Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Millenium Stadium kufunikwa wakati wa pambano la fainali ya UEFA

$
0
0

Uwanja wa Millenium Stadium umekuwa gumzo sana siku za usoni kwani uwanja huo ndio uwanja ambao mtanange mkubwa fainali ya UEFA kati ya Juventus na Real Madrid.

Millenium Stadium ambao siku hizi unaitwa Principality Stadium kutokana na sababu za masuala ya wadhamini, una uwezo wa kuingiza mashabiki 74,500.

Uwanja huu ulianza kujengwa mwaka 1997 na ni uwanja wa nyumbani wa timu ya rugby ya Wales, na ilipofika mwaka 1999 uwanja huu ulikamilika na mchezo wake wa kwanza kuchezwa ulikuwa ni kati ya Wales na South Africa.

Uwanja wa Millenium Stadium sio mgeni sana katika masuala ya soka kwani wakati flani uwanja wa Wembley ulipokuwa ukifanyiwa matemgenezo, Millenium Stadium ulitumika kuchezea fainali za FA.

Miezi mitatu kabla ya fainali hii ya champions league tayari hotel za mji wa Cardiff ambako ndipo uwanja huu zilipo zilishajaa na watu walishaweka vyumba kwa ajili ya mchezo huu.

Real Madrid sio wageni katika mji huu wa Cardiff kwani mwaka 2014 walishawahi kucheza fainali ya super cup katika mji wa Cardiff na kubeba kombe hilo wakiifunga Sevilla ya nchini Hispania kwa mabao ya Cristiano Ronaldo.

Kutokana na tishio la ugaidi linaloendelea kuitesa dunia,wasimamizi wa Millenium Stadium wameoma ni vyema uwanja huo ukachezwa huku paa lake likiwa limefungwa.

Hii inatokana na mbinu mpya ambayo magaidi wamekuwa wakitumia kulipua sehemu zenye msongamano wa watu kwa kutumia ndege zilikazo bila rubani.

Kwa video na kuona jinsi Millenium Stadium unavyojifunga unaweza kuingia katika YOU TUBE na kusbscribe channel.yetu ya Dauda Tv na kuangalia page yetu ya Instagram.

 


Huwezi amini Wenger anataka kutoa £100m kumnunua mchezaji huyu.

$
0
0

Arsene Wenger haondoki Arsenal na bado atakaa katika klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi na hii inamaanisha atakaa katika klabu ya Arsenal hadi mwishoni mwa mwaka 2019.

Wenger amekuwa akinyooshewa vidole kutokana na aina ya wachezaji anaowasajili kuonekana kama sio aina ya wachezaji ambao wanaweza kupigania ubingwa.

Wenger tofauti na Jose Mourinho au Pep Gurdiola ambao hutumia pesa nyingi sana kutafuta wachezaji ambao wanawataka na wachezaji wakubwa.

Arsene Wenger anaaminj zaidi katika vijana na hata wachezaji anaopendelea kusajili ni vijana ambao hata bei yao sokoni huwa sio kubwa tofauti na wachezaji wakubwa.

Aina ya usajili ya Wenger imekuwa ikiisaidia Arsenal katika upande wa kifedha kwani babu huyo amekuwa mchumi lakini inawaumiza sana uwanjani haswa linapokuja suala la kushindana na vilabu vikubwa.

Lakini Wenger amechoka kwani habari zinadai Wenger anajiandaa kutuma ofa ya kiasi cha £100m kwa Monaco ili kumsajili Mfaransa Kylian Mbappe.

Ni wazi na ni rahisi kwa Wenger kuuziwa Mbappe kutokana na kwamba Mbappe ni Mfaransa na wachezaji wengi wa taifa hilo wamekuwa wepesi kujiunga na Arsene Wenger.

Bado usajili unaendelea labda tusubiri tuone Mfaransa huyo atafanya nini katika kipindi hiki cha usajili ukizingatia kwamba anatoka kupata presha kubwa kutokana na matokeo aliyoyapata msimu uliopita.

 

Hatumwi mtoto dukani leo Juventus vs Real Madrid.

$
0
0

Ni siku iliyosubiriwa karibia na kila mpenzi wa soka duniani, siku ya kuamua kama Real Madrid watatetea kombe la Champions League au Juventus wataondoka nalo.

Massimiliano Allegri ameshatoa onyo kwa wapinzani wao na kuwaambia wazi kwamba leo haitakuwa rahisi kwani Juventus hawatakuwa na mchezo hata kidogo.

“Tutaingia kupambana, kwa mwaka mzima tulijipanga kuhusu hili na tunajua haitakuwa rahisi kucheza dhidi ya timu ambayo ni bingwa mtetezi”

“Makombe yote na ushindinwote tuliopata msimu huu vinatujenga zaidi kwenda kukabiliana na Real Madrid hii leo, ni mechi tunayopaswa kujiamini ili kuchukua kombe hili” alisema Alllegri.

Aliongeza kuwa “mwaka 2015 tuliongia kwenye fainali lakini nadhani hatukuwa imara sana na wala hatukujiamini lakini safari hii ni tofauti na hakika sisi ni bora”

Wakati Allegri akiongea hayo, kocha ambaye anapewa nafasi kuwa kocha wa kwanza kutetea kombe hilo Zinedine Zidane naye alikuwa na yake kuelekea mchezo huu wa leo.

