Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Kuelekea Dar derby, takwimu zinaonesha Lwandamina ni kibonde kwa Omog

$
0
0

Mechi ya Yanga vs Simba itakayochezwa October 28, 2017 inazalisha mechi nyingine ndani yake (yani mechi ndogo ndani ya mechi kubwa).

Leo tuanze na mechi ya makocha (George Lwandamina wa Yanga vs Joseph Omog wa Simba) ambao watakuwa na vita yao kuhakikisha mbinu zao zinaleta matokeo kwenye vikosi vyao.

Hawa wazee watakuwa wakikutana kwa mara ya nne, kabla ya hapowalishakutana katika michezo mitatu ya mashindano yote (VPL, Mapinduzi Cup na Ngao ya Jamii.)

Katika mechi zote hizo Joseph Omog anamatokeo mazuri dhidi ya Lwandamina, ameshinda mechi zote tatu walizokutana (mechi mbili kwa penati) na mchezo mmoja ameshinda ndani ya dakika 90.

Kwa mara ya kwanza Omog na Lwandamina kukutana ilikuwa ni January 10, 2017 mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup viwani Zanzibar. Simba walishinda kwa penati 4-2 baada ya kutoka suluhu (0-0) ndani ya dakika 90.

Mara ya pili walikutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara tarehe 25/02/2017 Simba ikashinda 2-1 kwa magoli ya Shiza Kichuya na Laudit Mavugo, Simon Msuva alifunga goli la Yanga kwa mkwaju wa penati.

Pambano la tatu kati ya Omog na Lwandamina ilikuwa ni August 23, 2017 mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Simba walishinda kwa penati baada ya mechi kumalizika bila timu zote kufungana ndani ya dakika 90. Simba walishinda kwa penati 5-4.

  • 10/01/2017 (Mapinduzi Cup) Simba 0-0 Yanga (Penati 4-2)
  • 25/02/2017  (VPL) Simba 2-1 Yanga
  • 23/08/2017 Yanga 0-0 Simba (Penati 4-5)

Jumamosi ijayo October 28, 2017 wababe hawa wataongoza wachezaji wao kutafuta matokeo kwenye mechi ya VPL, Lwandamina atakubali kunyanyaswa na Omog au atakata ‘utepe’ wa ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya Omog?


Makonda mekabidhi generator chama cha basketball Dar

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Jumanne October 24, 2017 ametoa msaada wa Generator ya kisasa, Mabati 150 na mipira 110 kwa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam ili kujengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.

Generator hiyo ya kisasa ina uwezo wa KV 35 na haitoi muungurumo wa sauti (silent) ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.

Makonda amesema anataka kuona timu ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa itakayotoa wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ndani na nje ya nchi.

Uamuzi wa Makonda kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa kikapu uwanja wa taifa na kujionea uchakavu wa bati unaosababisha wachezaji kunyeshewa na mvua, ukosefu wa Generator umeme ukikatika na uhaba wa mipira hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.

Aliahidi kujenga viwanja vitatu vya mchezo wa kikapu ambapo tayari ramani imetengenezwa na muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa viwanja hivyo.

Ili kuendelea kuimarisha michezo Dar es salaam, anaunda kamati maalum ya kushughulikia michezo ya aina zote.

Tayari amepata mdau atakaejenga Swimming pool la kisasa Kinondoni kwaajili ya mchezo wa kuogelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam Okare Emesu amemshukuru Makonda kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.

“Nitafunga tu, Lipuli hakuna tatizo”-Salum Machaku

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI wakipambana na kupata nafasi ya kurejea ligi kuu Tanzania Bara baada ya kukosekana kwa misimu isiyopungua 15, jina la kiungo-mshambulizi wa zamani wa Azam FC, Mtibwa Sugar, Simba, Salum Machaku lilitawala katika vinywa vya wapenzi wa soka Mkoani Iringa na kijana huyu kutoka Morogoro alitoa mchango mkubwa ili kuirudisha VPL timu ya Lipuli FC.

Machaku alifunga jumla ya magoli 13 katika michezo 14 na kuibuka mfungaji bora wa klabu yake na ligi daraja la kwanza msimu uliopita. Kabla ya mchezo ambao timu yake iliifunga Majimaji FC siku ya Jumapili katika uwanja wa Samora, Iringa mambo yameonekana kwenda ‘mrama’ kwa Machaku kwani alikuwa amecheza michezo miwili tu ya Lipuli katika ligi kuu msimu huu.

“Nimefanikiwa kucheza michezo miwili tu hadi sasa katika ligi. Nilimaliza dakika zote 90’ katika mchezo ambao tulitoka suluhu ya Njombe Mji, na ule wa ushindi dhidi ya Stand United ambao sikumaliza dakika 90.” Anasema Machaku nilipofanya naye mahojiano siku ya Ijumaa iliyopita akiwa Iringa.

