Baada ya kuangukia pua vibaya mbele ya Cleveland Cavaliers katika mechi yake ya ufunguzi, timu ambayo siku zote imekuwa ngumu na bora sana, Memphis Grizzlies usiku wa leo imepata ushindi mbele ya Indiana Pacers.
Memphis Grizzlies ilipata ushindi wa pointi 112-103 za Indiana Pacers.
Wachezaji saba wa Memphis walifunga wingi wa pointi zaidi ya kumi kila mmoja. Mike Conley alifunga point 13 na kutoa pasi 10, Zack Randolph alifunga point 11 na rebound 8, Marc Gasol yeye aliongeza point 20 kwa Memphis Grizzlies.
George Hill aliiongoza Pacers akifunga pointi 20 huku Paul George akimaliza na pointi 18, rebounds nane na pasi tano huku Pacers ikianza msimu kwa kupoteza michezo 2 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita .
Muda mfupi kabla ya mchezo , maafisa wa ligi walitangaza kuwa Paul George alikuwa amelimwa faini ya dola za kimarekani elfu kumi ($ 10,000 ) kutokana na kitendo chake cha kukosoa waamuzi hadharani baada ya mchezo wa Jumatano Indiana ikipoteza 106-99 mbele Toronto.
HIGHLIGHTS