Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

KASEJA KULAMBA DILI JIPYA

$
0
0

MBETA

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Klabu ya Mbeya City FC itampa mkataba wa mwaka mmoja na nusu mlinda mlango wake Juma Kaseja I Juma ambaye mkataba wake wa miezi sita unataraji kumalizika mwezi ujao. City ilimsaini kipa huyo mshindi mara 6 wa ligi kuu Bara katikati ya mwaka huu kama mchezaji huru itamuongezea mkataba nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars baada ya kulidhishwa na uwezo wake.

“Tangu alipojiunga katika timu yetu Kaseja amekuwa ni mtu mwenye mchango ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja pia. Amecheza zaidi ya mechi Tano na kufanya vizuri. Ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu, mchapa kazi na amekuwa akiwasaidia wachezaji vijana pia kwa ushauri na mafunzo madogo madogo kiuchezaji.” Anasema mtu wa ndani wa klabu hiyo ya ‘ Kizazi Kipya’ ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa timu hiyo

“Tutamuongezea Kaseja mkataba wa mwaka mmoja na nusu kama mazungumzo yetu yatakwenda vizuri.” Kaseja alianza kucheza ligi kuu mwaka 2001 akiwa na klabu ya Moro United ambayo wakati huo makao yake makuu yalikuwa mkoani Morogoro. Alijiunga na Simba mara baada ya kuichezea Mtibwa Sugar pambano la nusu fainali FA Cup dhidi ya Yanga SC, December, 2002.

Aliichezea Simba hadi katikati ya mwaka 2008 na kuisaidia kushinda mataji matatu ya ligi kuu. Alijunga na Yanga ambako alishinda pia ubingwa wa ligi msimu wa 2008/09 na kurejea Simba ambako alicheza kwa misimu mingine mitatu na kushinda mataji mawili ya ligi. December, 2013 alijiunga kwa mara ya pili na klabu ya Yanga kabla ya kutibuana msimu uliopita na kipa huyo akajiondoa baada ya michezo 7 tu kuchezwa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>