Mchezo wa Europa League uliokuwa unaikutanisha Sassuolo ya Italia dhidi ya KRC Genk umeahirishwa kutokana na hali ya hewa kutoruhusu mchezo huo kuchezwa.
Barafu iliyokuwa ikishuka imesababishwa mchezo huo kusogezwa hadi siku ya Ijumaa.
Katika mchezo huo ulioahirishwa, mtanzania Mbwana Samatta alipangwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza.
Genk inawania kuongoza Kundi F licha ya kufuzu kucheza hatua inayofata. Genk na Athletic Bilbao zote zinapointi tisa kabla ya kucheza mechi zao za mwisho za makundi.