Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

WESLEY MATHEWS AFANYA ANAYOYAFANYA VYEMA, AIONGOZA DALLAS KUANGUSHA WACHAWI WA WASHINGTON.

$
0
0

dallas

Wesley Mathews hakuwa na maisha mazuri mwanzo wa msimu huu, mpaka akajichukia mwenyewe. Akarejea kauli za Kobe Bryant kuwa nachukia nachokifanya mwenyewe kwa sababu sio ninachofanya katika uhalisia wangu. Tofauti yao ni kuwa Wesley ni mdogo kwa miaka 8 zaidi.

Katika kipindi chote hiki, Wesley Mathews hakuwa yule aliyewafanya Dallas wamsajili kutoka katika timu ya Portland Trail Blazers. Pointi tatu zake zilizozoeleka hazikuonekana kwa wingi wake. Na hata lugha ya mwili wake ilionekana kutokushabiana na ile ya Portlan. Walikuwa watu wawili tofauti.

Lakini siku zote kisu hakigeuki fimbo. Makali yake yamerejea katika mchezo wa alfajiri ya leo dhidi ya Washington Wizards. Alipata mitupo 10 ya pointi tatu, huku akimaliza na pointi 38 katika ushindi wa Dallas wa 116-104. Pointi 28 alizifunga katika nusu ya pili ya mchezo huo.

Baada ya kukutana na kukoselewa kwingi juu ya namna anavyocheza kwa siku za karibuni, John Wall amejibu mapigo. Akitoka kufunga zaidi ya pointi 30 katika michezo iliyopita, alifunga pointi 28 katika mchezo huu lakini ilimlazimu kutoka zikiwa zimesalia dakika 1:14 baada ya kukwaana na Jeremy Evans.

Wall amefanyiwa vipimo lakini bado hajapata majibu sawia ya nini kinaendelea. Wall alisema “kama ikitoka taarifa kuwa sipo fiti basi sitocheza, na ikitoka kuwa tatizo ni dogo tu nitarejea uwajani”.

Dirk Nowtzki alifunga pointi 19, Raymond Felton alifunga pointi 11 na rebound 10. Deron Williams alifunga pointi 11, pasi 9 na rebound 7.

HIGHLIGHTS

 

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>