“Msimu huu tumefanya kazi kubwa sana na kishinda kombe la La Liga na kufika katika fainali hii lakini kubwa sana kwetu ni kwa jinsi gani tumejiandaa kucheza katika fainali hii”

“Binafsi nimeshapoteza mechi nyingi na najua kama ilivyo kwa Juventus mmoja wetu anaweza kupoteza, cha muhimu ni kujitahidi kucheza mchezo wetu wa kila siku”

“Tunaweza kupewa nafasi katika mchezo huu lakini hii ni fainali na wote tuna nafasi ninkama tuko 50 50 lakini nategemea mchezo wa wazi kwa pande zote” alisema Zidane.

Vikosi vinaweza kuwa hivi Juventus, Buffon,Barzagli,Chiellini,Bonucci,Sandro,Khedira,Pjanic,Alves,Dyabala,Mandzukic,Higuain na Real Madrid wanaweza kupanga hivi Navas,Carvajal,Ramos,Varane,Marcelo,Modric,Casemiro,Kroos,Isco,Benzema,Ronaldo.

 

Dondoo za Shaffih Dauda kuelekea fainali ya UEFA Champions League 2016/17

$
0
0

Dunia itasimama kwa muda ili kushuhudia fainali ya aina yake ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid vs Juventus usiku wa leo Juni 3, 2017 kwenye mji wa Cardiff.

Shaffih Dauda ametoa uchambuzi wake kuelekea mchezo huo ambao utafatiliwa na mamilioni ya wapenda soka Duniani kote.

Huu ni uchambuzi wake binafsi na maoni yake kuelekea mchezo huo haimaanishi kila kitu kitakuwa kama anavyoamini yeye ila pia inaweza ikatokea kama anavyotarajia.

Juventus ndio timu pekee iliyoruhusu mabao chache kwenye michuano ya Champions League, imefungwa mabao matatu tu katika mechi 12 walizocheza hadi sasa.

Walifanilkiwa kuizuia Barcelona isifunge goli hata moja katika dakika 180 (mechi mbili) nyumbani na ugenini katika hatua ya robo fainali. Hiki ni kitu kizuri kwao na utaona ni jinsi gani walivyo na safu bora ya ulinzi wakiongozwa na golikipa wao mkongwe Gigi Buffon pale langoni, Bonucci, Barzagli na Chiellini wanatengeneza ukuta mgumu kupitika.

Real Madrid wameshafunga magoli 32 hadi sasa kwenye mechi zao za Champions League msimu huu, wakati Juventus wao wamefunga magoli 21 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 12.

Christiano Ronaldo kwa misimu sita mfululizo, anafunga mabao 10 na zaidi kwa hiyo amekuwa mfungaji mahiri katika michuano hii. Ronaldo amekuwa akimuonea Gianluigi ‘Gigi’ Buffon mara zote ambazo wawili hao wamekutana, Ronaldo ameweza kumfunga.

Katika fainali 5 zilizopita za UEFA Champions League ambazo Real Madrid walifanikiwa kucheza, wameshinda fainali tano, mara ya mwisho Real Madrid kupoteza mchezo wa fainali ya mabingwa wa Ulaya ilikuwa ni mwaka 1981 walikalishwa na Liverpool.

Fainali walizoshinda Madrid ni pamoja na 1998 walishinda dhidi ya Juventus, 2000 wakaifunga Valencia, 2002 wakaichukua kwa kuifunga Liverkusen, 2014 wakaifunga Atletico Madrid na kuchukua kombe na 2016 wakalitwaa tena.

Wakati Madrid wakishinda fainali 5 zilizopta ambazo walifanikiwa kucheza, kwa upande wa Juve kwao mambo ni tofauti kabisa. Wapeigwa katika fainali 4 zilizopita ambazo wamefanikiwa kufika hivi karibuni.

Fainali ya 1997 Juve walichezea kichapo kwa Dortmund, 1998 wakakaa kwa Real Madrid, 2003 wakapigwa tena na AC Milan, 2015 wakapoteza kwa Barcelona.

Fainali ni fainali na rekodi zipo ili kuleta msisimko, lakini nikiwaangalia Juve kwa jinsi walivyojengeka kwenye nafasi ya ulinzi kweli wapo vizuri lakini inategemea wanacheza na nani.

Real Madrid wana options nyingi, Gareth Bale asipokuwa sawa anaweza akacheza Isco na timu ikacheza kulingana na uwepo wa Isco na usione pengo la Bale.anaweza asicheze Benzema akacheza Morata, Danilo na Carvajal pia unaweza usione tofauti.

Juve wao wanajivunia kuwa na kuwa na kikosi cha kwanza bora, mechi yao ya fainali dhidi ya Real Madrid sitoshangaa kumuona Juan Cuadrado akianza ili kumnyima nafasi Marcelo ya kupanda juu kushambulia. Juve wakiwachezesha Dani Alves na Cuadrado katika upande wa kulia wanakuwa na nguvu sana na upande huo ndio Madrid wana nguvu kwa sababu ya Marcelo na Ronaldo.

