Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Takwimu 5 zinazoonesha United walistahili kipigo

$
0
0

Manchester United ni kama hawaamini kilichotokea hii leo baada ya kupigwa na timu iliyoonekana kibonde ya Huddersfield, lakini kwa takwimu ni wazi kwamba United walistahili kipigo.

Ball Possesion 78 ila mashuti matatu langoni, ina maana Huddersfield walikuwa na ball posession 22 lakini cha ajabu ni kwamba Huddersfield walilingana idadi ya mashuti yaliyolenga bao huku Hudders wakipata mabao mawili na Manchester United wakipata moja.

Wachezaji waliopambana sana wote wanatokea Huddersfield, takwimu zinaonesha Aaron Mooy alitembea kilomita 13 uwanjani hapo huku anayemfuatia ni Jonathan Hogg aliyetembea kilomita 12.6 na kisha ndio anatokea wa Manchester United Nemanja Matic (12.2km)

Majanga ya Victor Lindelof, hakuanza vizuri msimu huu na leo Mourinho alipoamua kumpa nafasi hakucheza vyema na ndio maana akaruhusu United kufungwa mabao mawili idadi sawa na mabao waliyofungwa katika michezo 8 ya mwanzo ya ligi.

Jose Mourinho ni mbovu wa comeback, tofauti na Sir Alex Ferguson rekodi zinaonesha Jose Mourinho akishatanguliwa kwa idadi ya mabao huwa hashindi, na rekodi inaonesha katika mara 19 timu pinzani ilitangulia kwa bao mbili dhidi ya Mourinho, alipata suluhu moja akapigwa 18.

Romelu Lukaku aanza kudoda, baada ya kukabwa vilivyo dhidi ya Liverpool mshambuliaji Romelu Lukaku hajafunga tena, hii inamaanisha sasa Lukaku amecheza michezo mitatu mfululizo bila kuziona kamba za wapinzani.


Mgoli yote na highlights Simba vs Njombe Mji

$
0
0

Jumamosi October 21, 2017 Simba imeshinda mechi yale ya mzunguko wa saba wa ligi kuu Tanzania bara kwa magoli 4-0 dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru .

Magoli ya Simba yamefungwa na Emanuel Okwi aliyefunga goli la kwanza dakika ya 28 Mzamiru Yassin akafunga goli la pili dakika ya 50 na la tatu daki ya 53 huku goli la nne likifungwa na Laudit Mavugo dakika ya 59.

Unaweza kushuhudia magoli yote kwa kubofya video hapo chini. Video hii ni kwa hisani ya Azam TV.

Mlipili amecheza mechi ya kwanza VPL tangu asajiliwe Simba, hii ni comment ya Omog 

$
0
0

October 21, 2017 ni siku ya kukumbukwa kwa beki wa kati wa Simba Yusuph Mlipili ambaye amecheza mechi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara akiwa amevaa uzi wa Msimbazi wakati Simba ilipocheza dhidi ya Njombe Mji na kuisadia timu yake kushinda 4-0.

Mlipili alianza kwenye kikosi cha kwanza kwenye beki ya kati sambamba na mganda Juuko Murshid, wawili hao walikuwa wakicheza pamoja kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya ligi na kufanikiwa kucheza dakika 90 bila kuruhusu goli chini ya uongozi wa golikipa wao Aishi Manula.

Baada ya mechi kumalizika, kocha wa Simba amesikika akimtaja Mlipili kuwa ni beki bora wa baada wa Simba

“Mlipili ni miongoni mwa mabeki wa kati bora wa baadae wa timu hii, ni mchezaji mzuri alifanya vizuri kwenye mechi yetu ya kirafiki tuliyocheza Dodoma”-Joseph Omog.

Omog amesema kikosi chake kilikuwa na mabadiliko makubwa kwenye mchezo wa leo kwa sababu ana wachezaji wengi lakini baadhi ya wachezaji wake wanauguza majeraha.

Tangu kuanza kwa msimu huu Method Mwanjale, Salim Mbonde na Juuko Murshid wamekuwa wakibadilishana katika sehemu ya ulkinzi wa kati katika mechi zilizo pita kabla ya mchezo wa leo.

Mlipili alisajiliwa Simba akitokea Toto Africans timu iliyoshuka daraja msimu uliopita.

