Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

RAPPER YOUNG KILLER AMTAJA MSHINDI WAKE WA BALLON D’OR…AKILI KUWA SHABIKI WA MCHEZAJI HUYU.

$
0
0

kill

Hivi sasa moja ya topic kubwa ni kuhusu tuzo ya Ballon D’or na kila mtu anajaribu kutoa sababu zake kuhusu nani atakua mshindi wa tuzo hii.

Kama ulikua hujui ni kwamba rapper Young Killer aliwai kucheza soka kwenye academy ambayo ilikua inasimamiwa na marehemu Mash huko Mwanza kabla hajaanza kuchana Hiphop.

Kuhusu nani atashinda Ballon D’or Young Killer amesema, “Mimi ni shabiki mkubwa Cristiano Ronaldo lakini kwenye swala la msimu uliopita hadi sasa hivi kwenye Ballon D’or mshindi wangu ni Lionell Messi. Huwezi kuzungumzia ubingwa Barcelona bila kumtaja Messi. Pia japokua timu yake ya taifa haijashinda hadi kushinda makombe lakini mchango wake ni mkubwa kwenye mafanikio yao. Ronaldo ana uwezo mkubwa na tunakubali swala lake la kutupia nyavuni lakini kwa Messi anatupa burudani na nyavu anacheza nazo. Pia mshkaji wangu Ronaldo, magoli mengi anayofunga hayajasaidia sana club yake, amefunga mengi lakini club haijapata makombe muhimi. So, hakuna umuhimu wa kufunga sana kama kombe hamchukui. Mshindi wangu ni Messi. Messi mnyama lakini mimi ni shabiki wa Ronaldo forever”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>