Video: Uchambuzi wa Coutinho kuelekea fainali Juventus vs Real Madrid

$
0
0

Fainali ya UEFA Champions League ndio story kubwa siku ya leo (Juni 3, 2017) katika kila pembe ya dunia ambapo Juventus watakuwa vitani kupambana kutaka kutwaa ndoo hiyo ambayo itawafanya waweke rekodi ya kutwaa vikombe vikubwa vitatu (treble) ndani ya msimu mmoja na kuungana na vilabu vingine kama Manchester United, Barcelona, Inter Milan, Ajax na vingine vingi ambavyo vimewahi kufanya hivyo.

Wakati Juve wakipambana kuhakikisha wanatwaa ndoo ya UEFA na kutengeneza rekodi yao, Madrid pia watakuwa wanajaribu kutengeneza rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutetea kombe hilo tangu lilipoanza kuitwa UEFA Champions League.

Kbabla ya kupigwa kwa mchezo huo kumekuwa na wachambuzi mbalimbali ambao wakielezea namna mechi itakavyokuwa, ufundi, mbinu na mambo mrengine ambayo unaweza kushuhudia kwenye fainali hiyo.

Nicasius Coutinho ameelezea kwa kifupi mambo mengi ambayo anatarajia kuyaona katika usikun wa fainali hii, angalia video hapa chini kujua nini alichokisema.

NI REAL MADRID TENA,UKUTA MGUMU WA JUVE WATEPETA.

$
0
0

Hakika mpira ni jambo la ajabu sana kwani usiku wa jana huwezi kuamini kwamba wale ndio Juventus ambao wamekuwa wakiaminika kuwa na ukuta mkali.

Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo na moja la Casemiro na lingine la Asensio yaliihakikishia dunia kwamba ukuta wa Juventus sio kitu kwa vijana wa Real Madrid almaarufu kama Los Blancos

Ilikuwa ni dakika ya 20 tu ambapo Cristiano Ronaldo alifungua ukurasa wa mabao kwa Real Madrid kwa kuiandikia bao la kwanza kabla ya Mandzukic kuisawazishia Juventus dakika ya 61.

Kipindi cha kwanza kiliisha huku Juventus na Real Madrid wakitoka uwanjani kwa sare ya bao moja kwa moja lakini kipindi cha pili Real Madrid waliingia na moto mpya.

Ilipofika dakika ya 61 Casemiro aliiandikia Real Madrid bao la pili lakini dakika chache baadae ilipofika dakika ya 64 Real Madrid waliandika bao la tatu kupitia kwa Cristiano Ronaldo.

Wakati watu wakiamini mpira huo ungeisha kwa mabao 3 kwa 1 alikuwa Marco Asensio dakika ya 89 alifunga bao la 4 na kuwaacha Juventus ambao walimaliza pungufu baada ya Cuardado kupewa kadi nyekundu wakibubujikwa na machozi.

Matokeo hayo yamemfanya Zinedine Zidane kuwa kocha wa kwanza kuchukua kombe la champions league mara mbili mfululizo katika historia ya UEFA.

Fainali ya Juventus na Real Madrid yaandika haya katika kitabu cha UEFA.

$
0
0

Hakuna kocha ambaye amewahi kulitetea kombe la Champions League toka ligi hiyo ianzishwe na kwa mara ya kwanza Zinedine Zidane anaingia katika vitabu vya UEFA kwa kuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo.

Real Madrid bao la la dakika ya 21 la Cristiano Ronaldo liiweka pia katika historia ya champions league kwani bao hilo limeifanya Madrid kuwa timu ya kwanza kufunga mabao 500 katika mashindano hayo.

Kabla ya mchezo huo kulikuwa hakuna mchezaji katika mashindano ya champions league ambaye aliwahi kufunga mabao katika fainali tatu tofauti lakini Mreno Cristiano Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Lakini pia mabao mawili ya Cristiano Ronaldo yamemfanya kufunga jumla ya mabao 600 toka aanze kucheza soka la kulipwa na mchezo wake wa jana ulikuwa mchezo wake wa 885.

Lakini mchezo huo ulimfanya beki wa kulia wa Juventus Dani Alves kufikisha jumla ya michezo 100 katika champioms league rekodi inayomfanya kuwa Mbrazil wa pili kufikisha idadi hiyo ya mechi baada ya Roberto Carlos.

Toka Ac Millan wachukue kombe la champions league mara mbili mfululizo mwaka 1989 na 1990 hakuna timu imewahi kufanya hivyo na sasa Real Madrid wamefanya kitu kama hicho

 

Ona makubwa ya Ronaldo toka July mwaka jana hadi usiku wa jana walipobeba UEFA.

$
0
0

Mwezi July mwaka jana safari hii bora ya Ronaldo ilianza ambapo alifanikiwa kubeba ubingwa wa mataifa ya Ulaya baada ya Ureno kuifunga Ufaransa katika fainali ya michuano hiyo.

Lakini ilipofika December mwaka jana Mreno huyo alifanya jambo kubwa tena katika soka lake baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa ballon d’or akimshinda mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi.

Kama hiyo haitoshi mwezi mmoja baadae yaani January mwaka huu Cristiano Ronaldo tena alibeba tuzo nyingine kubwa baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia tena na safari hii ikitolewa na FIFA.

