Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

UNAZO BILIONI 30 ZA MADAFU? MUONE JORDAN AKUACHIE MJENGO WAKE WA CHICAGO, NA AIR JORDAN MATOLEO YOTE ZILIZOSAINIWA

$
0
0

 

jumba la kifahari la Michael Jordan
jumba la kifahari la Michael Jordan

Mjengo wa kifahari wa Michael Jordan wuliopo kwenye eneo la futi 56,000 za mraba sawa na mita 520 za mraba umekuwa ukiwekwa sokoni kwa kipinid cha  takribani miaka mitatu sasa.

Na inaonekana nyota huyo wa mpira wa kikapu wa zamani pamoja na mawakala wake wa mali isiyohamishika wamechoka vya kutosha.Kupunguzwa kwa bei ya jumba hilo mara kwa mara hakujasaidia .

Jumba hilo limekuwa likiwekwa sokoni mara kwa mara na ilikuwa tangu mwaka 2012 ambapo bei ya kuuza ilikuwa dola za kimarekani milioni 29 ( $ 29,000,000)  na sasa  bei imekwenda ikishuka na ipo chini kwa takribani nusu ya iliyopita yaani dola milioni kumi na nne na laki tisa ($14,900,000) .

Awali iliwekwa mnadani takribani mara mbili na hakutokea mteja wa kuichukua. Mkakati mpya ni mkubwa na kampeni ya kuiuza inaonekana imepangwa kimaarifa safari hii . Njia za masoko ni pamoja na marejeo ya mmiliki wake maarufu , na kupendekeza kuwa jengo hilo lina hadhi kama Jordan mwenyewe.

Jambo la kufurahisha Wakati huu ni kuwa mnunuzi wa ilo jumba atapata jozi za viatu za kila Air Jordan iliyoingia sokoni saizi sawa kabisa na mguu wa mnunuzi na zenye saini ya Michael Jordan.

Baadhi ya yaliyomo kwenye nyumba hiyo ni Swimming Pool ya maana, uwanja wa golf, uwanja wa basketball, chumba cha kisasa cha mazoezi yaani gym, mabafu 15, garage yenye parking ya magari 15, vyumba 9 vya kulala, maktaba na mengine mengi.

PICHA ZA MJENGO WA MICHAEL JORDAN NDANI NA NJE
28B8F17700000578-3083645-No_Sale_The_basketball_star_hasn_t_had_any_luck_selling_the_nine-a-53_1431722188546 f images

Michael Jordan’s Highland Park Estate
Michael Jordan’s Highland Park Estate

tumblr_inline_mvvhznx6JP1qgw1en

 

VIDEO INAYOONYESHA NYUMBA HIYO IKINADIWA

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>