Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

YANGA ITAWEZA KUTETEA UBINGWA?

$
0
0

YANGA BINGWA

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam  

Ligi kuu Tanzania bara inataraji kuanza Jumamosi hii kwa timu 14 kushuka katika viwanja saba tofauti. Ndanda FC ya Mtwara itakuwa nyumbani  Nangw’anda Sijaona Stadium kuikabili JKT Mgambo ya Tanga,  Stand United itakuwa Kambarage Stadium kuwakaribisha mabingwa mara mbili wa kihistoria Mtibwa Sugar, Toto Africans ya Manza itakuwa nyumbani uwanja wa CCM Kirumba kucheza na Mwadui FC (timu zote zimepanda daraja msimu huu).

Mechi nyingine zitakuwa Majimaji FC ya Songea, Ruvuma itacheza na  JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa Majimaji, Songea,  African Sport ya Tanga itaikaribisha Simba SC ya Dar es Salaam na mechi ya mwisho siku ya ufunguzi  ni ile itakayowakutanisha Azam FC na Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi. Gemu Moja itachezwa siku ya Jumapili kati ya mabingwa watetezi Yanga SC na Coastal Union ya Tanga mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Taifa.

Tangu msimu wa 200/10 hakuna timu iliyoweza kushinda ubingwa wa Bara mara mbili mfululizo. Timu ya mwiso kutwaa taji hili ‘back to back’ ni Yanga ambayo ilifanya hivyo katika misimu ya 2007/08 na 2008/09 ilipokuwa chini ya mwalimu Mserbia, Dusan Kondic.  

Ikiwa imewasaini wachezaji wapya kama raia wa Zimbabwe, mshambulizi, Donald Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko, mlinzi wa kati raia wa Togo, ambao wataungana na nyota wengine wa kigeni kama Mbrazil, Andry Coutinho, Wanyarwanda, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima na mshambulizi Mrundi Amis Tambwe.  

Yanga pia imewasaini wachezaji kadhaa ‘wazawa’ kama mshambulizi aliyewasumbua sana msimu uliopita, Malimi Busungu, kiungo kinda Geofrey Mwashuiya, mlinzi wa pembeni, Hajji Mwinyi,  Deus Kaseke inaweza kutetea ubingwa wake kama tu kikosi kitaendelea kuwa na ‘umoja na mshikamano’ kama jinsi ilivyo sasa.  

Wana kikosi bora, wachezaji kama Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub (nahodha), Kelvin Yondan, Salum Telela, Said Juma ‘ Makapu’, Saimon Msuva (mfungaji bora wa msimu uliopita) walifanya vizuri sana na licha ya kuondoka kwa wakali kama Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga, Hussein Javu, Danny Mrwanda, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, Nizar Khalfan, Kpah Sherman kikosi cha Hans Van der Pluijm kinaweza kushinda tena ubingwa kwa kuwa kimekuwa na nidhamu ya hali ya juu katika miaka ya karibuni na kila mchezaji yuko tayari kimwili na kiakili.

Wataanzia nyumbani katika gemu tatu mfululizo, huku gemu ya nne pia wakicheza uwanja wa Taifa dhidi ya mahasimu wao Simba SC. Watakuwa na faida ila si rahisi kuifunga tena Coastal Union goli 8-0, wala Prisons hawatakubali tena kufungwa 5, na wasitarajie kupata mbereko ya Fred Minziro katika gemu ya tatu watakapoivaa JKT Ruvu. Je, Yanga wanaweza kutetea taji lao? Si rahisi ila wana historia ya kufanya hivyo.

0714 08 43 08


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>