Ilipofika April mwaka huu Ronaldo akaweka rekodi nyingine na safari hii akawa mchezaji wa kwanza kufunga jumla ya mabao 100 katika michuano ya Ulaya.

Ilipofika mwezi May mwaka huu Cristiano Ronaldo tena akaweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 400 na kuwa mfungaji bora wa klabu ya Real Madrid.

Usiku wa jana mabao yake mawili yaliifanya Real Madrid kuwa timu ya kwanza kufunga mabao zaidi ya 500 katika champions league na kufanikiwa kutetea kombe hilo.

 


Lebron James Katika Wakati Mgumu Wa Kujiuliza Dhidi Ya Durant Na Curry. Warriors Hawashikiki.

$
0
0

Fainali ya Cavaliers vs Warriors ilikuwa hivi tangu mwaka jana. Walianza 2-0 lakini kuna mambo mengi yamebadilika tangu msimu uliopita.Warriors wameshinda michezo 14 ya mtoano mfululizo mpaka sasa kwa msimu huu.

Kwenye nafasi aliyokuwepo Harrison Barnes ambaye alishindwa kabisa kuwa mchezoni na walau kuwa na point 15 kwa mchezo sasa yupo Durant anayemaliza na point 30. Kevin Durant ameendelea kuwa bora hasa ushindani wake na Lebron James na anaonekana kumzidi ujanja kwa sasa.

Wazungu wanasema Stephen Curry has got his Mojo Back now. Anacheza katika kiwango bora sana. Kuna sababu nyingi kwanini aliamua kutokutumia nguvu nyingi mwanzo wa msimu. .

Unapotaka kuishinda Warriors lazima uwe na kimo kwa sababu utawatesa eneo la Center. Tunasema perimeter shooting. Hii wanayo San Antonio Spurs pekee kwa sababu ya Aldridge, Pau Gasol na Kahwi Leonard. Warriors hawamwogopi Tristan Thompson na inabidi ajitokeze. .

Pamoja na Warriors kuwa timu ya kwanza Kwenye ushambuliaji, uwepo wa kocha Mike Brown akishirikiana na mtu asiyetajwa sana Ron Adams umewafanya kuwa timu ya pili kwa ubora Kwenye ulinzi kwenye ligi yote. Cavs inabidi wote wawe kwenye ubora huku Warriors wakicheza vibaya ili kuwaumiza.

Curry amejifunza kukaba. Unapoona anaweza kumaliza na walau Rebound 7 na Assist 7 kwenye Fainali hiyo ni improvement kubwa kwenye Fainali. Bahati Mbaya kipindi kama hiki last season Cavs walikuwa na Kyrie Irving, kawa wa baridi msimu huu.
Mwisho wa yote, Cavs hawatakiwi kupoteza mchezo wowote nyumbani msimu huu hasa kwa miwili ijayo. Warriors wanaonekana wanataka kisasi. Hii ndio sababu tajiri wa wa Warriors Joe Lacob alisema wazi mapema kuwa wanawahitaji zaidi Cavs msimu huu.

Katika mchezo wa alfajiri ya leo, Warriors wameshinda kwa pointi 132-113. Kevin Durant ameiongoza Warriors akiwa na pointi 33, akadaka rebounds 13, akatoa assists 6, akablock mipira mara 5 na kuiba mipira mara 3. Stephen Curry kaendelea kuwa bora kwenye fainali hizi baada ya kumaliza mchezo na pointi 32, assists 11 na rebounds 10 huku Klay akimaliza mchezo na pointi 22.

Kwa upande wa Cleveland Cavaliers, Lebron James ambaye amekiri wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kwa sababu Warriors wameshinda pamoja na wao kubadilika tofauti na mchezo wa kwanza, alimaliza mchezo na pointi 29, rebounds 11 na assists 14 huku Kevin Love akimaliza mchezo na pointi 27 na Kyrie Irving akimaliza mchezo na pointi 19.

Mchezo mwingine utakuwa siku ya alfajiri ya Alhamis ikiwa ni michezo miwili itakayochezwa Quickens Arena nyumbani kwa Cleveland Cavaliers.

HIGHLIGHTS

Karibu Kwenye Ulimwengu Mpya Wa Stephen Curry.

$
0
0

Inawezekana mchezaji Stephen Curry akawa ni mchezaji anayependwa zaidi kwa sasa kwnye NBA na anaendelea kujiongezea umaarufu kwa namna ambayo ameweza kubadili fikra za wengi na kufanya mapinduzi kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwa maana ya umuhimu wa matumizi ya pointi tatu.

Hajawahi kutokea shooter bora kumzidi kwenye NBA na historia yake. Ni huyu Curry ambaye anaongoza kwa kuuza jezi kwa miaka miwili mfululizo kwenye NBA akiwaacha wenzie mbali hata baada ya Kevin Durant kuongezeka kwenye kikosi cha Golden State Warriors.

Baada ya kuonekana kama hatoweza kufanikiwa kuishi vyema kwenye NBA kutokana na majeraha ya kila mara, NIKE waliamua kuachana nae na akachukuliwa na kampuni ambayo bado ilikuwa inakua ya Under Armour.

