Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

VIONGOZI SIMBA/YANGA MSIWAFANYE WAANDISHI KAMA KUKU WAPARUA CHINI

$
0
0

Simba vs Yanga 15

Na Hemed Kivuyo, Dar es Salaam

Waandishi wenzangu wa habari za Michezo nawapa Kongole popote mlipo kutokana na kazi zenu zakuwahabarisha wananchi hasa wapenda michezo.

Ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi yatu wanaokiuka maadili ya taaluma sijui nikwakukusudia ama la.

Taaluma ya Habari ina misingi yake kama zilivyo taaluma nyingine na kuongozwa na kanuni na maadili yake, moja kati ya misingi ya uandishi ni pale chanzo ‘source’ anapokataa kutajwa jina lake katika chombo cha habari basi lazima tamko lake liheshimiwe asitolewe.

Kadhalika ‘source’ anapoongea  ‘off record’ yaani akisema anaongea na wewe (mwandishi) nje ya taaluma yaani kirafiki tu na siyo mahojiano kwa ajili ya habari, basi lazima aheshimiwe. Ingawa sikuhizi kuna upotoshwaji na hata upotoshwaji wa misingi kila mtu akitafsiri anavyoona inafaa.

Wakati mwingine hata source anashiriki kumwezesha mwandishi kupotosha ama kutoa habari ambayo haijakamilika kwakuwa kuna baadhi ya watu hawataki kuthibitisha jambo fulani hata kama alipaswa kufanya hivyo ama kukanusha papo hapo.

Kuna mambo fulani hivi ambayo hufanywa na viongozi wa vilabu vya soka hasa Simba na Yanga ingawa wapo wengi, endapo kuna mchezo mkubwa uliyopo mbele yao, viongozi hao huonyesha ushirikiano mkubwa na vyombo vya habari ili mchezo wao utangazwe na kupata mashabiki wengi ambao wataingiza fedha nyingi katika vilabu vyao. Siyo mbaya kwakuwa ndiyokazi lakini…………..

Kama vilabu hivyo havina mchezo wanaodhani utawaingizia vipato siku chache zijazo, hawatoi ushirikiano kwa waandishi wa habari na kama wakitoa basi nikwa baadhi ya waandishi wenye ‘nasaba’ nao. Huu ni urasimu wa habari ambao ni hatari sana.

Hivi Karibuni timu moja ilifanya biashara ya kununua mchezaji, habari hiyo haikukamilika kutokana na klabu uiliyomuuza kukiri lakini iliyomnunua haikutoa neno.

Msemaji wa klabu hiyo ambaye ‘ulimi ni wembe wake’ hakupatikana kukiri ama kukanusha hilo, alipopigiwa simu akasema hawezi kuongea chochote anafanya kazi nyingine.

Alishindwa kukiri ama kukanusha hata kusema si kweli ama kweli aligoma. Lakini kazi yake ni usemaji.

Hayo ni majibu ambayo hapaswi kumpa hata mkewe sembuse mwandishi ambaye yeye humtumia ili kuingiza fedha klabu yake.

Panapotokea suala la kujibu ndani ya klabu msemaji hapatikani kujibu na hata akipatikana hataki kutoa maelezo yeyote, lakini akiona kuna mchezo unawakabili siku chache zijazo ambayo wataingiza mashabiki wengi huanza ‘kimbelembele’ cha kijinga

Atawaita waandishi na kucheka nao ‘jino la pembe’ na kujigamba hata kama timu yake anajua ni ya ‘hovyo’ ili mashabiki waingie wengi. Baada ya hapo simu hatapokea na ofisini kwake hatokuwepo na ukimbahatisha anakutolea ukali.

Yupo msemaji mmoja ambaye mara kadhaa amekuwa akifuatwa mpaka nyumbani na baadhi ya waandishi wa habari. Waandishi hufanya hivyo baada ya msemaji huyo kutaka afuatwe kuzungumzia jambo fulani. Hana ofisi huyu? Tena klabu kubwa kama hiyo?  Huu siyo utaratibu muafaka unaoendana na ukubwa na klabu hiyo.

Kuna msemaji mmoja aliwahi kuwaambia waandishi wa habari ni watu wanaoingiza ulimi katika pua zao.

Haya ni matusi yakiungwana ambayo hayakupaswa kutolewa na msemaji wa klabu kama hivyo.

Kuna mambo matatu ama mawili hapo,kama msemaji huyo hakufunzwa na wazazi wake basi alikiuka mafunzo ya wazazi wake ama waalimu wake na sasa anaongozwa na fikra zake zilizoelemewa na ‘umbilikimo’ wa kupitiliza.

Kama sivyo basi kichwa chake kitakuwa kama cha ‘kondoo’. Kondoo anaweza kuibuka usiku wa manane na kuanza kupiga banda kwa kichwa chake, hajakusewa kitu chochote, ni wadudu wake tu wamepanda kichwani. Kuwa na maafisa habari wenye vichwa kama ‘kondoo’ haisadifu hata kidogo.

Inawezekana msemaji mkuu wa klabu ni Mwenyekiti  (Rais) kama sivyo anafuatia Katibu Mkuu, na kisha Msemaji wa Klabu, lakini taarifa za klabu zinatoka zikiwa ‘potofu’ kwa kuwa tu wasemaji wa vilabu wameacha  kazi waliyoomba na sasa wamegeukia kuwa ‘wana propaganda’ wa vilabu vyao vijiweni na siyo rasmi kwa waandishi wa habari.

Msemaji anakuwa na waandishi wawili au mmoja ambaye humpa taarifa za ndani ya klabu kabla ya mkutano na waandishi wa habari ambao huwapa taarifa hizo ambazo anapotoa rasmi siyo taarifa mpya tena.

Hivi wasemaji wengine wamepewa kazi hiyo kwakukirimiwa ama kuna ‘wajomba zao’ vilabuni!!!

Ukiona klabu inakanusha habari mara kwa mara ujue msemaji wa Klabu kazi imemshinda na amebaki kukanusha tu habari ambazo zinaandikwa bila yeye kutoka na alificha habari hiyo kwasababu za kipuuzi tu.

Kuna katibu wa klabu moja ukimkuta ofisini kwake anakwmabia yupo bize, hata kama kuna jambo analotakiwa kulizungumiza atakwambia yupo bize. Hivi ubize si ni moja ya kuzungumzia klabu?

Kwanini mnaonyesha ushirikiano kwa waandishi wa habari pale mnapokuwa na shida zenu tu? Huu ni upuuzi ambao unalazimisha waandishi wa habari kukaa kama kamati na kuazimia kususia habari zenu za maandilizi ya mchezo mtakaocheza keshokutwa ama kesho ili muingize mapato.

Mnawaza kujaza matumbo yenu na siyo kuonyesha ushirikiano kwa waandishi ambao hufikisha taarifa hizo kwa wanachama na mashabiki wenu.

0655 250157…………….0752 250157


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>