Kutoka kuwa mfungaji bora wa klabu na ligi daraja la kwanza hadi kuwa mchezaji anayetafuta nafasi ya kucheza hivi sasa ni jambo la kuumiza hasa pale wachezaji wanaopewa nafasi hiyo wanaposhindwa kufunga.

Lipuli FC imefunga magoli manne tu katika michezo 7 ya VPL na Machaku ameanza kuzoea maisha ya benchi katika timu hiyo chini ya makocha Amri Said na msaidizi wake Selemani Matola.

“Ushindani ndiyo humkuza mchezaji. Ukitazama safu yetu ya ushambuliaji utawaona wachezaji kama Busungu, Lambele, Karihe, Wazir, Dotto Kayombo, Moka Shaaban na mimi mwenyewe. Hawa wote wanataka kucheza na kitendo cha sisi kuendelea kushindania nafasi ndiyo kunaifanya timu iimarike.” Anasema mchezaji huyo mshindi mara moja wa VPL.

“Ninajisikia vizuri katika timu hii. Nafasi itakapopatikana nitajitahidi kufanya vizuri kwa manufaa ya timu yangu. Tuna makocha wazuri na wanatusaidia sana. Kumbuka timu yetu ndiyo kwanza imetoka ligi daraja la kwanza hivyo kuna changamoto nyingi ambazo klabu lazima itapitia hasa wakati huu ligi ikiwa mwanzo.”

Cristiano Ronaldo anataka kushinda tuzo 7 za dunia na haya ndio matarajio yake katika World Cup 2018

$
0
0

Cristiano Ronaldo alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa FiFA kwa mara ya pili mfululizo jana jijini London, na nahodha wa Ureno jana baada ya kumalizika kwa shughuli ya ugawaji wa tuzo alifanya mahojiano na FIFA.

FIFA.com: Cristiano Ronaldo, hii ni awamu ya pili ya ufanyikaji wa tuzo za The Best FIFA Football Awards, na ni mara ya pili unashinda, unajisikiaje?


Cristiano Ronaldo:
Ni kitu kikubwa kwangu. Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu. Ni hatua kubwa kwenye maisha yangu ya soka, ninajisikia furaha sana.

Hii ni mara ya tano unapata heshima ya kuwa mchezaji bora kabisa wa soka, je heshima hii inakufanya kuwa miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea?
Nina furaha sana kushinda hii tuzo leo, lakini kitu nilichotaka tangu mwanzo ni kuwa na mafanikio katika huu mchezo na nashukuru nimefanikisha hilo. Kushinda makombe na kuwa miongoni mwa wachezaji tuzo nyingi binafsi ni jambo la kujivunia sana. Ni vitu ambavyo siwezi kusahau kwenye maisha yangu na vinazidi kunipa msukumo wa kujituma kwa kadri ninavyoweza.

Hivi karibuni umepata mafanikio ya kutwaa taji kubwa ukiwa na timu yako ya taifa ya Ureno, ushindi wa Euro 2016 na kuelekea fainali za kombe dunia 2018 nini mategemeo yako?


Ushindi wa wa EURO 2016 ulikuwa muhimu, kombe kubwa ngazi ya kimataifa ndio kitu kilichokuwa kinamiss kwenye kabati langu la mafanikio. Nashukuru mwaka huu tumefuzu na tunajiandaa kwenda Russia tena.

Tuizungumzie Russia, nchi ambayo uliitembelea wakati wa mashindano ya FIFA Confederations Cup.

Tayari nimeshacheza Urusi mara nyingi. Nimeshinda ubingwa wa Champions League kule, ni nchi ambayo nina bahati nayo. Lakini bahati haikuwa yetu, tulishindwa kushinda taji la Kombe la mabara, lakini nilipata uzoefu mpya.

Baada ya ushindi wa UEFA EURO 2016, baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakiipa nafasi Ureno kutwaa kombe la dunia. Unakubaliana na utabiri wao?


Hilo linaeleweka. Sisi ni mabingwa watetezi wa ulaya na hilo bila shaka linaongeza mategemeo, lakini ningependa kurudia nilichosema kabla ya EURO 2016: Ureno sio timu ambayo huwa inapewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa. Kuna timu nzuri zaidi yetu ukiangalia kwenye ukubwa wa kikosi, na mafanikio waliyonayo. Hivyo sisi tutaingia huku tukifahamu hilo, japokuwa tutajitahidi kufanya vizuri.