Manara amefunga mdomo kisa Yanga

$
0
0

Kuelekea pambano la watani wa jadi Yanga vs Simba October 28, 2017, afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wazi kwamba usitarajie kumsikia akizungumza chochote kabla ya mechi hiyo kuchezwa.

Manara amesema huo ni utaratibu maalum kwa sababu maalum kwa hiyo atasikia baada ya mechi yao dhidi ya Yanga, endapo utamsikia Manara kabla ya mechi hiyo basi itakuwa ni kwa ajili ya jambo la dhalura ambalo linahitaji kutolewa ufafanuzi wa haraka.

“Baada ya press yangu nanyi hapa kwa mechi hii, msitegemee jambo lolote kutoka kwenye kinywa changu wala maandishi yangu mpaka tutakapomaliza mechi. Nimeuweka utaratibu huo maalum kwa sababu maalum kwa hiyo naomba wale wanaolalamika sipokei simu wala wasijihangaishe, nawaarifu mapema sitaongea lolote labda itokee dhalura ambayo inahitaji ufafanuzi lakini kuelekea mchezo huo sitaongea.”

Manara pia amesema kikosi cha Simba kitaondoka Jumatatu October 23, 2017 kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Yanga.

“Timu itaondoka Jumatatu asubuhi kwenda Zanzibar itakaa huko hadi Jumamosi asubuhi itaporejea kisha badae itaelekea uwanjani kwa ajili ya mechi.”

Manara ameomba kama inawezekana mechi hiyo (Yanga vs Simba) ichezwe uwanja wa taifa kama uwanja huo utakuwa tayari baada ya ukarabati kuonekana unaridhisha.

Mambo niliyoyaona kwenye game ya Chelsea vs Watford Stamford Bridge

$
0
0

Nimehatika kushuhudia mchezo wa Chelsea dhidi ya Watford mechi ambayo imemalizika kwa The Blues kushinda 4-2,watu wengi wameonesha wasiwasi kwamba huenda timu hiyo ikashindwa kufanya vizuri kufuatia kukosekana kwa kiungo wao mahiri N’Golo Kante ambaye anauguza majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Mashabiki wa Chelsea hapa London hawamzungumzii sana kukosekana kwa kiungo wao Kante licha ya kwamba ni moja kati ya wachezaji mahiri na muhimu kwenye kikosi chao lakini kutokuwepo kwake inafahamika moja kwa moja kwamba kuna pengo.

Changamoto kwa Antonio Conte ni kuhakikisha timu inapata matokeo bila kujali kuna mchezaji fulani yupo au fulani hayupo, hapo ndipo inaonekana kazi na umuhimu wa kocha.

Katika siku za karibuni Chelsea imeonekana ikihangaika sana kuzua timu pinzani kwenda kwenye eneo lao la hatari kwa hiyo ukifuatilia mechi kadhaa ambazo wamecheza kwenye uwanja wao wa nyumbani ni mechi nyingi wameshindwa kumaliza bila kuruhusu nyavu zao kutikishwa. Bora wangekuwa wanaruhusu nyavu zao zitikishwe lakini mwisho wa siku wao wawe wamefunga magoli mengi kwa maana ya kwamba wameshinda mechi kama ilivyo kwa Liverpool.

Mechi zilizopita kwenye uwanja wao wa nyumbani hazikuwa zenye matokeo mazuri, mechi dhidi ya Tottenham walishinda 2-1, wakafungwa na Burnley 3-2, kilichokuwa kinazua mijadala ni kwa nini Chelsea imeshindwa kuwa na mwendelezo hasa kwenye eneo la kiungo.

Kama ilivyokuwa kwenye mechi kadhaa zilizopita, Conte amewatumia Bakayoko na Fabregas kwenye eneo la kiungo na kutengeneza mwonekano mpya wa safu ya ulinzi. Wengi tumezoea kumuona Conte akitumia mfumo wa mabeki wa tatu halafu anajaza watu wengi kwenye eneo la kiungo huku akitegemea zaidi ma-wing back wa kushoto na kulia (Victor Moses akitokea kulia) na (Marcos Alonso akitokea kushoto.)

