
Kocha mturuki Memik Vurucu wa Jang’ombe Boys ya Zanzibar atalazimika kurudi nyumbani kwao Istanbul, Uturuki kwa ajili ya shughuli muhimu, akizungumza na mtandao huu rais wa Jang’ombe Boys Ally Othman Kibichwa, amesema kocha wao ataelekea Uturuki kwasababu mji wa Istanbul unabomolewa na kujengwa upya hivyo, lazima aende akasaini sehemu yake anakoishi.
“Sisi klabu ya Jang’ombe Boys kwa masikitiko, siku ya Ijumaa tukimaliza mechi mwalimu wetu ataondoka kwenda nyumbani kwao Istanbul kwasababu mji wao unabomolewa kwahiyo kuna fomu atakwenda kujaza ili kurekebisha mji”, amesema Kibichwa.
“Kwa maana hiyo anatarajia kama mpira utakuwa unachezwa, baada ya wiki mbili au mwezi mmoja atakuwa amerejea”.
Baada ya kuulizwa kama wanatumia mwanya huo ili kuachana na kocha huyo kutokana na kushindwa kumhudumia Memik Vurucu alisema: “Sisi kama Boys tungeulizwa tuletewe pesa au kocha, sisi tungechagua pesa. Lakini sasa kocha tumeletewa mkataba nae sisi hatuna wanao hao ambao wamemleta na hao ndio wamemtumia nauli aende kwao akafanye mambo ya majengo”.
“Kwahiyo hata wakituambia hawamleti au wanamleta yote sawa kwasababu sisi tumesaidiwa tu kocha. Laki sio klabu ya Jang’ombe ambayo ilitangaza ‘tender’ ya kutafuta kocha”.
“Hao waliomleta wamempatia makazi na usafiri wenyewe, sisi kazi yetu ni kumlea na kumtunza”.
“Kocha wa Jang’ome Mimic Voloue aliwasili visiwani Zanzibar na kupokelewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo lakini kutokana na ligi ya Zanzibar kusuasua kutokana na kushindwa kuchezwa kufuatia kuwepo kwa kesi mahakamani kwa muda mrefu kabla ya kesi hiyo kuondoshwa mahakamani na kuruhusiwa ligi hiyo kuchezwa”.