Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Malmo vs Real Madrid: Cristiano Ronaldo vs Golikipa Aliyempa Historia ya Ufungaji Bora

$
0
0

Usiku wa leo Cristiano Ronaldo atakutana na wapinzani ambao wamempa kumbukumbu nzuri sana katika maisha yake ya soka kama mchezaji wa Real Madrid.

<> on September 15, 2015 in Madrid, Spain.
.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Malmo, mreno huyo alifanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid. Lilikuwa goli lake la 324 katika mechi ya 308 na Madrid, goli moja zaidi ya Raúl, ambaye alihitaji mechi 741ili kufikisha mechi 323.

2090992Hiyo ilikuwa tarehe 30th September 2015, tarehe ambayo iliingia kwenye historia kwa kila shabiki wa klabu na Ronaldo mwenyewe ambaye michuano hii imekuwa uwanja wake mzuri wa kuongeza idadi ya magoli hasa msimu huu. Kitu cha kushangaza Nahodha huyu wa Ureno, sio miongoni mwa wafungaji bora watatu wa La Liga – yupo nafasi ya nne, magoli manne nyuma ya Neymar, lakini hata hivyo Ronaldo anafanya vyema ulaya, mpaka ameshafunika Lewandowski na Müller (Bayern), Dyzuba (Zenit) pamoja na Luis Suárez (Barcelona).

Leo usiku Cristiano Ronaldo pia atakutana na sura anazozifahamu – golikipa wa Malmo Johan Wiland ameshakuwa mhanga wa kasi ya ufungaji wa Ronaldo, na sio tu kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Swedbank Stadion. Katika msimu wa 2013/14, mreno huyo na golikipa wa kiswedish walikutana wakati Real Madrid walipocheza na timu ya FC Copenhagen katika hatua ya makundi.

17245364Cristiano alifunga mara mbili katika mechi ya kwanza ndani ya s Bernabéu na akafunga goli lingine katika mchezo wa marejeano uliofanyika Copenhagen’s Parken Stadion. Magoli hayo matatu na mawili aliyofunga dhidi ya Malmo, yanafanya rekodi yake dhidi ya golikipa huyo wa kiswedeni kuwa magoli matano.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>