Namna alivyotumia muda mwingi kuiandaa timu kwa kuwategemea wachezaji hao hata anapoamua kufanya rotation ya kikosi chake bado wachezaji hao wamekuwa wakicheza mara kwa mara kwa sababu ni muhimili kutokana na aina yao ya uchezaji (wanakimbia sana uwanjani) kufanya coverage kubwa ukilinganisha na mtu kama Fabregas ambaye hakimbii sana lakini anafaida zake kwa sababu mipira yake mingi haipotei.

Mbio za Moses kwenda na kurudi ni tofauti na Cesar Azpilicueta ambaye yeye kwa asili ni beki wa pembeni lakini mfumo unamfanya awe wing-back, anavyocheza Moses ni tofauti na anavyocheza Azpilicueta. Kwenye mfumo unaomfanya Moses acheze, Azpilicueta anacheza ndani kwa hiyo kutokuwepo kwa hawa mabwana (Moses na Kante) kunabadili tempo na rhythm ya timu.

Kwa mfano leo nimemuona David Luis mwanzoni alikuwa kama mtu wa mwisho katikati huku Cahill akiwa ame-focus sana kushoto wakati Antonio Rüdiger yeye alikuwa makini zaidi na upande wa kulia halafu ma-wing back walikuwa Azpiticueta na Alonso, kwenye eneo la kiungo Fabregas alikuwa mbele kati ya wale watano wa katikati.

Tofauti ya Fabregas na Kante unakuja kuiona hapa, Fabregas anapoza mchezo kwa sababu yeye sio mtu wa mbio wala kupiga mipira za harakaharaka, anachokifanya ni kupokea mipira kisha kuanzisha mashambulizi kwa hiyo kulikuwa na kuchelewa kutoka mbele ya mabeki watatu kwenda mbele kwenye eneo la kushambulia hiyo inawafanya wapinzani kuziba mianya ambayo kwa aina ya uchezaji wa Chelsea hupiga mipira yao kwenye mianya hiyo  kwa hiyo ikishazibwa wanajikuta wanapiga pass karibukaribu kitu ambacho wapinzani wao wakipata mpira wanawakimbiza ndio maana utaona walitangulia kufungwa.

Baada ya kuona wako nyuma 2-1 kipindi cha pili Conte akafanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa Alonso na kumuingiza Willian kisha kumbadilisha Azpilicueta kwenda kushoto na kucheza kama wing-back wa kushoto kisha kumrudisha kulia Pedro kuja kucheza kama wing back na kumwachia nafasi Hazard kutlia halafu Bakayoko akarudi chini Fabregas akasogea mbele.

Wakati huo Conte akamuingiza Michy Batshuayi baada ya Morata kuonekana kama alikuwa anakimbiakimbia kwa sababu hakuwa anapata mipira mingi mizuri. Na kama ulifuatilia, mipira mingi mirefu kwa namna Chelsea walivyokuwa wanacheza Watford walikuwa wanakaba mshambuliaji mmoja kwa mabeki wawili, kwa hiyo ukipiga mpira mrefu wale mabeki wawili wanamvuruga mshambuliaji na kumfanya akose nafasi kuukimbilia mpira uliopigwa mbele yake.

Kuingia kwa Batshuayi kuliisaidia timu kutokana na nguvu zake, composure, ubunifu ukaongezeka kwa sababu mipira mbingi ikawa inaenda kwa Hazard na Pedro ambao walikuwa upande mmoja kushoto unamkuta Azpilicueta na Willian kwa hiyo timu ikabadilika tofauti na ilivyokuwa imeanza mwisho wa siku wakatengeneza nafasi za kutosha na kufunga magoli yaliyowafanya washinde mechi.

Kipigo chaanza kuleta mtafaruku OT, Mourinho amchana Herrera

$
0
0

Kwa mara ya kwanza hapo jana Manchester United walikubali kuchezea kichapo katika msimu huu, United wakiwa ugenini walikubali kipigo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Huddersfield.

Baada ya mchezo kuisha kiungo wa Manchester United Ander Herrera alidai kwamba wapinzani wao walijituma zaidi haswa katika dakika 30 za mwanzo kuliko vile ambavyo Manchester United walijituma.

