1; Timu moja itacheza kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya mataifa ya Africa ambayo ni Guines Bissau. Hii inapunguza idadi ya nchi ambazo hazijawai kucheza AFCON kutoka 16 hadi 15.
2; Wanaume wawili wameshinda AFCON kama wachezaji na kama makocha. Wa kwanza ni EL Gohary (1959 na 1998) na Stephen Keshi wa Nigeria (1994 hadi 2013)
3; Ghana wamefungwa mara tatu kwenye fainali za AFCON. Imefungwa na Ivory Coast mwaka 1992, Egypt mwaka 2010 na Ivory Coast tena mwaka 2015. Ghana imecheza mara 9 kwenye fainali za AFCON zaidi ya nchi nyingine yoyote.
3; Ni nchi tatu tu zimeweza kushinda AFCON mfululizo ambazo ni Ghana (1963, 1965), Cameroon (2000,2002) na Egypt (2006,2008,2010).
5; Ni rekodi ya kufunga magoli matano iliwekwa na mchezaji Laurent Pokou akifunga kwenye mechi moja dhidi ya Ethiopia. Mwaka 1970 Ivory Coast ilishinda 6-1 na yeye alipiga 5. Hadi leo bado rekodi haijavunjwa.
7; Ni idadi ya makombe yanayoshikiriwa na Egpyt. Wamechukua mara 7 wakifuatiwa na Ghana na Cameroon ambao wamechukua mara nne.
9; Ni idadi kubwa ya magoli iliyowai kufungwa kwenye mechi moja. Mechi kati ya Egypt walipata ushindi wa 6-3 dhidi ya Nigeria mwaka 1963 na kuweka rekodi hiyo.
18; Idadi ya magoli ambayo inamfanya Etoo kuwa mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli mengi kwenye michuano ya AFCON. Laurent Pokou anafuatia kwa kufunga magoli 14, Rashidi Yekini anafuatia kwa magoli 13.
23; Sekunde zilimchukua Ayman Mansour wa Egypt kufunga goli la haraka zaidi kwenye michuano ya AFCON. Alifunga goli hili mwaka 1994 dhidi ya Gabon.
36: Ni idadi ya mechi ambazo Rigobert Song amecheza kwenye michuano ya AFCON kati ya mwaka 1996 na 2010.
90; Idadi ya mechi ambazho Egypt imecheza kwenye AFCON. Nyingi kati ya hizi wameshinda ambazo ni mechi 51 na kufunga idadi ya magoli 154.