Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MCHEZAJI MWENYE MKONO MMOJA AFUNGA KIKAPU CHAKE CHA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA VYUO YA MPIRA WA KIKAPU MAREKANI…

$
0
0

Zach

Mungu ndiye mwamuzi ya yote, Mungu ndiye mpangaji na yeye ndiye mpaji. Kijana anayesoma katika chuo cha Florida Zach Hodskins lazima anauishi usemi huu. Ni kijana aliyezaliwa na tatizo la kuwa na mkono mmoja ulio kamili huku wa pili ukikosa kipande cha chini.

Lakini hilo halikuwahi kumtatiza katika kufanya mambo yake mwenyewe. Maishani amekuwa anapigana kuwaonyesha walemavu kuwa wakiamua wanaweza kufanya mambo ambayo hata watu wenye ukamilifu wa viungo wanafanya.

Amekuwa akifanya shughuli mbalimbali kama kuwasaidia watu wasio na mikono yote kama yeye namna ya kufunga kamba za viatu bila shida. Hii imekuwa ni moja ya programu zake ambazo amekuwa akizifanya kwa njia ya mtandao yaani youtube.

zachhh

Ni kama ambavyo amekuwa mstari wa mbele kushiriki mchezo anaoupenda wa mpira wa kikapu. Tofauti na walemavu wengine ambao hushiriki michezo inayowahusisha walemavu wenzao, huyu yupo katika timu ya chuo.

Alisajiliwa na kocha Billy Donovan katika timu hiyo ya chuo cha Florida. Donovan kwa sasa ni kocha wa timu ya Oklahoma City Thunder. Zach Hodskins ana urefu wa futi 6.4 na moja ya vitu anavyowashangaza wezie ni namna ambavyo amekuwa akiweza kudunk katika mazoezi.

Huu ni msimu au mwaka wake wa pili katika timu hiyo maarufu kama Florida Gators ambapo msimu uliopita hakuwahi kupata mtupo wowote aliojaribu kati ya miwili yote.

hod

Mwaka huu alipata nafasi japo kwa uchache, ijapokuwa nako alikosa mitatu ya mwanzo mpaka alfajiri ya leo alipopata kikapu chake cha kwanza ambacho kila mmoja aliinuka ktini. Alifunga kwa staili ya kumzunguka mtu (spin move layup) na kumwacha aliyekuwa anamkaba asijue la kufanya.

Uwanja mzima uliripuka kwa shangwe, watangazaji walimwaga sifa wanazoweza kutoa, na mwisho wachezaji wenzie walirukaruka kwa furaha kubwa. Hata yeye alishindwa kujizuia na kuruka kwa furaha. Alipata na nafasi ya kurusha mtupo huru kutokana na faulo aliyochezewa wakati anajaribu kufunga lakini alikosa.

Mchezo huo ulimalizika kwa Florida Gators kuibuka na ushindi wa pointi 89-65 dhidi ya Jacksonville.

TIZAMA HAPA KIKAPU CHAKE CHA KWANZA CHA CHUO.

Lakini maisha yake yalianzia High School ambako alipata umaarufu wa kuwa moja ya guards wazuri. Alikuwa na wastani wa pointi 11 kwa mchezo katika mwaka mmoja, na wastani wa pointi 6 na pasi 2.3 kwa mchezo katika msimu mwingine.

Hii iliwafanya Chuo cha Florida kuamua kumpa nafasi ya kujiunga nao, na kusomeshwa pale. Alikuwa akisoma katika shule ya Milton High School.

SWALI: ATAWEZA KUINGIA AMA KUPATA NAFASI YA KUCHEZA NBA SIKU MOJA?

zachh

MTIZAME UBORA WAKE AKIWA HIGH SCHOOL


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>