Baada ya kauli hiyo ya Herrera kocha wa Manchester United Jose Mourinho naye alisema yake na kuonesha wazi kwamba hajapendezwa na majibu ya Herrera kuhusu dakika 30 za mwanzo za mchezo huo.

Mourinho anasema inasikitisha sana kwa mchezaji kama Hererra kusema kwamba walizidiwa katika kujituma na ni mbaya sana, Mourinho anasema bora kwake kama kocha lakini kauli ya namna hiyo haiwafanyi mashabiki kujisikia vizuri.

Lakini Mourinho amekiri kwamba Hudders walikuwa vizuri sana na wameshinda kwa kuwa walikuwa vizuri zaidi yao huku akishangazwa na namna walivyokuwa akikiri kwamba hakutegemea wangekuja hivyo.

Kipigo cha Manchester United kimeongeza pengo la alama kati yao na Manchester City ambapo kwa sasa Manchester City wanaongoza ligi wakiwa na tofauti ya alama 5 na anayewafuatia.

Arsenal wampa mzee Wenger zawadi kubwa ya birthday kwa mara ya 3

$
0
0

Happy birthaday Arsene Wenger, leo ni siku ya kuzaliwa kwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger na hii leo alikuwa akitimiza miaka 68, Wenger ametimiza miaka 68, rekodi zinaonesha Wenger ameahinda katika siku yake ya kuzaliwa mara tatu 2006,2014 na hii leo.

Alianza Wayne Rooney kufungua ukurasa wa mabao huku likiwa bao lake la 12 dhidi ya Arsenal katika Epl na la 15 katika michuano yote, idadi inayomfanya kuwa mchezaji ambaye amewafunga zaidi Arsenal katika Epl.

Lakini Nacho Monreal aliwasawazishia Arsenal kabla ya Mesut Ozil kuwafungia bao la pili kwa kichwa na kuwafanya Arsenal kuwa timu yenye mabao mengi kwa kichwa tangu msimu uliopita kuanza, wana mabao 23.

Alexis Sanchez aliwafungia Arsenal bao la tatu bao ambalo linamfanya kuwa mchezaji kutokea Ufaransa mwenye mabao mengi zaidi mwaka 2017 ambapo hadi sasa anakuwa amefunga mabao 27.

Aaron Ramsey alifunga bao la nne na Alexis Sanchez akafunga bao la tano na kuwafanya Arsenal kuwa timu ya kwanza kufunga mabao mengi zaidi dhidi ya timu moja baada ya leo kufikisha idadi ya mabao 100 dhidi ya Everton.

Ajib kaipeleka Yanga kwa Simba

$
0
0

Ibrahim Ajib ameendelea kuwasha moto akiwa na Yanga baada ya leo Jumapili October 22, 2017 kuifungia mabao mawili kwenye ushindi wa  4-0 dhidi ya Stand United na kuifanya Yanga ifikishe pointi 15 sawa na Simba na Mtibwa Sugar.

Simba na Mtibwa zilifikisha pointi 15 baafa ya kushinda michezo yao ya jana lakini ushindi wa  Yanga leo unafanya timu tatu kufungana pointi lakini tofauti ya magoli ndio unazitofautisha katika msimamo wa ligi.

Ajib ndio anaongoza kwa ufungaji kwenye kikosi cha Yanga akiwa na magoli matano (5) aliyoyafunga kwenye mechi saba alizocheza.

Magoli ya Ibrahim Ajib

  • Njombe Mji 0-1 Yanga (Ajib)
  • Yanga 1-0 Ndanda (Ajib)
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga (Ajib-assist goli la kwanza likafungwa na Chirwa, yeye akafunga la pili).
  • Stand United 0-4 Yanga (Ajibu amefunga magoli mawili, Pius Buswita na Obrey Chirwa wamefunga moja kila mmoja)

Anamfukuza Okwi kimyakimya 

Ajibu yupo nyuma ya Okwi kwenye orodha ya wafungaji VPL, Okwi amefunga magoli nane (8), Ajib magoli matano (5) na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye magoli manne (4).