Umeshashinda tuzo 5 za uchezaji bora wa dunia. Ungependelea kumaliza na ngapi katika maisha yako ya soka?
7, ningependelea kushinda idadi hiyo, 7 ndio namba yangu ya bahati. Lakini hayo yote yapo kwenye wakati ujao, kwa sasa nitaendelea kujituma na kufurahia matunda ya jitihada zangu.

Cr7 na Lioneil Messi nani ana tuzo nyingi zaidi?

$
0
0

Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi ndio wanasoka ambao kwa sasa ndio bora duniani, hilo halina ubishi. Kama kuna mchezaji mwingine bora ni bora baada ya wanasoka hao wawili.

Kwa sasa katika dunia ya sasa hakuna mwanasoka ambaye siyo tu kugusa bali hakuna hata anayekaribia level za tuzo za wanasoka hawa wawili kwani miaka 

Cristiano Ronaldo amemburuza Lioneil Messi katika jumla ya tuzo binafsi ambapo kabati la Ronaldo limebeba tuzo 287 huku kabati la Lioneil Messi hadi sasa likiwa limebeba jumla ya tuzo 157.

Lakini Lioneil Messi amemburuza Ronaldo katika tuzo ya Ballon D’Or ambalo Muargentina huyo ana tano huku Cr7 hadi sasa akiwa na nne lakini baadae mwaka huu anatarajia kubeba tuzo ya Ballon D’Or ya tano.

Lioneil Messi pia amempoteza vibaya Cristiano Ronaldo katika ligi ya La Liga ambapo Messi amechukua tuzo ya mchezaji bora wa La Liga mara sita ambapo Cristiano Ronaldo yeye amechukua mara moja tu.

Pamoja na kwamba majina ya hawa wote yamejitokeza katika kikosi cha FIFA mara 11 lakini kinachombeba Cr7 ni ushiriki wake katika ligi kubwa mbili barani Ulaya La Liga na Epl huku kote akibeba makombe.

Kwa ujumla katika tuzo kubwa ambazo zinafahamika dunia nzima Cristiano Ronaldo amezibeba tuzo 157 akiwa amemzidi tuzo 27 Lioneil Messi ambaye ana tuzo 130.

Roho yamuuma Diego Maradona  kumkabidhi tuzo Cr7

$
0
0

Habari kubwa jana na leo ni kuhusu Cristiano Ronaldo, Mreno huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya The Best Fifa Player Of The Year 2017 ikiwa ni mara ya pili mfululizo na akimbwaga mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi.

Katika utoaji wa tuzo hizo usiku wa jana mjini London gwiji wa Argentina Diego Maradona alitoa tuzo ya mchezaji bora wa kiume iliyokwenda kwa Cr7 na Maradona kukiri kutofurahia jambo hilo.

Maradona anasema angefurahi kama tuzo hiyo asingeimkabidhi Cristiano Ronaldo na badala yake angemkabidhi Muargentina mwenzake Lioneil Messi ambaye naye alikuwepo katika usiku wa tuzo hizo.

Maradona ambaye aliwahi kuwa kocha wa Lioneil Messi katika timu ya taifa mwaka 2008 na 2010 amesema jambo la kumpa Ronaldo tuzo hiyo lilikuwa likimuumiza roho wakati akitekeleza suala hilo.

Lakini Maradona amekiri kufurahia kuonana na Lioneil Messi kwani wawili hao walitajwa kuwa na msuguano jambo ambalo lilithibitika zaidi pale Messi alipomtosa kadi ya mualiko Maradona katika harusi yake.

Maradona alimponda Messi kwa kutokuwa kiongozi bora wa timu ya taifa lakini usiku wa jana amekiri kwamba Muargentina huyo ni muhimu kwa timu yao ya taiafa na atakuwa bora kwa muda mrefu zaidi.

Dogo aliyewavusha Arsenal alikataliwa Chelsea

$
0
0

Michuano ya Efl Cup iliendelea usiku wa jana kwa Manchester United na Arsenal kufudhu katika robo fainali ya michuano hiyo, lakinj shukrani kwa wachezaji makinda kuwabeba katika mechi hizo.

“Litle Eddie” hilo ni jina la utani la bwanamdogo Eddie Nketiah ambaye ana umri wa miaka 18 tu na jana Arsene Wenger alijaribu kumpa nafasi Nketiah katika mchezo wa jana akitokea benchi.

Wakati Nketiah akipewa nafasi tayari Arsenal walikuwa wamelala bao moja lakini zikiwa zimebaki dakika 5 mpira kuisha isawazisha kabla yadakika ya 96 kuongeza bao lingine na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga akiwa amezaliwa wakati Wenger ni kocha wa Arsenal.

