Mtangazaji maarufu nchini wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM na shabiki wa kutupwa wa Chelsea Bw. Gerald Hando ametoa ya moyoni baada ya kocha wa Chelsea Jose Miurinho kutimuliwa kwenye klabu hiyo kutokana na timu kufanya vibaya kwenye mechi za ligi kuu ya England msimu huu.
Hando alihojiwa kwenye kipindi cha michezo cha Sports Extra cha kituo hichohicho cha radio na kusema bado anaimani na Mourinho kama kocha bora duniani lakini anaunga mkono hatua ya klabu yake kumtimua kocha huyo ili kuinusuru klabu ambayo kwa sasa haifanyi vizuri kwenye mechi zake za ligi.
Amesema kuwa anadhani mambo yalikuwa hayaendi sawa kati ya Mourinho na baadhi ya wachezaji na ndiyo sababu kubwa ya The Blues kushindwa kufanya vizuri msimu huu lakini akasisitiza kuwa hana shaka na uwezo wa kocha huyo raia wa Ureno.
“Mimi nakubaliana na uamuzi wa klabu yangu kwasababu ameshindwa ku-manage timu akiwa kama manager na kushindwa kupata matokeo na kufika hapa tulipofikia, lakini mimi ninaimani na Mopurinho lakini pia nianaimani na klabu yangu kwa uamuzi waliokubaliana wa Mourinho kuondoka”, amsema Hando.
“Nachofahamu mimi kunakuwa na makubaliano ya kimsingi mutual understanding kwahiyo hii inaonesha kwamba kuna makubalioano kabla ya uamuzi huo kufikiwa”.
“Lakini nataka kufahakwamba nini kimetokea na nini hasa sababu ya msingi kwasababu wote tunajua Mourinho ni top couch wala sio siri. Katika makocha watano bora duniani Mourinho yupo, lazima kutakuwa na jambo, wafatiliaji na wachambuzi wa soka wanajua hii siyo hali ya kawaida lazima kuna kitu ndani ya wachezaji kilichopelekea Mourinho aondoke”.
“Kwa maoni yangu mimi napendekeza mtu kama Guardiola ndiye anafaa kuichukua Chelsea, sioni mwalimu kama Ancelotti wala Grant kuwa makocha bora ndani ya Chelsea”.
Mourinho ameiacha Chelsea ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa EPL pointi moja mbele ya timu ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka daraja lakini ikiwa ponti 20 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester City.