
Uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa kisoka wa Temeke, umezuiwa kwa agizo la mahakama kutokana na Sud Mlilo kupeleka malalamiko mahakamani dhidi ya baadhi ya viongozi wa vyama vya soka wanaosimamia uchaguzi huo.
Mtandao huu umezungumza na Rashid Sadala ambaye ni mwenyekiti wa uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ili kujua kilichopelekea uchaguzi huo kusitishwa na utafanyika lini baada ya kuzuiwa.
“Ni kweli agizo la mahakama limezuia uchaguzi kufanyika, imezuia kwasababu kuna mtu amefungua shauri pale akimshtaki mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TEFA, mweniki wa kamati ya uchaguzi ya DRFA ambaye ni mimi na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Bw. Aloyce Komba kwahiyo kunamadai ya msingi ambayo inabidi yasikilizwe kwanza na mahakama halafu mahakama itatoa uamuzi ni lini uchaguzi ufanyike lakini kwa sasa uchaguzi umezuiwa mpaka hapo mahakama itakapolisikiliza ombi la aliyeshitaki”, amesema Sadala.
Uchaguzi wa TEFA ulikuwa ufanyike Jumapili November 22, 2015 lakini umezuiwa na haifahamiki utatangazwa kufanyika lini. Uchaguzi huo umekuwa ukipigwa danadana kutokana na sababu mbalimbali lakini nyingi zikiwa za kutoelewana kati ya wagombea na wanaosimamia uchaguzi huo.