Star wa soka ambae alifanya vizuri sana akiwa na club ya Arsenal kwenye EPL na baadae kwenye club nyingine amekua balozi wa Startimes kwa bara Africa kuanzia October 29 hadi miaka 3 ijayo.
Startimes inatoa huduma zake Nigeria, Tanzania, Mozambique, South Africa, Kenya, DRC, Uganda na kwingineko. Hivyo basi Kanu atahusika kwenye uchambuzi wa baadhi ya mechi ambazo zitaonekana kwenye king’amuzi cha Startimes.
Pia Kanu atashirikiana kwa ukaribu na Jonathan Akpoborie ambae ni mchezaji wa zamani wa Nigeria aliyetumia muda wake mwingi kucheza soka la kulipwa kwenye ligi ya Bundesliga.
Executive Officer wa StarTimes Nigeria, Mr. Jack Liu akielezea kwanini Kanu ndie amekua balozi alisema hivi,”Kutokana na mafanikio ya Kanu kama mchezaji wa kimataifa, umaarufu wake haushii Nigeria tu. Pia mafanikio yake yanaonyesha story halisi ya kiafrica, kupata mafanikio kutoka mbali na kuvuka vikwazo vingi. Kanu ni star ambae mastar wa baadae wanaweza kujifunza kwake”
Jack aliongeza, “Kwenye ulimwengu wa digital TV, Startimes tuna lengo la lengo la kutoa huduma na kufanya uwekezaji sahihi kwa Nigeria na Africa nzima.Tunajitahidi kuwahamasisha watu wengi wajiungana na kuwahamasisha kwa kuboresha huduma ya Startimes.”
Kanu pia aliongeza hivi,”Nina furaha ku-support na kuhamasisha StarTimes kama balozi wa Africa, lengo langu ni kuona Africa imejiungana digital TV ikfika June 17, 2017. Nikiwa kama balozi wa Startimes naamini tutafanikiwa hili,”