Wade alifunga pointi 24 na Miami Heat kuwapiga Sacramento Kings 116-109 Alhamisi usiku ,huku wakitumia faida ya Sacramento kumkosa nyota wao DeMarcus Cousins baada kusimamishwa mchezo mmoja.
Chris Bosh alikuwa na pointi 23 na 11 rebounds , na Tyler Johnson alikuwa na pointi 19 na kuisaidia Miami kupata ushindi kwa mara ya nne katika mechi tano .
“Haikuwa moja ya michezo yetu bora ya kujilinda ndani ya msimu huu, lakini kuna baadhi ya utekelezaji bora wa baadhi ya mambo ambayo tumekuwa tukijifunza kiushambuliaji , ” kocha wa Miami Heat Erik Spoelstra alisema.
Mchezaji wa Sacramento Kings, Rajon Rondo alikuwa na takwimu za juu za msimu kwenye pasi kwa kutoa pasi 18, huku pia akimaliza na pointi 14 na rebounds 9. Hii ikiwa ni baada ya Triple doubles katika michezo yake ya awali minne.
“Nadhani mchezo wake ni wenye kutia moyo sana na chanya kwa kila mtu,” kocha wa Sacramento Kings George Karl alisema. ” Yeye hufanya kila mtu kwenye timu yake awe bora . Yeye hufanya mchezo mliopanga kutokea.”
Rondo ana wastani wa pointi 14.2 , pasi 14.2 na 9.8 rebounds katika michezo yake mitano iliyopita.
TAKWIMU
Sacramento ina matokeo mabovu ya 3-25 katika uwanja wa Miami. Kings ‘ walipata ushindi wa mwisho katika uwanja wa Miami hii ilikuwa Novemba 10, 2001 .
Wakati Wade akicheza , Miami ina matokeo chanya ya 11-0 katika mechi za nyumbani dhidi ya Wafalme (Kings) hawa wa Sacramento na 18-1 ujumla dhidi yao.
HIGHLIGHTS