Nketiah na zao la Chelsea na waligundua kipaji chake mwaka 2014 alipokuwa timu za mtaani lakini baadae Chelsea waliachana naye ndipo Arsenal wakamchukua na msimu wa mwaka juzi tu akiwa na miaka 16 alifunga mabao 24 katika mechi 28 za under 18.

Manchester United nao jana walikuwa na kiungo kinda aliyekichafua sana katikati ya uwanja Scott Mc Tominay, kiungo huyu alizaliwa Uingereza na klabu yake ya kwanza kuichezea ilikuwa Manchester United.

Alex Tuenzebe naye sio jina jipya lakini amezidi kudhihirisha ubora wake baada ya kiwango kizuri sana usiku wa jana na shukrani zimuendee Jesse Lingard kwa kufunga mabao yote mawili yaliyowavusha United.

Leicester City nao wamefudhu baada ya kuinyuka Leeds mabao 3 kwa moja, Manchester City wakashinda kwa mikwaju ya penati huku Afc Bournemouth wakiitoa Middlesbrough.

“Sikupiga kura kuchagua mchezaji bora wa FIFA 2017”-Samatta

$
0
0

Nahodha wa timu ya taifa ya ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta amesema hakuhusika katika zoezi la kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa FIFA 2017 (The Best FIFA Football Awards 2017).

Samatta amesema hakuwepo lakini alifahamishwa baadae kuwa walimjazia nafasi yake kama nahodha lakini kama angepiga kura mwenyewe angemchagua Messi, Ronaldo kisha Neymar.

“Sikuhusika na uchaguaji wa majina ya wachezaji bora, sikuwepo, nilifahamishwa baadae kuwa walinijazia nafasi ya captain, ila bora wangu walikuwa Messi, Ronaldo na Neymar”-Samatta.

Ukiangalia kwenye documents za FIFA za manahodha waliopiga kura kuchagua mchezaji bora mwaka 2017 Samatta anaonekana aliwatosa Ronaldo na Messi na kura yake ilikwenda kwa Neymar, N’golo Kante na Pierre Aubameyang.


Kuelekea Dar derby: Mchezaji wa Yanga anaamini Simba wapo kwenye presha kubwa

$
0
0

Beki wa zamani wa Tanzania Prisons na Yanga Samson Mwamanda amesema, kuelekea mechi ya watani wa jadi klabu ya Simba ndio itakuwa kwenye presha kubwa ya kuhitaji matokeo ya ushindi kwa sababu ya aina ya kikosi walichonacho ukilinganisha na wenzao Yanga.

Mwamanda ameshawahi kucheza mechi za Yanga na Simba miaka kadhaa iliyopita anaamini mashabiki na viongozi wa Simba wanaamini kikosi chao ni kizuri kuliko cha Yanga hivyo hawaoni kama Yanga wana nafasi ya kushinda mechi hiyo.

“Kutokana hali ilivyo, Simba wana wakati mgumu sana kwenye mechi ijayo kutokana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki na viongozi kwa sababu ya kikosi chao kuwa kipana sana, wanawachezaji wenye uzoefu kwa hiyo mashabiki na viongozi wanaimani timu yao itashinda.”

“Kwa upande wa Yanga kwa jinsi walivyoonesha kiwango kwenye mechi iliyopita na matokeo waliyoyapata yatawasukuma kwenda kwenye mechi dhidi ya Simba wakiamini watapata aina yoyote ya matokeo.”

“Nawapa nafasi kubwa sana Simba kwenye mchezo wa Jumamosi lakini kutokana na uzoefu wangu napata wasiwasi hasa timu hizi mbili zinapokutana, unaweza ukaiona Yanga au Simba ni dhaifu lakini matokeo yanakuja kuwa tofauti lakini pia inategemea na bahati kwa sababu kwenye mchezo wa soka inanafasi yake.”

Simba walifanya usajili wa wachezaji wengi wenye majina makubwa ndani na nje ya nchi huku wakiwa wazoefu wa ligi kuu Tanzania bara kama Emanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Aishi Manula na wengine wengi.

Kuelekea Dar derby: “Sidhani kama Omog atabaki salama”-Mchezaji wa zamani Yanga

$
0
0

Mechi za Simba na Yanga hufukuzisha kazi makocha wengi ambao hupoteza mechi hiyo ya mahasimu wa soka Bongo, imekuwa ni kawaida kushuhudia kocha anatupiwa virago anaposhindwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya wapinzani wake, wala si jambo la kushangaza kabisa kwa vilabu hivi vikongwe nchni.

Utaratibu huo ndio unamfanya beki wa zamani wa Yanga Samson Mwamanda kuamini kwamba kocha wa Simba Joseph Omog anaweza kuwa kwenye wakati mgumu ikitokea akapoteza mechi ya Yanga Jumamosi October 28, 2017.

