Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

LEO NI BIRTHDAY YA SIMON MSUVA, KUNA KITU KIZURI AMEKIANDAA KWA AJILI YA MASHABIKI WAKE

$
0
0

IMG-20151203-WA0000

Ikiwa leo ni December 3, 2015 star wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva anaadhimisha siku yake ya kuzaziwa (birthday), hii ni siku muhimu sana kwake kama ambavyo imekuwa muhimu kwa watu wengine ikiwemo hata wewe msomaji wangu.

Katika kusherekea birthday yake, Msuva amepost ujumbe kwenye moja ya account zake za social media akiwalika ndugu, jamaa na marafiki kujumuika pamoja kwenye tafrija itakayofanyika kwenye ukumbi wa Kez Club maeneo ya Kimara-Kona kuanzia mida ya saa 3:00 usiku.

Msuva

Ujumbe huo unasomeka hivi: “Mimi Simon Msuva napenda kukukaribisha kwenye party yangu ya kuzaliwa kwangu siku ya leo ndani ya Kez Club Kimara-Kona lengo la kukukaribisha ni uwepo wako wa karibu kwangu hivyo karibu tufurahi pamoja na kubadilishana mawazo, kukutana na watu tofauti. Muda ni saa 3 usiku, asante”.

Huyu jamaa ni mchezaji bora na mfungaji bora wa msimu uliopita, mbali kipaji cha kucheza mpira, Msuva pia ni dancer wa music na alishawahi kuwa chini ya Tanzania House of Talents (THT) pia akifanya kazi pamoja na kundi la muziki la Makomando.

Mtandao huu unaungana na ndugu, jamaa na marafiki wa Simon Msuva kumtakia kila la heri katika siku ya leo anapokumbuka siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha mema na afya njema kila siku.

HAPPYBITHDAY #27SIMON MSUVA


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>