Kocha Arsene Wenger yupo katika matatizo na chama cha soka cha Uingereza Fa.Kocha huyo aliamriwa aende jukwaani dakika ya 92 katika mchezo wao zidi ya Burnley baada ya kuondoka katika eneo lake na kumfokea muamuzi.Ndipo muamuzi wa mchezo huo Jon Moss kumtoa nje Arsene Wenger.
Tukio la muamuzi kumtoa nje kocha huwa adhabu yake ni kocha kufungiwa mechi mbili.Lakini Wenger anaweza kukabiliwa na adhabu kubwa zaidi kwani baada ya Jon Moss kumuamuru aende jukwaani Arsene Wenger alifanya tukio lingine kwa kumsukuma muamuzi wa pembeni.
Wenger akiwa kwenye njia ya kwenda vyumbani alionekana kubishana na Anthony Taylor ambae ni muamuzi wa pembeni.Mbaya zaidi kwa Mfaransa huyo ni tukio lake la kumsukuma Taylor.Sheria za soka zinakataza kwa mchezaji ama mtu yeyote wa benchi la ufundi kumsukuma au kupeleka mikono yako kwa muamuzi na hii huwa ina adhabu yake ni kufungiwa mechi kadhaa.
Sasa kwa hili hii Wenger anaweza kufungiwa mechi zaidi ya mbili.Kosa la kwanza kutoa lugha isiyofaa kwa muamuzi kosa ambalo huwa wanafungiwa michezo miwili.Kosa la pili kumsukuma muamuzi wa pembeni.Hii itampelekea Wenger kuukosa mchezo wao zidi ya Chelsea tarehe 4 mwezi ujao.