“Hii mechi ya Jumamosi Yanga vs Simba, mimi ninawasiwasi sana na upande wa Msimbazi kwa maana moja, Joseph Omog atakuwa na wakati mgumu sana endapo atafungwa, si dhani kama atabaki salama. Hizi timu watu hawapendi kufungwa, zinapokuwa zimefungwa viongozi wao ili wajisafishe kwa  wanachama na wapenzi, lazima watafute sehemu ya kutupia mzigo”-Samson Mwamanda.

Imesha sikika mara kadhaa kwamba, Omog ataondoka kwenye kikosi cha Simba kwa sababu ameshindwa kupata matokeo kwenye baadhi ya mechi za ligi msimu huu lakini Simba wamekuwa wakitoa taarifa rasmi kwamba kocha huyo bado ana mkataba na klabu haina mpango wowote wa kumuondoa kikosini.

Kuelekea Dar derby: Manara anataka Ajib afananishwe na Okwi sio Niyonzima

$
0
0

Baada ya mitandaoni kuchafuka kwa wadau wa soka kuwafananisha wachezaji wawili wa Simba na Yanga Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib, afisa habari wa Simba Haji Mnara amesema, watu wasimfananishe Ajib na Niyonzima badala yake wawafananishe Ajib na Emanuel Okwi.

Manara amesema Niyonzima na Ajib wanacheza nafasi tofauti Niyonzima ni kiungo na Ajib ni mshambuliaji lakini Ajib na Okwi wote ni washambuliaji hivyo wanamfanano wa moja kwa moja.

“Haruna asifananishwe na Ajib, Ajib mnanano wake uwe ni Okwi kwa sababu wao wote ni washambuliaji. Ajib ni striker na Okwi ni striker, Haruna ni kiungo unawafananishaje,ni sawa kuwafananisha Mohamed Ali na Bruce Lee nani anajua kupigana. Wote wanacheza mchezo wa ugomvi lakini mmoja anacheza boxing mwine kung fu,” Manara aliiambia K TV ya visiwani Zanzibar ambako Simba imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Yanga Jumamosi October 28, 2017.

“Mfananisheni Ajib na Okwi. Okwi ana magoli nane Ajibu ana magoli matano, Okwi ana assists nne Ajibu ana mbili, mbingu na ardhi. Tumemruhusu Ajib aende Yanga tukamleta Okwi ni kama vile kwenye timu umruhusu Mohamed Salah aende kwenye timu nyingine halafu umlete Messi.”

“Kwa historia, Okwi anafunga kila mahali lakini Ajib hata timu ya taifa hana namba ya kudumu Tanzania ambayo inashika nafasi zaidi ya 130 kwenye viwango vya FIFA Okwi anacheza Uganda timu  ambayo ipo kwenye nafasi 70 bora za viwango vya FIFA na anafunga sio na Somalia na Burundi ila anawafunga Misri sasa fananisha Okwi na Ajib uone mbigu na ardhi iliyopo hapo. Sio kama simthamini, Ajib ni best player lakini juu yake kuna best,best, best, Emanuel Okwi.”

Hadi sasa Okwi ndio anaongoza kwa magoli katika orodha ya wafungaji wa VPL akiwa amefunga magoli nane katika mechi sita alizocheza huku Ajib akiwa na magoli matano baada ya kucheza mechi saba. Haruna Niyonzima bado hajafunga tangu aliposajiliwa kujiunga na Simba akitokea Yanga wakati wa dirisha la usajili kabla ya kuanza kwa msimu huu (2017/2018)

Hivi ndivyo kesi ya Paul Pogba na Juventus ilivyoisha

$
0
0

Klabu ya Juventus ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi na shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na kile kilichodaiwa kwamba walikiuka kanuni za masuala ya usajili katika mauzo ya Paul Pogba kwenda United.

Hiyo ilikuwa miezi michache iliyopita lakini hii leo kumetolewa taarifa mpya na FIFA ambapo shirikisho hilo la soka duniani limeishafisha Juventus katika kashfa hiyo na kusema hawakufanya kosa lolote.

Msemaji wa FIFA katika taarifa yake amesema kamati ya nidhamu ya FIFA imefuta kesi hiyo dhidi ya Juventus na kusema kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuiendeleza kesi hiyo dhidi ya Juventus.

Wakati Paul Pogba akisajiliwa na United kwa ada ya £89m mengi yalizungumzwa kuhusu usajili huo huku kiasi ambacho alikipata wakala wa Paul Pogba bwana Mino Raiola  kilizua mashaka kuhusu usajili huo.

Kwa sasa kiungo Paul Pogba yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha yake iyoyapata katika mchezo wa Champions League dhidi ya Fc Basel huku akitarajiwa kurejea uwanjani katikati ya mwezi ujao.

