Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

HAWA NDIO WANAUME WANAOMNYAMAZISHA ROONEY NA TAIFA LAKE KWA REKODI ALIYOIWEKA JUZI

$
0
0

Thomas MullerNa Salym Juma

Wiki hii vyombo vingi vya habari vya Uingereza na mataifa yote yaliyo chini ya jumuiya ya madola yalitawaliwa na habari moja pekee. Nadhani kwa unayefuatilia michezo utakuwa una fahamu kuwa stori ya Wayne Rooney kufikisha magoli 50 na hatimaye kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye taifa lake ndiyo iliyotawala hadi watu kusahau habari za Lowasa na Magufuli. Binafsi nilidhani Rooney hakupaswa kujisifia kwani kuna watu wa kizazi chake kutoka nchi zingine ambao wamefanya makubwa na wanatarajiwa kuitikisa dunia kwa kufunga magoli mengine mengi ndani ya miaka ijayo kama Mwenyezi atawaepusha na majeraha.

Rooney ana miaka 12 kwenye uzi wa timu ya taifa lake huku akiwa na magoli 50. Huu ni wastani wa magoli 4 kwa mwaka huku yeye akiwa na faida ya kuitwa mara zote tangu 2003 na kutofungiwa mara kibao kama akina Suarez. Rooney kwa sasa ana miaka 29 na kutokana na kutotabirika kwa kiwango chake inawezekana akacheza misimu 4 ijayo kwenye taifa lake hivyo kuwa na magoli 16 na hatimaye kustaafu akiwa akiwa na magoli yasiyozidi 65. Naamini baada ya kutoka Urusi kwenye kombe la dunia mwaka 2018, Rooney atastaafu.

Pia Rooney atakwenda Urusi akiwa tayari yupo hoi katika idara ya ushambuliaji na huenda akaenda kama kiungo na sio mshambuliji, hii ni kutokana na uwepo wa vijana kama akina Kane, Sturidge na Sterling. Kutokana na Waingereza kujisifia kwa kitendo cha Rooney leo nakupa ushahidi wa wachezaji 5 wa kizazi cha Rooney ambao wamefanya makubwa na takwimu zinaonesha watafanya makubwa sana miaka ijayo kabla hawajastaafu na kudhihirisha taifa la Uingereza lina mpira wa
magazetini na kwenye ngazi ya kimataifa bado sana……..

LIONEL MESSI

Ni mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, kwa sasa ana miaka 28. Alianza kuonekana kwenye uzi wa timu ya taifa ya Argentina tangu mwaka 2005 hivyo hadi sasa ana miaka 10 kwenye timu yake ya taifa. Kwa sasa ana jumla ya magoli 49 katika michezo 105 aliyocheza. Ukipiga hesabu hapo jamaa ana wastani wa kufunga magoli 5 kila mwaka. Kwa kiwango chake ni wazi kuwa jamaa bado ana miaka 6 ya kucheza kwenye timu ya taifa, kwa wastani huu wa magoli 5 kwa mwaka, Messi atafunga magoli yanayokadiriwa kufika 30 kwenye miaka yake ijayo ya kucheza soka hivyo kustaafu akiwa na magoli takribani 80.

Kama hatoandamwa na majeraha inawezekana Messi akaonekana kwenye timu ya taifa lake akiwa na miaka 34 japokuwa hatopewa nafasi ya mara kwa mara ila bado ataitwa kama mkongwe wa kikosi. Takwimu hizi zinazidi kumdidimiza Rooney na Uingereza kubakia kama taifa la kawaida sana kisoka.

NEYMAR JUNIOR

Ni mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Santos ila kwa sasa anakipiga pale FC Barcelona. Neymar ameanza kuonekana kwenye timu ya Selecao tangu mwaka 2010. Kwa sasa ana miaka 23 ila tayari amecheza michezo 67 pekee huku akifunga magoli 46. Kwa hesabu za haraka ni kwamba jamaa ana wastani wa magoli 9 kila mwaka. Ni wastani mkubwa sana kwa kizazi cha leo kwani kutokana na uwezo wake mkubwa, Neymar bado ana miaka takribani 10 ya kuonekana kwenye uzi wa Njano na Bluu. Kwa wastani wake wa magoli 9 kwa mwaka, Neymar anakadiriwa kutupia magoli
yasiyopungua 90 miaka ijayo.

