Kila mtu yupo kwenye mood ya Christmas na anatumia muda kuwa karibu na familia yake kwa ajili ya mapumziko. Hivyo hivyo inakua kwa sports stars na wao pia hutumia muda huu kuwa karibu na familia zao.
Hawa ni baadhi ya watu maarufu kwenye michezo jinsi walivyosherekea sikukuu ya Christmas ambayo ni siku muhimu sana kwa nchi nyingi za Ulaya na Marekani hasa wakati huu wa mapumziko.
Zlatan Ibrahimovic yeye ametuma salamu za Christimas kwa kwenda kwenye dimbwi la snow na kuanza kujiachia juu yake akiwa na boxer tu. Kwa jinsi inavyoonekana na ile snow maana yake nje kulikua na baridi kali sana kiasi lakini huyu jamaa alijitoa akili na kutoka bila nguo yoyote zaidi ya hiyo boxer. Hii hapa ni video yake akiwa kwenye snow.
Cesc Fabregas alipata mgeni ambaye amevalia kama Santa Clause, mgeni huyo ni Methieu Flamini. Bila shaka Flamini alipeleka zawadi kwa ajili ya watoto wa Fabregas ikiwa kama desturi ya pale Santa anapotembelea nyumba ya mtu wakati wa Christmas.
Barcelona star alionyesha uwezo wake wa kuoendeza na kupiga picha kali pembeni ya mti wa Christmas akiwa nyumbani kwake huko Brazil.
Club ya Liverpool na wachezaji wote walipiga picha ya pamoja wakiwa wamevaa kofia za Santa Claus ikiwa ni salamu maalum kwa mashabiki wao.
Rooney baba wa famili lazima atumie muda wake kuwa na wanae pamoja na mke wake. Hivyo ndivyo ilivyokua ambapo ali post picha akiwa na furaha pamoja na familia yake na kutuma salamu za Christmas na kusema kwamba anaamini watu wote wana enjoy siku ya leo
Philipe Coutinho na Ashley Young nao hawakua nyuma kusherekea siku yale kama unavyowaona hapo.
Mchezaji nyota wa NBA Le Bron James alipost mti mkubwa wa Christmas na kusema kwamba wakati yupo mdogo alitamani kuwa na mti kama huo hatimaye ameupata.