Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

KAGERA SUGAR MRUDISHENI MAYANJA…

$
0
0

IMG_9624.JPG

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Makocha wana ajiriwa ili kufukuzwa kazi. Wengi tunaamini kuwa ili kocha aweze kudumu katika timu moja kwa muda mrefu analazimika kuisimamia vizuri timu yake ili ipate matokeo mazuri kama si ya wastani, makocha wengi wanafukuzwa kwa sababu ya timu zao kupata matokeo mabaya. Hakuna mmiliki au klabu ambayo inapenda kufanya vibaya katika kila gemu.

Hadi kufikia raudi ya 7 msimu huu katika ligi kuu ya Tanzania bara ni makocha takribani wawili wameachishwa kazi. Wa kwanza alikuwa Fred Felix Minziro ambaye kufikia raundi ya nne timu yake ya JKT Ruvu ilikuwa imepoteza gemu zote. Coastal Union ya Tanga ilicheza mechi 6 mfululizo pasipo kupata ushindi wala kufunga goli lolote.

Kabya ya kucheza na Kagera Sugar siku ya Jumatano hii uongozi wa timu hiyo ulifikia uamuzi wa kumfuta kazi Mganda, Jackson Mayanja ambaye aliisimamia timu hiyo kwa mara ya mwisho dhidi ya timu yake ya zamani na kupata ushindi wa kwanza msimu huu. Coastal imecheza gemu saba imeshinda mara moja na kufanikiwa kupata sare ya bila kufungana katika gemu tatu, imepoteza gemu tatu na sababu kubwa ya timu hiyo kufanya vibaya ni utawala kuzidiwa na mambo mengi.

Ndani ya miezi miwili ya kampeni za urais, wabunge na madiwani nchini baadhi ya viongozi wa timu hiyo wameonekana kujikita zaidi katika mambo ya siasa na kabla ya gemu ya wiki iliyopita dhidi ya Mwadui FC, Mayanja alipigwa na ‘butwaa’ baada ya kufika uwanja wa mazoezi lakini hakukuwa na mchezaji wala kiongozi wa timu. Wachezaji waligoma kwa sababu ya kudai mishahara na hela zao za usajili. Kiujumla Mayanja alifanya makosa ya kuicha Kagera Sugar na kuichagua Coastal Union timu ambayo ‘haina mtazamo wa kufanikiwa’.

Kagera pia imekuwa na hali mbaya tangu kuondoka kwa Mlange Kabange na Mayanja. Mbwana Makatta ambaye alishinda tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita baada ya kuisimamia Tanzania Prisons katika mechi nane na kuisaidia isiteremke daraja ameshindwa kabisa kuifanya timu hiyo kucheza kwa kiwango. Si uwanja wa nyumbani tu, hadi ugenini Kagera imekuwa ikipigwa tu msimu huu.

Jumatano wamefungwa kwa mara ya tano msimu huu, imeshinda mara moja tu siku ya ufungizi dhidi ya Mbeya City na imebahatika kupata sare mara moja. Ni kweli timu hiyo imewasajili wachezaji wengi wapya lakini katika gemu 7 zilizopita zimeonesha wazi mapungufu makubwa ya timu hiyo. Tatizo la Kagera ni kocha, na mtu sahihi kwao ni Mayanja ambaye anashindwa kufanya vizuri kazi yake katika timu ya Coastal kwa sababu ya kukutana na viongozi wababaishaji.

Ningependa kuona Mayanja akirejea Kagera Sugar baada ya kutimuliwa Coastal Union kwa sababu ya kushindwa kuipa matokeo. Kagera wameangukia katika nafasi ya tatu kutoka mkiani na kama wataendelea kuamini kuwa Makatta atawapaisha watakuwa wanajiweka katika mazingira mabaya zaidi. Ushindi mara moja na vipigo vitano chini ya Makatta, Kagera mrudisheni Mayanja mtu mwenye uwezo wa kufundisha mpira.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>