SL Benfica na Manchester United FC ni wapinzani wa muda mrefu katika soka la barani ulaya – wakati United wakiuwinda ushindi wa 3 katika kundi A huku Benfica wakiutafuta ushindi wa kwanza baada ya kupokea kipigo kizito katika mchezo wa mwisho dhidi ya Basel.
Mechi zilizopita
• United wameshinda mechi 6 katika mechi 9 walizokutana, mchezo wa kwanza ulikuwa ushindi wa robo fainali ya michuano ya ulaya msimu wa 1965/66 na baadae katika mchezo wa fainali ya ulaya msimu wa 1967/68 na United wakashinda ubingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza.
• Ushindi pekee wa Benfica dhidi ya United kwa goli la ushindi wa Luisao kwenye ushindi wa 2-1 jijini Lisbon mnamo mwaka 2005, ushindi huo uliiondoa United kwenye makundi ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.
• United walilipa kisasi cha kipigo wakati Louis Saha alipofunga goli pekee katika mchezo uliopigwa September 2006 jijini Lisbon. Mchezo wa marudiano katika dimba la Old Trafford – Benfica walianza kufunga lakini wa mchezo United walishinda 3-1 na kuwaondoa Benfica kwenye hatua ya makundi.
• Timu hizi mbili zilipangwa kwenye makundi msimu wa 2011/12, walitoka sare ya 1-1 jijini Lisbon, Ryan Giggs akifunga goli dakika ya 42 na Cardozo Oscar akifunga dakika ya 24.
• Mchezo wa pili ulikuwa November 2011, goli la kujifunga la Phil Jones na goli la Pablo Aimar yaliipa Benfica sare ya 2-2 baada ya magoli ya Dimitar Berbatov na Darren Fletcher.
• Benfica, wakati huo wakiwa wanafundishwa Jorge Jesus, walishika nafasi ya kwanza kwenye kundi C msimu wa 2011/12, United wakamaliza wa 3 nyuma ya FC Basel
Benfica
• The Eagles walipata kipigo kizito zaidi katika UEFA Champions League baada ya kufungwa 5-0 na Basel.
• Benfica wameshacheza mechi 34 dhidi ya vilabu vya Uingereza; rekodi yao inaonyesha wameshinda mechi 11, sare 6 na wamefungwa 17. Walifungwa na United fainali ya ulaya 1968 na pia wakapoteza mchezo wa fainali ya Europa League dhidi ya Chelsea mwaka 2013 jijini Amsterdam
Manchester United
• Rekodi ya United katika michezo dhidi ya vilabu vya Ureno ugenini ni ushindi mechi 6, sare 2 na wamefungwa 4. Hawajapoteza mchezo hata mmoja katika mechi 5 zilizopita nchini humo – mara ya mwisho kufungwa ilikuwa 2005 vs Benfica.
• Huu ni msimu wa 21 katika UEFA Champions hatua ya makundi, ni mara ya 4 tu ndio wameshindwa kuvuka hatua hiyo. Mara 2 kati ya 4 walizotolewa ilikuwa katika misimu 4 iliyopita; United walimaliza nafasi ya 3 msimu wa 2011/12 na 2015/16, msimu wa mwisho katika UCL.
• Mourinho alianza kufundisha soka akiwa Benfica mnamo September 2000, lakini hakukaa sana zaidi ya miezi ya miwili tu. Misimu mitatu iliyofuata alikuwa UD Leiria na FC Porto, alikutana na Benfica mara 7 (Ushindi 4, sare 2, amepoteza 1). Kipigo pekee alipata katika mchezo wa fainali ya kombe la Ureno msimu wa 2003/04.
• Victor Lindelöf amejiunga United akitokea Benfica mwanzoni mwa msimu huu, akiwa ameitumikia Benfica mara 48 katika miaka mitano aliyokaa na klabu hiyo ya Ureno.
• Nemanja Matić alikuwa Benfica kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014, alifunga magoli 7 katika mechi 56 za ligi.
• Rui Vitória akiwa UD Vilafranquense walifungwa 4-0 ugenini na Porto ya Jose Mourinho msimu wa 2003/04.
Taarifa za Vikosi
•Manchester United leo wamepata ahueni baada ya Luke Shaw na Marcos Rojo wamejumuishwa katika kikosi kilichosafiri kwenda Lisbon.
United bado itamkosa Paul Pogba, Maroune Fellaini na Michael Carrick.
•Benfica wao watamkosa André Almeida ambaye ana kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopata dhidi ya FC Basel.