Image result for curry 2

Maisha yalibadilika kwa kasi sana kwani tangu msimu wa 2014-2015 alikuwa hashikiki kwenye mauzo ya viatu vyake na 2015-2016 akawa mchezaji aliyeuza zaidi akiwazidi Kyrie Irving, Durant na Kobe kwa pamoja. Hii ilikuwa ni katika matoleo ya Curry 1 mpaka Curry 2.

Wabunifu wa viatu kwa Under Armour ni kama walijisahau kwani toleo la Curry 3 lilikuwa bovu na likaonekana kutokukubalika kwa wapenzi wengi wa mchezo wa mpira wa kikapu ikizingatiwa viatu vingi vya Curry ni shingo ndefu, huku wavaaji wengi wakipendelea shingo fupi. Kwenye mauzo ya maduka ya vifaa vya michezo vilikuwa haviuziki kiasi cha Under Armour kuamua kushusha bei maradufu.

Image result for curry 4

Katika kuona hali si shwari Curry hajaamua kuumaliza msimu kimya. Kwenye fainali za NBA zinazoendelea ambazo Warriors wanaongoza 2-0 Curry ameamua kuzindua viatu vyake vipya vinavyoitwa Curry 4s. Sneakers hizi bado hazijaingia sokoni lakini Curry alizitambulisha rasmi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Cavs na anaweza kufurahi sasa kwani washabiki wake na wengine wamevipokea vyema kweli.

Curry amesemekana kuwa hakufurahia kabisa kitendo cha viatu vyake kushuka kwa kiasi kikubwa thamani na kutokuuzika na hivyo kipindi hiki akaamua kusimamia kuanzia idea mpaka utengenezwaji wake mwenyewe na hakutaka kusubiri mpaka mwisho wa msimu huu au msimu ujao bali akataka kuvitumia kwenye fainali za NBA jambo ambalo Under Armor wamefanya.

Mpaka kufikia fainali za mwaka jana wakati Curry akitumia Curry 2, katika miezi 12 alikuwa ameizalishia kampuni ya Under Armour zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 yeye peke yake. Lakini zilipoingia Curry 3 hali ikawa sio shwari hasa pia kutokana na bei yake ya dola 140. Curry na Under Armour kwa pamoja wanategemea viatu hivi (Curry 4) kufanya vyema jambo ambalo linaonekana litafanikiwa. We unavionaje msomaji?

 

Video: Matuta yaliyoipeleka Yanga nusu fainali michuano ya SportPesa

$
0
0

Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia timu hizo kumaliza dakika 90 kwa matokeo ya suluhu.

Shujaa wa mchezo alikuwa golikipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ ambaye alifanikiwa kupangua penati moja ya Clifford Alwanga huku penati ya Stephen Owusu ikigonga mwamba wa juu na kutoka nje.

Yanga walikwamisha penati nne kambani huku Tuster wakifanikiwa kufunga mikwaju miwili na kutupwa nje ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Matuta ya Yanga yamefungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyefunga penati ya kwanza akifuatiwa na Obrey Chirwa, kisha Maka Edward Mwakalukwa na Said Mussa wakafunga penati zao.

Kwa upande wa Tusker, waliofanikiwa kufunga mikwaju ya penati ni Noah Wafula na Brian Osumba.

Matokeo hayo yataikutanisha Yanga na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.

 

“Sijui kama nitabaki Chelsea” Eden Hazard.

$
0
0

Baada ya tetesi za muda mrefu mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard ameweka wazi kuhusu uhamisho wake wa kwenda Real Madrid katika msimu ujao wa ligi.

Hazard amekuwa akihusishwa kuhamia katika klabu ya Real Madrid tangu msimu uliopita lakini msimu huu tetesi zimekuwa kubwa kwamba mshambuliaji huyo anaondoka.

Tetesi hizi zimekuwa zikiongelewa kwa muda mrefu lakini sio upande wa Real Madrid wala Hazard mwenyewe ambao wameshazungumzia uhamisho huo lakini Hazard ameamua kufunguka.

Hazard amesema hajui kuhusu nini kitatokea msimu ujao lakini kama kuna ofa kutoka Madrid ije na wataiangalia kwani ndoto yake na yeye ni kushinda kombe la Champions League siku moja.

“Kuhusu kuondoka tutaliangalia hilo lakini kama kutakuja ofa na zije tuu,kusema ukweli sijui nini kitatokea msimunujao lakini ninachojua ni kwamba nina mkataba na Chelsea wa miaka mitatu”

“Tumekuwa na msimu bora sana katika klabu yetu na kocha wetu mpya na kuingia Champions League tungependa kubeba kombe hilo ila kuhusu kubaki Chelsea hakuna ajuaye kuhusu hilo” alisema Hazard.

Real Madrid usiku wa Jumamosi walifanikiwa kutetea ubingwa wa Champions League na hiyo imewafanya wachezaji wengi dunia kuvutiwa na kuhamia katika klabu hiyo.

 

Hawa wanakaribia kusaini Manchester United na Liverpool

$
0
0

Tayari usajili umeanza kwa nguvu kubwa sana,kila klabu inajitahidi kupata mchezaji imtakaye ili kuimarisha vikosi vyao kabla ya msimu ujao wa ligi kuanza.

Tayari Manchester United wametolewa nje na Antoinr Griezman ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu sasa na hii imewafanya wabadili muelekeo.