Yanga imeshinda mechi yake ya nne msimu huu sawa ikiwa imetoka sare mara tatu huku ikiwa haijapoteza mchezo sawa na matokeo ya Simba pamoja na Mtibwa Sugar huku timu zote zikiwa zimecheza mechi saba hadi sasa

  • Yanga 1-1 Lipuli
  • Njombe Mji 0-1 Yanga
  • Majimaji 1-1Yanga
  • Yanga  1-0 Ndanda
  • Yanga Mtibwa 0-0 Mtibwa Sugar
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga
  • Stand United 0-4 Yanga

Ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga 

Yanga ilikuwa haijashinda mechi kwa zaidi ya magoli mawili, huu ni ushindi wao mkubwa Tangu kuanza kwa VPL msimu huu. Walifunga goli moja mfululizo kwenye mechi zao nne za kwanza kabla ya kupata ushindi wa magoli 2-1 walipocheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliopita.


Sami Khedira na Memphis Depay wapiga hat trick

$
0
0

Udinesse walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Stadio Friuli kuikaribisha Juventus na wakatangulia kwa goli moja dakika ya 8 kabla ya Juventus kuwashushia mvua ya mabao wenyeji hao.

Kiungo Sami Khedira alipiga hat trick huku Daniele Rugani, Miralem Pjanic na bao la kujifunga la Samir liliwafanya Juventus kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabo 6 kwa 2 dhidi ya Udinesse.

Wakati Juventus wakishinda bao 6 kwa 2, wahenga wa ligi hiyo klabu ya Ac Millan walikuwa uwanjani kwao San Siro na kulazimishwa sare ya bila kufungana na sasa wanashika nafasi ya 11 katika msimamo.

Ligue one nako Lyon walikuwa ugenini dhidi ya Troyes na kuibuka kidedea kwa mabao 5 kwa nunge huku winga wa zamani wa Manchester United akipiga hat trick huku Bertand Troure na Mariano Diaz wakifunga mengine.
Nchini Hispania Kevin Gameiro aliiokoa Athletico Madrid baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Celta Vigo, Villareal wakiwa nyumbani waliidondoshea mvua ya mabao Las Palmas baada ya kuichapa bao 4 kwa nunge.

Nchini Uingereza Tottenham Hotspur wameifikia Manchester United kwa alama ya pointi baada ya Harry Kane(2), Min Son, Delle Ali kuiua Liverpool kwa mabao 4 kwa 2 na kufikisha alama 20.

Al Ahly waipa kipigo cha mbwa mwizi Etoile Du Sahel na kwenda fainali

$
0
0

Baada ya kushinda bao mbili kwa moja nchini Tunisia siku chache zilizopita, hii leo klabu ya Etoile Du Sahel hawakuamini kilichowatokea katika dimba la Al Ahly baada ya kupeea kipigo cha mbwa mwizi.

Al Ahly waliwaadhibu bila huruma Etoile Du Sahel kwa kuwapiga bao 6 kwa 1 na kipigo kilianza dakika ya kwanza tu kwa bao la Ali Maaloul kabla ya Walid Azorou kuweka kambani bao mbili kabla ya half time.

Kipindi cha pili Walid Azorou alifunga bao lake la tatu kabla ya Hamid Nagguez kujifunga na kisha Rami Rabia kufunga bao la sita huku Etoile Du Sahel wakipata la kufutia machozi kupitia kwa Rami Badoui.

Kwa matokeo ya leo Al Ahly watakabiliana na Wydad Casablanca katika fainali ya michuano hiyo ya mabingwa wa Afrika, Wydad Casablanca walifudhu kwenda fainali baada ha hapo jana kuwafunga Usm Alger mabao 3 kwa 1.

“Tunacheza katika muonekano wa kisu, Bodi ya ligi iwalinde wachezaji wasiolipwa mishahara VPL”-Amri Said

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

LIPULI FC ilifanikiwa kupata ushindi wa pili msimu huu katika ligi kuu ya Tanzania baada ya kuifunga 1-0 Majimaji FC siku ya Jumamosi iliyopita katika uwanja wa nyumbani (Samora Stadium.) Ushindi huo umeipeleka timu hiyo hadi nafasi 8 wakiwa wamefunga kila kitu na Ndanda FC.

Timu hizo mbili zimekusanya pointi 9 kila moja huku kila timu ikiwa imefunga magoli manne na kufungwa manne. Kama ilivyo kwa Ndanda FC, timu ya Lipuli nayo imepoteza game mbili, sare tatu na kushinda michezo miwili katika michezo 7 iliyopita.

