Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

EXCLUSIVE: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAWEZA, KIKUBWA NI JUHUDI, MALENGO NA KUJUA UNATAKA NINI-SAMATTA

$
0
0
Mbwana Samatta muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mbwana Samatta muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Nyota wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewasili nchini leo asubuhi tayari kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria siku ya Jumamosi kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2018

Samatta na Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi wakitokea Nairobi, Kenya ambako walikwama jana kutokana na ndege yao kuzuiliwa kuruka kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri.

Mtandao huu umefanya mahojiano maalumu na Mbwana Samatta muda mfupi bada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania kutaka kujua mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mafanikio yake katika soka.

Shaffihdauda.co.tz: Unawaambia nini wachezaji wa Tanzania ambao wanatamani kufikia mafanikio uliyoyapata wewe?

Samatta: Wanaweza, wachezaji wa Tanzania wanaweza kikikubwa ni juhudi, malengo na kujua unataka nini. Kujituma kunaweza kukufikisha mbali zaidi hasa pale unapokuwa na nia ya dhati.

Shaffihdauda.co.tz: Umepata mafanikio makubwa lakini mama yako mzazi hajashuhudia mafanikio haya, una-miss nini kutoka kwake?

Samatta: Nam-miss yeye, ingekua vizuri zaidi kama angekuwepo ili ashuhudie hiki kinachoendelea

Shaffihdauda.co.tz: Kabla ya mchezo wa marudiano wa fainali ya klabu bingwa Afrika kati ya Mazembe na USM Alger, Katumbi alikwambia kitu gani kabla hujaingia uwanjani?

Samatta: Kabla sijaingia uwanjani hakuniambia kitu lakini baada mechi kumalizika alinipongeza pamoja na timu nzima kwa kutwaa ubingwa na mimi kuwa mfungaji bora wa mashindano kwa mwaka huu.

Shaffihdauda.co.tz: Kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Algeria mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2018, watanzania watarajie nini kutoka kwako?

Samatta: Tumekuja kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria, tunafahamu Algeria ni timu bora na ngumu barani Afrika, lakini tukishirikiana naamini tunaweza kufanya vizuri kwenye mechi ya nyumbani. Pia naamini mwalimu atakuwa ameiandaa timu vizuri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria.

Shaffihdauda.co.tz: Hakuna viongozi wa serikali ambao wamekuja kukupokea na kukusapoti kwa mafanikio uliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuiletea heshima kubwa Tanzania pamoja na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yako ukiwa ugenini, unajisikiaje kwa hili?

Samatta: Hawa watanzania waliojitokeza kuja kunipokea wanatosha sana kwangu, na hili ni jambo zuri pia.

Wakati huohuo, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kuwasili leo jioni ikitokea Afrika Kusini ambako ilikuwa imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa kutafuta nafasi ya kushisiriki fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi mwaka 2018. Stars itafanya maandalizi ya mwisho ikiwa na kikikosi kizima wakiwemo Samatta na Ulimwengu ambao wamewasili leo, kabla ya kuwakabili Algeria siku ya Jumamosi November 14.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>