Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Baada ya mechi ya El Classico, refa afungiwa kwa kuwa karibu na Barcelona

$
0
0

refa

Sasa hivi imethibitishwa na refa msaidizi Paul Devis amefungiwa na La Liga kutokana na kuonekana kuwa karibu sana na Barcelona kwenye mechi ya El Classico.

Baada ya mechi hiyo kutoka 1-1, Radio moja ya huko Hispania inaitwa Cadena SER ilianzisha zengwe kwamba mwamuzi huyo wa pembeni alionyesha kwa kiasi kikubwa kuwa close na wachezaji wa BArcelona kitu ambacho kileta mashaka juu ya maamuzi aliyotoa siku ya mechi.

Radio hiyo ilisema kwamba refa huyo alionekana kuongea sana na wachezaji wa Barcelona kwa karibu sana wakati wa mapumziko. Ukaribu huo na mazungumzo hayo yalionekana hadi kwenye camera za CCTV.

Real Madrid hawakupeleka malalamiko yoyote licha ya story hii kuwa kubwa kwenye vyombo vya habari vya Hispania. Siku ya Jumapili imetoka taarifa kamba refa huyu amefungiwa kuchezesha mechi kwa muda wa siku 14. Licha ya kwamba hakuna malalamiko yoyote juu ya maamuzi yake ya uwanjani lakini bado haukuwa sawa kuwa karibu na wachezaji wa timu nyingine hasa kwa mechi muhimu kama ile.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>