Hata kama wakiwa hawakucheza mchezo wao uliozoeleka na kiwango cha chini, Golden State Warriors imeweza kudumisha muendelezo wao uliokuwa bora.
Stephen Curry alifunga pointi 37 na kuisaidia Golden State Warriors ambao ni mabingwa watetezi wa NBA kupata ushindi wa 12 mfululizo tangu kufunguliwa kwa msimu.
Ilikuwa mechi ngumu ambayo Golden State Warriors waliibuka na ushindi 115-110 dhidi ya Toronto Raptors Jumanne usiku. Klay Thompson aliongeza pointi 19 na Andrew Bogut alifunga 13 kwa Warriors, kuchagiza rekodi bora katika NBA tangu Dallas iliposhinda michezo yake 14 ya kwanza katika msimu wa 2002-03.
Golden State Warriors inahitaji ushindi mara tatu kuweka na kufikia rekodi ya ligi ya 15-0 , iliyowekwa msimu wa 1948-49 na Washington capitols na 1993-1994 ilipowekwa na Houston Rockets.
Kuanza msimu kwa 12-0 inamaanisha pia wamefungana rekodi na Chicago Bulls ya msimu wa 1996-1997 kwa rekodi ya pili bora kwa kuanza kwa msimu kwa mabingwa watetezi , nyuma tu ya Boston Celtics ya msimu wa 1957-58 ( 14-0 ).
Stephen Curry anaongoza NBA akiwa na pointi 404 katika msimu huu ikiwa ni pointi 101 zaidi ya anayemfuatia kwa karibu, mchezaji wa Portland Trail Blazers, Damian Lillard.
Lowry na Demar DeRozan walifunga pointi 28 kila moja kwa Raptors , ambao wamepoteza michezo mitano kati ya saba ikiwa ni baada ya kuanza msimu kwa ushindi wa 5-0.
HIGHLIGHTS