Kutokana na majeraha na umri kusogea hivyo kiwango kushukuka tuna ‘assume’ Neymar atafunga nusu ya magoli hayo, 45. Magoli haya bado ni mengi sana, kitu ambacho Waingereza wataendelea kukiota hadi kesho na kudhihirisha wamezidiwa kisoka na mataifa mengine duniani.

THOMAS MULLER.

Ni mchezaji anayecheza kwa jihadi sana uwanjani. Kwa sasa yupo pale Bayern Munich na kwa upande wangu huyu ndio mchezaji bora wa Bayern kwa sasa kutokana na moyo wake wa kujituma na kucheza kwa jihadi. Muller ana miaka 25 na alianza kuonekana kwenye timu ya taifa tangu 2010. Hadi sasa amecheza michezo 65 huku akitupia magoli 30. Jaribu kupiga hesabu utagundua jamaa ana wastani wa kutupia magoli 6 kila mwaka. Umri wake utamruhusu kucheza miaka 8 ijayo kama hatopata majeraha. Kwa wastani huu ni wazi Muller anatarajiwa kufunga magoli yasiyopungua 48 na hatimaye kustaafu akiwa na magoli yasiyopungua 80.

Kutokana na uwezo wake naamini Muller atayafikia haya magoli mapema kabla hajatundika daluga. Muller pia anatarajiwa kuvunja rekodi ya Miroslav Klose ya kuwa mfungaji wa kombe la dunia wa muda wote. Kitendo hiki kitazidi kuonesha kuwa Ujerumani ni taifa lililoiacha mbali Uingereza katika ngazi ya kimataifa.

LUIS SUAREZ

Ni mshambuliaji namba 9 hatari kwa sasa duniani ukimuacha Kuni Aguero. Huyu jamaa alifungiwa mechi kibao kutokana na tabia yake isiyotabirika. Suarez kwa sasa ana miaka 28 na ameshacheza michezo 82 huku akifunga magoli 43. Alianza kuonekana kwenye timu yake ya taifa tangu mwaka 2007. Ukikokotoa vizuri utagundua jamaa ana wastani wa kufunga magoli 5 ila wastani huu utakuwa ni wa kumuonea kwani amekosa mechi kibao kutokana na kufungiwa na FIFA. Kama tabia mbovu na majeraha havitomuandama, ni wazi kuwa Suarez ana miaka 6 ya kucheza Uruguay kama walivyofanya nyota wengine wa Uruguay hapo nyuma.

Kutokana na wastani wake wa kutupia magoli 5 kwa mwaka, Suarez anakadiriwa kufunga magoli yasiyopungua 30 kipindi kijacho hivyo kufikisha magoli karibu 80. Kama atakuwa vizuri kiafya, rekodi hii itatimia kwani huyu jamaa ni hatari sana akicheza kati. Hali hii itazidi kudhihirisha kuwa Waingereza wana mpira wa magazeti na kwenye ngazi ya kimataifa wanazidiwa na taifa dogo kabisa kama hili.

CRISTIANO RONALDO

Hii ni mashine ya kutoa magoli. Jamaa anafunga pale anapoamua kufunga. Ni hatari sana hasa pale anapocheza na timu yangu na huwa nachukia sana akipewa pasi kwani ameshanichania ‘mikeka’ kibao. Kwa sasa yupo Real Madrid na ana miaka 30. Ameshacheza michezo 122 tangu 2003 kwenye timu ya taifa lake huku akitupia magoli 55. Kwa hesabu za kugawanya utagundua huyu jamaa ana wastani wa magoli karibu 5 kwa mwaka. Ronaldo bado ana miaka 4 ya kucheza timu ya taifa kama hatotangaza kustaafu mapema. Kutokana na wastani huu ni wazi CR7 anatarajiwa kufunga magoli yasiyopungua 20 baada ya kombe la dunia nchini Urusi.

Kutokana na moyo wake wa kujituma na nidhamu nzuri aliyonayo, nina imani fundi huyu atatimiza magoli 70 hadi 80 kwenye taifa lake na kumkalisha Rooney na taifa lake ambalo soka lao limebaki kwenye magazeti.

saijuzedoctor@gmail.com


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>