Tayari Ivan Perisic winga wa Inter Millan anatajwa sana kwamba huenda safari yake kwenda United imeiva na Inter Millan tayari wameanza kutafuta mtu atakayeziba nafasi ya Perisic.

Lakini Manchester United wanaweza kumtangaza Victor Lindelof wiki hii kama mchezaji wao mpya baada ya kumuwinda kwa muda mrefu.

United wamekuwa wakifanya jitihada za muda mrefu kumnasa mlinzi huyo wa Benfica na sasa inasemelana klabu ya Benfica imekubali kumuuza Lindelof kwa dau la £30m.

Lakini wakati Manchester United wakikaribia kumnunja Lindelof, Liverpool nao wanakaribia kumnunja farao mchezaji wa zamani wa Chelsea Mohamed Salaah.

Inasemekana tayari Liverpool na As Roma wamekubaliana kiasi cha £35m kumnunua Salah ambaye Liverpool walishaonesha nia ya kumtaka hata kabla hajasaini Chelsea.

 

Baada ya Serengeti kukwama Gaboni, huku ndiko Shime anakoelekea

$
0
0

Kocha mkuu aliyekiongoza kikosi cha Serengeti Boys kwenye fainali za AFCON U17 2017 Bakari Shime ‘Mchawi mweusi’ amesema, licha ya kikosi cha JKT Ruvu kushuka daraja bado ataendelea kuwa nayo na atahakikisha anairejesha ligi kuu Tanzania bara.

Shime amesikika akitoa msimamo wake Juni 5, 2017 kupitia Sports Extra ya Clouds FM alipozungumza na Said Karsandasi kutoka jijini Tanga.

“Maisha Yangu yapo kwenye kufundisha mpira kila wakati napenda niishi nikifundisha, niliondoka nikiwa nafundisha JKT Ruvu na kwa bahati mbaya imeshuka daraja bado nitaendelea kuwa nao, kushuka kwao kwangu sio tatizo sana kwa nitaendelea kuifundisha JKT Ruvu hadi pale TFF watakapokuwa wamenipa maelekezo mengine.”

“Nitarudi tuone kama tunaweza kupanda daraja, sioni tatizo kwa sababu hata makocha wakubwa duniani wameweza kufanya hivyo vitu wameshuka na timu na wamepanda nazo kwa hiyo ni sehemu ya kazi na majukumu kwa hiyo kwa sasa siwezi kuwakimbia JKT Ruvu labda itokee ofa ya timu nyingine au kitu kingine.”

“Nimeondoka akili yangu ikiwa JKT Ruvu na nimerudi hivyo lakini kwa upande wa pili nina program na TFF ambazo nazo baada ya fainali zile uongozi utaelekeza nini cha kufanya kwa hiyo kupitia maelekezo hayo nitakuwa na picha rasmi ya mwelekeo katika kazi yangu ya kufundisha.”

Azam wataweza kuishi wanachokiamini?

$
0
0

Azam FC imeanza kuboresha kikosi chake baada ya leo Juni 5, 2017 kuingia mkataba na mshambuliaji Waziri Junior kutoka Toto African ambayo imeshuka daraja, kwa mujibu wa website ya timu hiyo, Junior alipendekezwa na kocha mkuu Aristica Sioaba na amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam.

Azam wamewapa nafasi vijana wengi kutoka kikosi cha vijana na usajili wa mchezaji wao wa kwanza ni mzawa kwa hiyo unaanza kuona wanauvaa uhalisia katika uendesha wa klabu.

Wadau inabidi wawape muda Azam kwa sababu Azam imeamua kuja na aina mpya ya uendeshaji wa klabu yao kwa kuwatumia wachezaji wanaowalea wenyewe huku wakitumia kiasi kidogo cha pesa katika usajili.

Hawajaanza kupata pesa za kutosha zinazotokana na vyanzo vya klabu kwa hiyo unaweza kuhoji pesa nyingi wanazotumia katika usajili wanazitoa wapi? Hapo ndipo kwa wenzetu Ulaya utakutana na rungu la Financial Fair Play .

Endapo vilabu vingine vya Tanzania vitafuata nyayo za Azam katika mfumo wao mpya walioamua kuja nao, kuna kitu kikibwa tutavuna baada ya muda.

Ukiangalia timu kama Mbao FC imeweza kufanya iliyoyafanya msimu huu huku ikiwa na bajeti ndogo tu, kila mtu anaijua historia ya Mbao kwamba ilipewa taarifa ya kucheza ligi kuu siku chache kabla ya msimu kuanza.

Wakasajili vijana ambao hawakuwa na majina makubwa hapo kabla wakawajenga ili kupambana na moto waliouwasha msimu uliopita kila mmoja ameuona na kuvutiwa na timu hii change kwenye soka la Tanzania.

Kwa hiyo watu wameanza kuvutiwa kwamba, inawezekana kuwekeza kwa vijana ikiwa watajengwa vizuri na kuaminiwa.

Lakini kikubwa ni suala la malengo ya klabu, kila klabu ina malengo yake na tamaduni zake iliyojiwekea yenyewe. Kuna klabu ambazo malengo yao ni kuzalisha wachezaji na kuwauza huku ikihakikisha haishuki daraja na wala haipambani kupata ubingwa. Kuna klabu ambazo ndoto zao za kila siku ni kunyanyua ‘makwapa’ hapa utazitaja Simba, Yanga pamoja na Azam.

