Baada ya kuwasili toka Juventus ya Italia kwa dau la rekodi ya dunia,Paul Pogba anaonekana kama hajaletwa United kuleta tu mafanikio ya uwanjani bali pia ya nje ya uwanja.Kiwango chake uwanjani kimekuwa kiking’ara siku hadi siku lakini nje ya uwanja akiingizia United fedha.Pogba ni mgodi wa fedha United kwani ndani ya wiki 3 tu jezi ya Pogba United ilishaiingizia Manchester United £190m.Pogba amekuwa gumzo na kivutio dunia nzima toka asajiliwe kutoka Juventus.Amekua akiangaliwa uwanjani uchezaji wake na hadi staili yake ya nywele.

Pogba mwenyewe alionekana kufurahia jambo hilo na kuwashukuru Twitter kupitia ukurasa wake.Hii ni muhimu sana kwa klabu ya Manchester United kuwafikia mashabiki wao,Manchester United ndio timu inayoongoza kuwa na wafuasi wengi mitandaoni,kwani hadi sasa inakadiriwa United ina wafuasi zaidi ya milioni 130 huku ikiwa na idadi ya mashabiki 659 milioni dunia nzima.Kwa mwaka jana tu Manchester United waliongoza kwa kupata wafuasi katika twitter kwa kuongeza watu milioni 3.3.
Mkurugenzi wa masuala ya mitandao wa Manchester United Richard Arnold alisema “emoji hii ni mafanikio kwetu katika masuala ya digitali na itatusaidia kimtandao kwenye mechi dhidi ya Liverpool,toka Pogba arudi kwetu amekuwa muhimu sana kama mchezaji na mtu maarufu” huku Iain Liddle mwakilishi wa twitter katika masuala ya michezo nchini Uingereza akiiongelea United kuwa timu yenye ushawishi sana katika twitter lakini pia Pogba kama kati ya wachezaji bora duniani kwa sasa ndio maana wamempa emoji.Manchester United ina watu milioni 73 Facebook,9.8 milioni katika Twitter na 15.4 milioni katika Instagram huku Pogba akiwa na 5.9m Facebook,3m Twitter na 11.9m Instagram.