Simba U20 imetinga hatua ya fainali ya michuano ya ligi kuu Tanzania bara kwa vijana chini ya miaka 20 baada ya kuifunga timu ya Stand United ya Shinyanga.
Dakika 90 za mchezo huo wa nusu fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ulimalizika kwa timu zote kufungana goli 1-1.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, zikaongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika kwa matokeo ya 1-1.
Mikwaju ya penati ikabidi kutumika kumpata mshindi atakayekwenda kwenye hatua ya fainali. Simba wakaibuka washindi kwa jumla ya penati 8-7.
Simba walikuwa ni vinara wa Kundi B ambalo lilicheza mechi zake kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Stand United wao wakiwa ni washindi wa pili kutoka Kundi A lilicheza mechi zake kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.