Jumapili hii nilifanya mahojiano marefu na kocha mkuu wa kikosi hicho, Amri Said ‘Stam’ ambaye ni mshindi wa mataji ya ligi ya kuu Tanzania mwaka 1998 akiwa na Majimaji FC, VPL 2001, 2003 na 2004 akiwa Simba SC.

Amri ameichukua timu hiyo baada ya kurejea ligi kuu na amezungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea kikosini mwake na katika ligi kiujumla. Hii ni sehemu ya mahojiano hayo

www.shaffihdauda.co.tz: Habari yako mwalimu?

Amri Said: Namshukuru Mungu niko salama. Sijui hali yako?

www.shaffihdauda.co.tz: Nashukuru pia mambo yanakwenda. Nafuatilia sana timu yako, napendezwa na mwendo wenu katika michezo hii saba iliyopita.

Amri Said: Asante sana.

www.shaffihdauda.co.tz: Unaizungumziaje ligi baada ya game saba za mwanzo?

Amri Said: Ligi ni ngumu na bado tuna changamoto kadhaa, unajua timu yetu ilichelewa kufanya usajili jambo ambalo lilipelekea tuchelewe pia katika maandalizi ya msimu. Kwa ufupi hatukuwa na maandalizi ya kutosha kabla ya ligi kuanza.

Unajua hivi sasa ukitazama katika ligi yetu kuna makocha kadhaa raia wa Burundi. Wingi wao unatokana na kufanya vizuri na kutimiza malengo yao katika timu wanazozifundisha. Sasa ni kupambana nao ili kudhihirisha uwezo wetu sisi kama makocha wazawa. Tunapaswa kutimiza malengo yetu na klabu.

www.shaffihdauda.co.tz: Ni kupambana nao tu Mwalimu.

Amri Said: Ndio tunachofanya hapa Lipuli FC nikiwa na wenzangu wakiongozwa na Selemani Matola. Kama unavyojua niliichukua timu hii wakati ambao muda umeshakwenda na ligi ilikuwa karibu kuanza, hivyo muda wetu mwingi kama benchi la ufundi tumekuwa tukiutumia kuimarisha kikosi chetu.

www.shaffihdauda.co.tz: Unafanya nini ili kwenda sawa na hali hiyo maana tayari mko katika mapambano

Amri Said: Nimekaa na wenzangu na kuzungumzia hali hiyo. Tunajipanga kikamilifu kukabiliana na hali hiyo ili tufanye vizuri.

www.shaffihdauda.co.tz: Nimetazama ligi hadi sasa. Timu nyingi zimekuwa na changamoto ya ufungaji hata timu yako pia. Unachukuliaje hali hiyo?

Amri Said: Nafikiri hilo ni tatizo kubwa hata upande wetu, bado timu yetu haina mtu maalum wa kufunga magoli. Tegemeo letu kubwa ilikuwa ni yule kijana Madebe lakini bahati mbaya bado hajaruhisiwa kutoka ofisini na waajiri wake.

www.shaffihdauda.co.tz: Machaku alifunga goli 13 katika game 14 kwanini? Inakuwaje anakosa nafasi sasa?

Amri Said: Machaku si mchezaji mbaya kiufungaji ila tumemuongezea majukumu, sasa hivi tumekuwa tukimtumia kama kiungo mshambuliaji.

www.shaffihdauda.co.tz: Anayaweza majukumu hayo? Kama anaweza kufunga na timu haifungi kwanini usimrudishe nafasi ya kati?

Amri Said: Tunafanya hivyo ili timu isifungwe magoli mara nyingi na ukitazama hadi sasa tumefanikiwa kwa maana licha ya kuwa tunafanya maandalizi tukiwa katika ligi ila hatujaruhusu magoli mengi.

www.shaffihdauda.co.tz: Game ijayo mnacheza na nani? Wapi

Amri Said: Mechi inayofuata tunacheza na Mbao FC katika uwanja wetu wa nyumbani.

www.shaffihdauda.co.tz: Kweli ligi inaanza kuwa ngumu zaidi. Mbao FC wametoka kucheza mechi 6 mfululizo pasipo ushindi kati ya hizo nne mfululizo wametoa sare nyumbani, unadhani itakuwa mechi ya aina gani upande wenu?

