Brooklyn Nets wameifunga Atlanta Hawks kwa point 90-88. Kabla ya mchezo wa leo, Brooklyn walikuwa wamepoteza michezo 6 dhidi ya Atlanta. Ushindi wao wa mwisho ukiwa ule wa January 26, 2014.
Mpaka sasa wakiwa na rekodi ya kufungwa michezo 9 huku wakishinda 2, ni rekodi mbovu zaidi tangu mwaka 2010 walivyopoteza michezo 18.
Mchezaji Joe Johnson wa Brooklyn Nets ameweka rekodi ya NBA kwa kufunga kikapu walau kimoja katika michezo 895 mfululizo.
Pia point 3 zake mbili, zimemaanisha kuwa anapanda mpaka nafasi ya 12 kwa wachezaji waliopata mitupo mingi zaidi ya point 3 akiwa amefikisha 1720.
Ijapokuwa Cleveland Cavaliers wamepoteza mchezo wao dhidi ya Detroit Pistons, lakini LeBron James kaweka rekodi mpya.
Katika robo ya kwanza alifunga mtupo wa point 3 uliomfanya kutoka nafasi ya 20 mpaka ya 19 katika wafungaji wa Muda wote akimpita Jerry West. Amefikisha point 25193.
LeBron alimaliza na point 30 na kufikisha mchezo wa nne mfululizo msimu akiwa na walau point 30.
Mchezaji wa New York Knicks kinda huyu, Kristaps Porzingis amefunga point 29 na Rebound 11 katika ushindi wa New York Knicks dhidi ya Charlotte Hornets. Anakuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kupata walau point 25 na Rebound 10 katika Historia ya Knicks.
Ikumbukwe mchezaji huyu alikosolewa sana Rais wa New York Knicks katika kumchagua kwake msimu huu katika NBA Draft. Lakini anaonekana kuwaprove wrong watu.
Mchezaji Kevin Garnett leo katika ushindi wa Minnesota Timberwolves dhidi ya Miami Heat alifikisha michezo 66 akicheza dhidi ya timu hiyo.
Ameungana na Reggie Miller katika nafasi ya 5 kwenye orodha ya wachezaji waliocheza michezo mingi dhidi ya Miami Heat. Wengine ni Paul Pierce (77), Allan Houston (68), Patrick Ewing na Charles Oakley wote wakiwa na 67.
Minnesota walishinda 103-91.