi ya fujo kwa mashabiki katika michezo kadhaa, hali iliyopelekea kuongezeka kwa mbinu za ulinzi katika uwanja huo ikiwemo ongezeko la polisi.
Wagonga nyundo hao walicheza mchezo wao wa mwisho na wa kwaheri kwa uwanja huo siku waliyocheza na klabu ya Manchester United, Mei 10, katika mchezo ambao bao la Weinston Reid lilipoipa ubingwa wa mabao 3-2.
Tangu mchezo wa kwanza mwaka 1904, Upton Park umekuwa uwanja ambao umebeba historia kubwa ya klabu hiyo, ikiwemo mchezo wa nusu fainali wa kombe la washindi barani Ulaya dhidi ya Eintracht Frankfurt mwaka 1976, shindano la robo fainali la kombe la wakishinda dhidi ya Aston Villa mwaka 1980 na moja ya matukio likiwemo bao kali la Paolo Di Canio dhidi ya Wimbledon mwaka 2000.
Upton Park pia imezalisha wachezaji wengi wakiwemo nyota waliotwaa ubingwa wa Dunia Geoff Hurst, Bobby Moore na Martin Peters mpaka kipindi cha Frank Lampard na Rio Ferdinand.
Wale mashabiki waliokuwa na tiketi za msimu walipata nafasi ya kununua siti zao kabisa kwenye uwanja huu mpya.