Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MASTAA WAPAMBA BIRTHDAY PARTY YA SIMON MSUVA

$
0
0
Msuva akiwa na washkaji zake wa karibu kutoka kundi la Makomando, Muki (katikati) pamoja na Fred
Msuva akiwa na washkaji zake wa karibu kutoka kundi la Makomando, Muki (katikati) pamoja na Fred

Siku ya December 3 kila mwaka ni siku muhimu sana kwa star wa soka la Bongo anayecheza kwenye klabu ya Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, huyu si mwingine bali ni kijana Simon Happygod Msuva.

Kila ifikapo December 3 ya kila mwaka, Msuva huadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) kama alivyofanya mwaka huu.

Ukitoa kucheza katika kikosi kimoja hawa jamaa ni washkaji sana Simon Msuva na Juma Abdul
Ukitoa kucheza katika kikosi kimoja hawa jamaa ni washkaji sana Simon Msuva na Juma Abdul

Baada ya pilika na mishemishe zote za siku ya Alhamisi, Msuva alikutana na ndugu, jamaa na marafiki katika tafrija fupi ya kusherekea siku hiyo ambayo ni ya kukumbukwa kwake. Party ya kufurahia kutimiza miaka kadhaa ilinogeshwa na mastaa wa soka la bongo pamoja na wasanii mbalimbali lakini mashabiki wa mchezaji huyo bora na mfungaji bora wa msimu uliopita pia walikuwepo.

Katika party hiyo ambayo ilifanyika maeneo ya Kimara-Kona, Dar es Salaam, Msuva aliwashukuru wote wanaomsapoti kwa namna moja au nyingine hadi kufikia alipo sasa lakini aliwashuku pia masahabiki na wote waliomtumia salamu za kum-wish happy birthday.

Msuva pamoja na Dummy Utamu wakiwa wameketi pamoja wakati party ikiendelea
Msuva pamoja na Dummy Utamu wakiwa wameketi pamoja wakati party ikiendelea

Msuva ana-share birthday yake na star mwingine wa ambaye ni dancer wa msanii Diamond Platnums kutoka kundi la Wasafi Classic anaye kwenda kwa jina la Dummy Utamu ambaye pia alijumuika na Msuva kwenye party ya kusherekea siku yao ya kuzaliwa.

Wakati wa Mose Iyobo kulishwa keki na Msuva ukafika
Wakati wa Mose Iyobo kulishwa keki na Msuva ukafika

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>