Mario Chalmers ghafla amepitia mageuzi kutoka mmoja wa wachezaji wengi waliopitua maisha ya kudharauliwa katika uwanja wa Memphis. Lakini imemchukua michezo mitatu tu kugeuka kuwa moja ya wachezaji walioshangiliwa kwa nguvu kubwa.
Chalmers alifunga 16 ya pointi zake 29 katika robo ya nne na kuisaidia klabu yake mpya ya Memphis Grizzlies kuibuka na ushindi mtamu wa 122-114 dhidi ya Oklahoma City Thunder.
Huku Chalmers akiwa katika kiwango bora katika robo ya mwisho , mashabiki wa Memphis , walikuwa wima wakishangilia anachokifanya mchezaji huyu aliyepatikana wiki iliyopita katika biashara na Miami Heat .
Shabiki mmoja akatamka wazi : ” kamwe sikuwahi kufikiri kama ningekuja kumshabikia na kumshangilia Mario Chalmers . ”
Kabla ya biashara, Chalmers alikuwa anajulikana sana Memphis kama mtu ambaye pointi 3 yake alofunga 2008 katika michuano ya kitaifa ya ubingwa wa basketball katika mchezo dhidi ya Memphis Tigers na kuipeleka katika dakika za nyongeza na hatimaye alishinda kwa timu ya Chalmers ‘ ya Kansas Jayhawks kuibuka mshindi.
Mike Conley alikuwa na pointi 22, Jeff Green alifunga 20 , wakati Marc Gasol aliongeza 17. Zach Randolph alimaliza na pointi 12 na rebounds 10.
Russell Westbrook aliiongoza Thunder na pointi 40, 12 zikiwa katika robo ya nne huku akijaribu kuileta Oklahoma City kutoka nyuma ya 11. Serge Ibaka alikuwa na pointi 18 na Enes Kanter alifunga 16. Steven Adams na Dion Waiters walimaliza na pointi 14 kila moja.
Memphis Grizzlies pia walifanya throwback kwa kuvaa Aina ya jezi walizotumia mpaka msimu wa 1974-75 kipindi hicho ligi ya NBA ikifahamika kama ABA.
Kwa wapenzi wa kikapu watakumbuka kipindi hicho ilikuwa inaitwa Memphis Sounds kabla ya kupitia mabadiliko kadhaa ya kuuzwa kutokana na matatizo ya kifedha mpaka miaka ya 2000 ilipozaliwa Vancouver Grizzlies na baadae kubadilika jina kuwa Memphis Grizzlies.
Hii ni mara moja kati ya nane ambazo timu hiyo imepanga kuvaa kumbukumbu ya jezi hizo, na zitagawanywa katika makundi ya Nyeupe na Nyekundu.
HIGHLIGHTS