Mke wa mshambuliaji mpya wa Yanga Paul Nonga ‘amejifungua’ mtoto tarehe 26 December 2015 ambayo ilikuwa ni siku ya Boxing Day, lakini mrembo huyo anayekwenda kwa jina la Jacky Paul Nonga ametupia picha kwenye account yake ya instagram zikimuonesha enzi hizo wakati akiwa mjamzito.
Moja ya picha hizo ni ile anayoonekana akiwa kwenye gari akiwa na uja uzito ambapo ameandika maneno yananayosomeka: “Kitu cha miezi 8 hapo bado nadunda tu…I love you my Paul Junior”.
Wakati mwandani huyo wa Nonga akisherekea kupata mtoto sambamba na sherehe za mwaka mwaka mpya, mumewake (Paul Nonga) yupo visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi Cup ambayo inatarajiwawa kutimua vumbi kuanzia January 3, 2015 (kesho, Jumapili).
Achana na hilo la Nonga kujaaliwa kuwa baba, mwandani wake pia amefichua siri nyingine pia ambayo inawezekana hauijui. Paul Nonga huvalia jezi yenye namba 26 mgongoni lakini kitu kizuri ni pale mtoto wao alipozaliwa tarehe 26 December, 2015 tarehe ambayo ni sawa na namba ya jezi ambayo huvaliwa na baba yake.
Mke wa Nonga amepost picha nyingine akiwa na mumewake na kuandika: “Baba yake anavaa jezi namba 26 na amezaliwa tarehe 26. 12. 2015. Thanx God kwa kunipa Paul Nonga Junior”.
Nonga amejiunga na Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi December 2015 akitokea klabu ya Mwadui FC ya mjini Shinyanga.