Sasa kama Azam wtaamua kuchukua ubingwa isiwe kipaumbele chao kwa kuamua kuwatengeneza vijana wao wenyewe, kuwamini na kuwapa nafasi ili badae washindane bila kutumia gharama kubwa kwa kusajili wachezaji wa bei mbaya na kuwalipa mishahara mikubwa.

Mtego kwa Azam ni kwamba, Je, wako tayari kucheza bila presha ya ubingwa? Hapa ndipo inakuja tofauti kati ya Mbao na wao kwa sababu Mbao wanacheza wakiwa hawawazi ubingwa wanachokifanya wao ni kutengeneza timu na kuhakikisha wanakuwa kwenye nafasi nzuri, kama ubingwa ikitokea wamepata ubingwa kama ilivyokuwa kwa Leicester City basi ni jambo jema.


Kivuli cha Bocco kinaendela kuwatesa Azam

$
0
0

Watu wengi bado hawaamini kama John Bocco ‘Adebayor’ kaondoka kwenye kikosi cha Azam, mmoja kati ya watu ambao wamesikitishwa na namna ambavyo nahodha huyo ameondoka katika timu hiyo ni shabiki mkubwa wa Azam anaefahamika kwa jina la Issa Azam ‘mjukuu wa Bakhresa.

Shabiki huyo amesema, kuondoka ni jambo la kawaida ila tatizo ji namna ambavyo Bocco ameondoka ambapo hata yeye hakuridhishwa.

Suala la kuondoka kwa Bocco sio baya kwa sababu wenye timu wameamua kufanya mabadiliko na nia ya Azam ni kufika mbali.

Kuondoka kwa Bocco style ile hata mimi sijaelewa, mimi ninawaomba radhi mashabiki wa Azam Tanzania nzima kwa niaba ya Azam na uongozi wa klabu. Watusamehe kwa sababu Bocco hatukumuondoa ipasavyo na kwa sababu sisi ni binadamu watusamehe.

Tunajua umuhimu wa Bocco na tunajua alikuwa anatusaidiaje na alipoitoa timu. Ni mchezaji mwenye nidhamu Tanzania nzima ana historia ya kuzifunga Simba na Yanga kila siku lakini mwisho wa siku historia yake imeishia pale tunamuomba na yeye atusamehe .

Kwa maoni yangu, Bocco angeandaliwa mechi ya kuagwa halafu sisi ambao tunampenda Bocco tungetoa awadi zetu za heshima kwake kama ishara ya kumuaga, lakini ameondoka kimyakimya mimi sijafurahi. Juzi alinipigia simu tukaongea lakini hatukuongea mambo yanayohusu timu kwa sababu naona aibu kwa sababu nipo ndani ya Azam .

Tunajipanga na timu mpya, asikwambie mtu Azam imekufa atakuwa anaongea uongo kwa sababu timu inakuja upya na malengo ni timu kuwa ya kutisha sana.

Hii ndio safari ya Tiote kutoka mtaani hadi Newcastle mpaka mauti.

$
0
0

Ilikuwa ni mwezi wa sita tarehe 21(siku 15 baada ya leo) lakini huo ulikuwa mwaka 1986 katika mtaa wa Yammousokro nchini Ivory Coast ambapo alizaliwa kijana mwenye nguvu za miguu na mfupi kiumbo aliitwa Cheick Ismail Tiote.

Akiwa na miaka 15 tu alianza kumiliki viatu vya kuchezea mpira na hapo ndipo wazazi na watu mtaani kwao wakajua huyu atakuwa mwanasoka bora siku moja.

Akiwa na miaka 15 tu alianza kucheza soka katika klabu ya nchini Ivory Coast ya Fc Bibo, Tiote aliamua kuachana na kila kitu na hata shule akaachana nayo ili apambane katika soka.

Mungu sii Athumani kwani mwaka 2005 Tiote alifanikiwa kwenda Ulaya kucheza soka, Tiote alisajiliwa katika ligi ya Ubelgiji katika klabu ya Anderchelt.

Maisha ya Anderchelt hayakuwa mazuri sana na klabu hiyo iliamua kumtoa Tiote kwa mkopo kwenda katika klabu ya Roda Jc ambako alipewa nafasi ya kucheza.

Mwaka 2008 Tiote alifanikiwa kusainiwa katika klabu nyingine ya Ubelgiji ya Twente ambako nako kidogo dogo akaanza kupata nafasi ya kucheza.

Mwaka 2010 ndipo alipata nafasi ya kujiunga na Newcasstle ilikuwa tarehe 28 mwezi wa 10 na hapa ndipo Tiote alisema anaona ni kama ndoto zake zimekuwa kweli.

Tarehe 5 mwezi February mwaka 2011 ni siku ambayo mashabiki wa Arsenal hawataweza isahau mkwaju wa Tiote alulowafunga katika mchezo ambao uliisha kwa bao 4 kwa 4.

Tiote ambaye msimu wa mwaka 2013-2014 alipewa unahodha wa Newcastle,ilipofika January mwaka huu ndipo alijiunga na klabu ya Beijing ambako mauti yalimkuta.