TFF imetangaza ratiba ya kwanza FA Cup 2017-18

$
0
0

Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), imezinduliwa rasmi leo Jumatano Oktoba 25, 2017 kwa droo maalumu kwa timu zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali.

Droo hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam ambako Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema: “Michuano ya msimu huu itaanzia hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.”

Amesema kwa ujumla tu, michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, itashirikisha timu 91 msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).

Kwa kuanzia hatua ya awali, kundi la timu 27 la RCL timu sita zitakazocheza mechi tatu baada ya wachezaji watatu wa zamani wa timu ya taifa Abeid Mziba ‘Tekelo’, Boniface Pawasa na Salum Sued ‘Kusi’ kuchagua vitufe sita ili kupata timu hizo.

Timu zilizopatikana katika droo hiyo hatua ya awali Buselesele ya Geita itayocheza na Green FC ya Songwe; Kisarawe United ya Pwani itacheza na Silabu ya Mtwara ilihali Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga kati ya Oktoba 31; Novemba mosi au mbili.

Raundi ya Kwanza ya ASFC itaanza Novemba 7, 8 au 9 ambako timu zilizochaguliwa kwenye droo hiyo ni kama ifuatavyo:

Mashujaa ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buselesele ya Geita na Green FC ya Songwe; wakati mechi nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora ilihali Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.

Kwa mujibu wa droo, Mji Mkuu FC ya Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza na Ndovu ya Mwanza.

Changanyikeni ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors ya Kinondoni wakati Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.

Michezo mingine ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia ya mjini humo wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati The Mighty Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.

Timu ya Burkina FC ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako Heroes ya Njombe  itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja Moja itapambana na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African Sports ya Tanga.

Mechi nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini FC ya Arusha ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati New Generation itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza na Kitayose ya Kilimanjaro.

Antonio Conte kutimuliwa Chelsea? Wengine hawa hapa

$
0
0

Uwekezaji unaofanywa na timu za barani Ulaya haswa Uingereza unawafanya mabosi kukosa uvumilivu kwa makocha wao, miezi mitatu tu tayari Craig Shakespaere, Ronald Koeman na Frank De Boer wametimuliwa lakini nani amafuatia?

Antonio Conte? Ni kocha ambaye ana presha kubwa sana kwa sasa, aliwapa Chelsea ubingwa msimu uliopita lakini matokeo ya siku za hivi karibuni ya Chelsea yanaweza kumtibua tajiri Abromovich.

Katika michezo minne ya Chelsea iliyopita wameshinda mchezo mmoja tu na hiyo inazidisha presha darajani huku tetesi kutoka klabuni hapo zinasema kuna msuguano wa chinichini kati ya Conte na viongozi wa timu.

Slaven Bilic, sasa achana na Conte ,kocha wa West Ham Slaven Bilic anaonekana wazi kwamba anaweza kuondoka wakati wowote kuanzia sasa kutokana na ubovu wa West Ham msimu huu.

Hawana matokeo mazuri hata kidogo katika Epl lakini kipigo cha bao 3 kwa sifuri toka kwa Brighton Ijumaa iliyopita kinaweza kumuweka Bilic kwenye nafasi kubwa kufungashiwa virago.

Mark Hughes, Stoke City nao pamoja na mwenyekiti wa timu kumuunga mkono Hughes lakini uwepo wao katika nafasi ya 17 unatishia uhai wao katika Epl na ni wazi mabosi wa Stoke hawatakuwa tayari kuvumilia hilo.

Paul Clement, Clement na yeye ni kati ya wanaopewa nafasi kubwa kuondoka Epl, wameshapigwa mara 5 katika michezo 9 huku jana wakitolewa katika michezo ya Efl na wiki ijayo wako na Arsenal.

Maurcio Pellegrino, Southampton wamesuluhu mara tatu, wamepigwa mara tatu na kupata ushindi mara nne lakini mabosi hawaridhiki na maendeleo ya katika timu hiyo kwani hadi sasa wako nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi.

Samatta kaukimbia ukame wa mabao

$
0
0

Usiku wa Jumatano October 25, 2017 nahodha wa Tanzania na klabu ya Genk ya Ubelgiji alifunga bao moja wakati timu yake ikipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Club Brugge kwenye uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena.

Samatta amefunga goli lake dakika ya 90 na kumaliza wimbi la kucheza bila kufunga ambapo alishacheza mechi tisa bila kutupia kabambani kabla ya kuwafunga Brugge, bao la kwanza la Genk limefungwa na Ruslan Malinovskiy dakika ya 43 kipindi cha kwanza.

Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Genk katika mechi tano zilizopita, kabla ya ushindi huo waliwafunga Anderlecht 1-0 ugenini.

Matokeo ya Genk katika mechi tano zilizopita

  • Genk 1-1 KV Oostende
  • AS Eupen 3-3 Genk
  • Genk 1-1 Royal Excel Mouscron
  • Anderlecht 0-1 Genk
  • Genk 2-0 Club Brugge

Kama unafuatilia ligi ya Ubelgiji (First Division A) ni kwamba, Club Brugge ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 30, kipigo kutoka kwa Genk ni cha pili kwao wakiwa wamesha cheza mechi 12 wameshinda 10 na kupoteza michezo miwili hawajatoka sare hata mechi mmoja.

Ushindi wa Genk dhidi ya Brugge unawafanya wafikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi 12 na wamepanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi. Katika mechi 12 ambazo Genk wamecheza, wameshinda nne, sare tano huku wakipoteza mechi tatu. Wamefunga magoli 20 huku wenyewe wakiwa wameruhusu kufungwa magoli 17 hivyo kufanya wastani wa magoli kuwa ni tatu.

October 28, 2017 Genk watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Kortrijk mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji.


Kuelekea Dar derby: Takwimu za Simba, Yanga, mechi za nyumbani na ugenini

$
0
0

Jumamosi October 28, 2017 kitawaka pale uwanja wa Uhuru utakapochezwa mchezo wa ligi kuu Tanzania Yanga vs Simba mzunguko wa nane wa ligi hiyo.

kabla ya mechi hiyo kupigwa, kuna takwimu muhimu za kufahamu ili kujua ubora wa kila timu na mapungufu yake inapocheza ugenini au uwanja wa nyumbani.

Simba

  • Nafasi: 1
  • Mechi ilizocheza: 7 Nyumbani: 3 Ugenini 4
  • Ushindi: 4 Nyumbani: 3 Ugenini: 1
  • Sare: 3 Nyumbani: 1 Ugenini: 2
  • Kupoteza: 0 Nyumani: 0 Ugenini: 0
  • Magoli ya kufunga: 19 Nyumbani: 15 Ugenini 4
  •  Magoli ya kufungwa: 4 Nyumbani: 1 Ugenini: 3
  • Pointi: 15 Nyumbani: 10 Ugenini: 5
  • Cleen sheets: 4 Nyumbani: 3 Ugenini: 1
  • Mechi waliyoshindwa kufunga goli: 1 Nyumbani: 0 Ugenini: 1
  • Ushindi Mkubwa: 7-0 Nyumbani: 7-0 Ugenini: 2-1
  • Kipigo kikubwa: 0

Yanga

  • Nafasi:2
  • Mechi ilizocheza: 7 nyumbani: 3 ugenini: 4
  • Ushindi: 4 nyumani: 1 ugenini 3
  • Sare: 3 nyumbani: 2 ugenini: 1
  • Kupoteza: 0 nyumbani: 0 ugenini: 0
  • Magoli ya kufunga 10 nyumbani: 2 ugenini: 8
  • Magoli ya kufungwa:3 nyumbani: 1 ugenini 2
  • Pointi: 15 nyumbani: 5 ugenini: 10
  • Clean sheets: 4 nyumbani: 2 ugenini: 2
  • Mechi waliyoshindwa kufunga goli: 1 nyumbani: 1 ugenini: 0
  • Ushindi mkubwa: 4-0 Nyumbani: 1-0 Ugenini: 4-0
  • Kipigo kikubwa: 0

Nou Camp kubadilishwa jina kuanzia msimu unao.

$
0
0

Klabu ya Barcelona inataraji kubadili jina la uwanja wao wa sasa wa Nou Camp na kuwa “Nou Camp Grifol” jina ambalo litaanza kutumika katika msimu ujao wa ligi wa 2018/2018.

Barcelona wamekubali kubadili jina hilo baada ya kusaini dili na kampuni inayohusiana na masuala ya madawa na kemikali iitwayo Grifol ambapo dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya kiasi cha £340m.

Makataba wa Grifol na Barcelona utawafanya Grifol kulipia marekebisho ya uwanja wa sasa wa Barcelona lakini vile vile mkataba huo wa Grifol unaweza kutumika katika mkataba mpya wa Lioneil Messi.

Redio mmoja nchini Hispania usiku wa jana ilitangaza dili hilo na kusema Grifol wako tayari kutoa kiasi £535m kwa ajili ya matanuzi na kuuboresha upya uwanja wa sasa wa Barcelona.

Dili hili linataraji kuwaboost Barcelona katika mkataba mpya wa Lioneil Messi ambaye hadi sasa hajasaini mkataba mpya kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho Messi anataka kupewa katika mkataba huo.

