Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Dkt. Msola amezungumzia issue ya wachezaji kutoa rushwa ili waitwe timu ya taifa

$
0
0

dsc_0069

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Daniel Amokachi ambaye pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, ametoa ya moyoni kuhusu suala la kupewa rushwa na mawakala ili awaite wachezaji wao kwenye timu ya taifa.

Sasa katika kuangalia hali ipoje hapa Bongo, mchambuzi wa masuala ya soka wa Clouds FM na Clouds TV amezungumza na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Dkt. Mshindo Msola kutaka kujua wakati akiwa kocha wa Stars, alishawahi kukutana na hali kama hiyo?

“Kipindi cha Cecafa 2002 kule Rwanda, walikuja mawakala wakitaka taarifa za wachezaji wawili niliokuwa nao kwenye timu, Ulimboka Mwakingwe na Faustine Lukoo. Bahati nzuri wale walikuwa ni wachezaji wangu toka Reli.”

“Sijawahi kuombwa na wakala nimchague mchezaji wake kwenye timu ya taifa ili yeye apate pesa zaidi kwa sababu mchezaji wake yupo kwenye timu ya taifa.”

“Inawezekana kwenye nchi nyingine kuna utapeli wa aina hiyo, kwa uzoefu wangu wa zaidi ya miaka nane kwenye timu ya taifa nimekutana na mawakala wengi lakini siyo kwa aina hiyo. Wengi walikuwa wanaulizia back ground ya mchezaji kwamba nilimpataje ametoka wapi kama alipita kwenye academy ili wajue wao wanaanzia wapi.”

“Kwa style yangu nilivyo na historia yangu ya elimu ilivyo si dhani kama mtu anaweza kuja kwa aina hiyo. Hata kama wangekuja kwa aina hiyo nisingekubali kwasababu sio mtu wa aina hiyo, siishi kwa mpira.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>