Klabu ya Chelsea ya jijini London inakabiriwa na adhabu pamoja na faini kutoka kwa chama cha mpira England FA kutokana na utovu wa nidhamu uliopelekea kadi 6 za njano.
Sheria za FA ziko wazi kuhusu adhabu za kadi, na kwamba kadi sita za njano ukijumlisha na nyekundu ya Nemanja Matic, Chelsea sasa inakabiriwa na adhabu moja kwa moja.
Aidha FA inasubiri taarifa ya mwamuzi Moss aliyechezesha mchezo huo ili kupata taarifa zaidi juu ya kipi hasa kilitokea huku Mourinho pia akiwa tayari na adhabu yake mkononi kwa lugha isiyo ya kiunguana kwa mwamuzi.
Katika mchezo huo, Chelsea walifungwa goli 2-1 toka kwa Westham United zote za London na kuifanya Chelsea iendelee kubakia na points zake 11 katika nafasi ya 15.
Kocha Jose Mourinho amekalia kuti kavu hivi sasa klabuni hapo na tetesi zinasema huenda mchezo wa Chelsea dhidi ya Liverpool jumamosi hii ukaamua hatima ya Mourinho klabuni hapo endapo atapoteza mchezo huo.
Tayari Carlo Ancelloti na Guss Hiddink wanatajwa kama mbadala wa haraka kama Jose Mourinho ataondoka klabuni hapo hivi karibuni.