Kisa cha mtoto aliyeokota pesa na kumtumia Mooy akimshukuru kwa kuiadhiri Manchester United

$
0
0

Aaron Mooy wikiendi iliyopita alikuwa gumzo kubwa sana kutokana na kiwango kikubwa sana alichokionesha dhidi ya United na kusababisha kipigo cha kwanza kwa Manchester United katika msimu huu wa ligi.

Sasa kuna mshabiki mmoja ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 9 ambaye ni shabiki wa Huddersfiled United alishindwa kuzuia hisia zake baada ya ushindi wa Hudders na kiwango kikubwa cha Mooy.

Dogo huyu anaitwa Adam Bhana aliamua kuchukua kiasi cha pesa alichokiokota uwanjani wakati wa mchezo dhidi ya United na kuamua kumtumia Mooy kama shukrani ya kile alichowafanya Manchester United.

Baba wa mtoto huyo amesema mwanzo mwanae alitaka kutoa kiasi hicho kidogo cha pesa kwa timu ili aweze kuwasaidia kumnunua Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid lakini baadae alibadili mawazo.

Katika kipande cha barua ambacho alikiambatanisha na pesa hiyo Adam aliandikia Huddersfield na kuwaomba wamfikishie Aaron barua na pesa hiyo na kisha kuituma barua hiyo kwa timu.

Adam Bhana alimwambia baba yake wasingeweza kukaa na kiasi hicho cha pesa kwa kuwa hawakustahili kukaa nayo na ilistahili kwenda Mooy kutokana na furaha aliyowapa mashabiki wa Huddersfield.

Tayari Mooy amejibu ujumbe wa shabiki huyo na kumuomba waonane ili amshukuru kwa kiasi cha pesa alichompa na ujumbe aliomuandikia katika mchezo huo.

Hii ndio sababu ya Chelsea kumuacha Eddie Nketiah kabla Wenger kumkamata

$
0
0

Eddie Nketiah amekuwa gumzo sana wiki hii baada ya kuibeba Arsenal katika mchezo wa Carbao Cup na kuipeleka Arsenal katika robo fainali ya michuano hiyo.

Eddie Nketiah alinaswa na rada za Arsenal mwaka 2015 ambapo alikuwa hana timu baada ya kuachwa na Chelsea na kurudi kucheza mtaani kwao.

Lakini nini haswa kilipelekea Chelsea kumuacha Nketiah? Taarifa zinasema klabu ya Chelsea iliamua kuachana na Eddie kutokana na umbile lake ambalo lilionekana dogo.

Taarifa zinasema academy ya Chelsea moja kati ya vigezo vyao vikubwa ukiacha kiwango cha mchezaji ilikuwa ni kimo na kwa kipindi hicho Nketiah hakuwa na umbo zuri kuitumikia Chelsea.

Baadaye ndipo mzee Arsene Wenger alilifumbia macho umbo la Nketiah na akamuweka kwenye academy ya Arsenal kutokana na uwezo aliokuwa nao katika kupasia nyavu.

Arsene Wenger ameshangazwa pia na kitendo cha Chelsea kumuacha Nketiah akisema kwamba kwa ubora alionao dogo huyo haoni sababu ya Chelsea kumruhusu aondoke.

Kuelekea Dar derby: “Simba walifanya kosa kumwacha Ajib aondoke”-Rage

$
0
0

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema, yalifanyika makosa kwa uongozi wa klabu yake kuwaachia Ibrahim Ajib pamoja na Amis Tambwe ambao wote walisajiliwa Yanga kwa nyakati tofauti.

“Lazima nikiri kwamba viongozi wangu walifanya makosa kumwachia Ajib, ni kijana mzuri lazima niseme ukweli, inawezekana alikuwa na matatizo yake lakini wachezaji hawakosi kuwa na matatizo, kinachotakiwa siku zote ukiwa kiongozi ni kuwa mvumilivu na kujaribu kuwa na lugha nzuri ya kumvuti mchezaji”-Rage.

“Mchezaji mdogo kama Ajib kumuachia au Tambwe ilikuwa ni makosa makubwa kwenye klabu ya Simba. Kwa kuwa ameondoka na kwenda kwa watu, siku zote watu ambao wanatoka Simba kwenda Yanga basi tena wanapoteza ile thamani yao  hata uwe mzuri kiasi gani.”

Ajib amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu ya Yanga tangu asajiliwe kabla ya kuanza kwa msimu huu na tayari ameshafunga magoli matano katika mechi saba za VPL. Tambwe pia ameendea kufanya vyema tangu ajiunge na Yanga baada ya kutemwa Msimbazi na amekuwa akiwafunga kwenye mchezo wa watani wa jadi.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>