Neymar na Luis Suarez waliendelea na rekodi yao bora ya ufungaji msimu huu wakiiangamiza RealMadrid na kuendeleza wigo wa pointi kufikia 6.
Pengine sasa Barcelona inathibitisha ubora wake kwa vilabu vya ulaya na sio Real Madrid pekee hata kama inamkosa Lionel Messi huku Neymar akionekana kukomaa na kuwa tayari kubeba majukumu. Barcelona ikiiangamiza Real Madrid 4-0 katika uwanja wake nyumbani yaani Santiago Bernabeu.
Messi alikuwa tu fit na kutosha kuanzia katika benchi la Barca baada ya kurejea kutoka katikamajeruhi yaliyomweka nje kwa takribani miezi 2 baada ya kupata jeraha la goti.
Lakini Neymar na Suarez waliendelea kuwa katika fomu zao nzuri na kipindi cha wakafunga mawili kabla Iniesta na Suarez hawajaongeza mbili zaidi baada ya mapumziko.
Suarez alifunga bao kwa upande wa Luis Enrique ya dakika 11, Madrid hawakuweza kukabiliana na harakati za Barca , na Neymar akafanya yake na kuongeza la pili dakika sita baadae.
Barca alimanusura waongeze latatu katika kipindi cha kwanza dakika za majeruhi baada ya Neymar kufanya kazi kubwa na kumuwekea Suarez ambaye hata hivyo alishuhudia Marcelo akiokoa juhudi zake za kutaka kuweka mpira wavuni.
Ni kama Madrid hawakukaa sawa wakiwa wameanza kwa kasi kipindi cha pili, kwani Iniesta aliwanyamazisha kwa kuongeza bao latatu mapema kipindi cha pili dakika 54.
Iniesta alifunga goli lake la kwanza msimu huu, na pia lakwanza tangu Machi 2014 ambapo alifunga pia dhidi ya Madrid. Suarez alimaliza kazi dakika ya 74 kwa kufunga goli la 4-0. Isco alishuhudia kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika 5 mpira kumalizika.
JE HII NI BYEBYE KWA RONALDO?
Ni ngumu kusema ndio moja kwa moja lakni kutokana na mienendo ya karibuni ya mchezaji huyo na namna anavyochezeshwa ni wazi kuwa unaweza kubet kuwa maisha yake sio marefu ndani ya Bernabeu.
Ronaldo kashinda kila kitu akiwa pale Los Blancos, kaweka rekodi anazotaka ndani ya misimu takribani sita, na hivi Paris Saint Germain wapo tayari kuvunja benki na kumpa mshahara uliokithiri yote yanawezekana.
Inasemekana kelele za kuzomea usiku wa jana yaani Boos zilimlenga yeye. Lakini Madrid panabaki kuwa nyumba ya kifalme, wanaweza kufika dau lolote. Kama James Rodriguez na Bale hawatolipa magoli, basi kumuondoa huyu mapema ni ngumu.
HIGHLIGHTS