 

Mawasiliano ya mwisho ya Cheikh Tiote yavuja.

$
0
0

Ulimwengu wa soka umetawaliwa na wingu jeusi siku ya leo baada ya kifo cha kiungo wa zamani wa klabu ya Newcasstle Cheikh Tiote aliyefariki asubuhi ya Jamatatu.

Sasa mawasiliano ambayo Tiote aliyafanya mara ya mwisho kwa njia ya whatsapp yemevuja, Tiote kwa mara ya mwisho mwisho aliwasiliana na rafiki yake aitwaye Yussuf Tumi.

Habari zinasema Tiote na Tumi ambaye ni mbunifu wa mitindo walikuwa katika mpango wa kuanzisha kampuni yao ya mavazi katika siku za hivi karibuni.

Katika mawasiliano hayo inaonekana Tiote alikuwa akitaniana na Tumi kuhusu masuala ya biashara ambapo Tumi alikuwa na saa na alitaka kumuuzia Tiote.

Tiote alimuambia Tumi kwa utani “inabidi unipe bure” akitaka apewe saa hiyo bure baada ya Tumi kumuambia kuwa alikuwa na mzigo mpya wa saa ambao inabidi aupate.

Tiote na Tumi walionekana kutaniana na Tumi akimuambia Tiote anatamani mungu awasaidie katika mambo yao huku Tiote akimjibu Tumi kwa kumuambia mungu ni mkubwa na atawasaidia.

 

Hili ndio chama bora la CHAMPIONS LEAGUE.

$
0
0

Baada ya fainali ya Champions League kupigwa na Real Madrid kubeba kikombe hicho sasa kikosi bora katika mashindano hayo msimu huu kimeshatajwa huku majina makubwa kama Neymar,Suarez na Paulo Dyabala yakikosekana.

Katika kikosi hicho golikipa wa Juventus Gianluig Buffon amekuwa kipa namba moja wa kikosi hicho huku akisaidiwa na mlinda mlango wa klabu ya Atletico Madrid Jan Oblak.

Katika walinzi yumo mlinzi wa kati wa klabu ya Juventus Leornado Bonnucci huku walinzi watatu wa Real Madrid Sergio Ramos,Marcelo na Dani Carvajal wakiwepo eneo la ulinzi huku mlinzi wa Atletico Madrid Diego Godin naye pia akiwepo.

Katika eneo la kiungo, wachezaji wanne kati ya sita waliochaguliwa katika nafasi hiyo ya kiungo wanatokea Real Madrid ambao ni Casemiro,Modric,Isco na Toni Kroos huku Miralem Pjanic wa Juventus na Tiemoue Bakayoko wa Monaco nao wakiwemo katika kikosi hiki

Katika nafasi ya ushambuliaji Cristiano Ronaldo,Lioneil Messi na Antoine Griezman wapo katila kikosi hicho huku bwanamdogo Kylian Mbappe wa Monaco na Robert Lewandoski wa Bayern Munich nao wakiwepo katika eneo la ushambuliaji.

 

Wachezaji wamlilia Cheikh Tiote.

$
0
0

Hakika atakumbukwa, alikuwa mtu wa mungu na alikuwa kwenye mfungo wa Ramdhan wakati mauti ilipomkuta, Cheikh Tiote kiungo ambaye nashukuru mungu nimeweza kushuhudia akicheza.

Nilivutiwa sana na Tiote hadi wakati Fellaini anajiunga na Manchester United nilitamani pengine labda Tiote ndiye angeenda United na sio Fellaini kutokana na ubora wake.

Baada ya kifo chake hapo jana baadhi ya wachezaji maarufu wameshindwa kuficha hisia zao na kuamua kumlilia Tiote kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Yohan Cabaye ambaye alicheza pamoja na Tiote wakati yuko Newcastle amesema kwamba anakosa hata uwezo wa kuongea kwani kifo hicho kimemuacha katika hali ya uchungu sana.

“Mungu akuangalie huko uliko,maneno yameshindwa kuelezea huzuni niliyonayo moyoni kuhusu wewe,hakika tutakukumbuka Cheikh Tiote” aliandika Cabaye.

Naye mlinzi wa kushoto wa Crystal Palace Andros Townsend amekiri kwamba Tiote ni kati ya watu poa sana na wachangamfu kuwahi kukutana nao katika maisha yake ya soka.

“Ni habari mbaya sana kuhusu Tiote,ni kati ya watu poa sana kuwahi kukutana nao, tutakukumbuka sana Tiote” aliandika Towmsend katila ukurasa wake wa Twitter.

Naye Didier Drogba ambaye ameshawahi kucheza timu moja na Townsend amesema hawezi kusema chochote kuhusu Tiote kwani ni habari iliyomchanganya sana.

Yaya Toure ameandika “kaka yangu Tiote siamini kama umeondoka hakika sitaweza kukusahau” huku Mohamed Salah akiandika “pumzika kwa amani Tiote”

Mchezaji nguli wa zamani wa Uingereza na Newcastle Alan Shearer ameleza pia kushtushwa na kifl cha Cheikh Tiote huku golikipa Rob Elliot akimtaja Tiote kama shujaa.

 

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>