Amri Said: Ni kweli ligi ngumu na tunakwenda kucheza mchezo mwingine mgumu wikend ijayo. Kwetu sisi kila mchezo ni mgumu hivyo tumejiandaa kukabiliana na hali hiyo kadri itakavyowezekana.

Tunafahamu Mbao ni timu nzuri, lakini tunajipanga kuhakikisha tunachukua pointi zote tatu katika uwanja wa nyumbani.

www.shaffihdauda.co.tz: Uwanja wa nyumbani ni nyenzo muhimu katika ligi. Unadhani timu yako inapata sapoti ya kutosha katika uwanja wa Samora?

Amri Said: Hakika, tena napenda kuwashukuru watu wa hapa (Iringa). Kumalizika kwa tatizo lililokuwa nje ya uwanja baada ya uongozi wa juu wa Mkoa, wilaya na Wazee wa Iringa, sasa Lipuli FC ni timu moja na hata kiwango cha juu cha mashabiki waliofurika katika mchezo wetu wa Jumamosi walikuja pale kuisapoti timu yao. Kwa kweli nawapongeza sana wakuu wa wilaya zote na mkuu wa Mkoa, wazee wa Iringa na mashabiki kiujumla.

www.shaffihdauda.co.tz: Baada ya game 7 za mwanzo msimu huu, unazungumziaje uchezeshaji wa waamuzi hasa kwa game mlizocheza ugenini?

Amri Said: Siwezi kuwalaumu waamuzi kwa sababu wengine huchezesha mechi pasipo kuwa na uzoefu hivyo matokeo yanapokuwa sare katika mchezo mwamuzi wa aina hii hujiona amechezesha vizuri. Wengine hujisifia kuwa wamemudu pambano lakini wakati mwingine ukweli mpira huchezwa katikati ya uwanja zaidi na kupelekea kukosekana kwa mashambulizi mengi golini.

Ukitazama hata katika michezo mingi iliyomalizika kwa sare utaona mpira ulichezwa zaidi katikati ya uwanja. Mechi isipokuwa na mashambulizi mengi si rahisi kupima uwezo halisi wa mwamuzi.

www.shaffihdauda.co.tz: Kuna chochote hupendezwi nacho katika ligi?

Amri Said: Mabadiliko ya waamuzi pasipo taarifa na mwamuzi mmoja kurudia rudia kuchezesha timu moja zaidi ya mara mbili wakati ligi ipo mzunguko wa saba tu. Kingine ni mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba.

www.shaffihdauda.co.tz: Mmeshakutana na mabadiliko ya ghafla ya waamuzi? Ilikuwa wapi?

Amri Said: Ndiyo, kama kocha niliona hili wakati timu yangu ilipocheza na Majimaji jana (Jumamosi iliyopita) lakini sijalalamika.

www.shaffihdauda.co.tz: Umevutiwa na lolote hadi sasa katika ligi?

Amri Said: Ndiyo, kuna mambo yamenivutia hasa kuona baadhi ya viwanja vikiboreshwa kwa kiwango kizuri katika eneo la kuchezea. Pitch ni sehemu muhimu sana kwa wachezaji, kwani ikiwa nzuri humfanya mchezaji kuwa tayari kucheza na kupokea maagizo ya walimu wake.

www.shaffihdauda.co.tz: Timu yako imeonekana kucheza vizuri katika kujilinda. Kuwa beki wakati wa uchezaji wako ndio kunapelekea hali hiyo?

Amri Said: Kwa kiasi fulani inanisaidia kwa sababu mara nyingi nimefanya mazoezi jinsi ya kulinda wakati nikiwa mchezaji. Tunalinda kama kilivyokaa kisu-mbele mtu mmoja, golikipa na wachezaji wengine wanajaa katikati ya uwanja.

www.shaffihdauda.co.tz: Neno lako kwa bodi ya ligi

Amri Said: Wajipange kwa ajili ya kuongeza wadhamini, na waweke mikataba na wanasheria watakaosimamia haki za wachezaji wanaocheza ligi na haki zao. Ni aibu kuona mchezaji wa ligi kuu ya Tanzania bara akicheza na kumaliza ligi nzima pasipo kulipwa mshahara huku timu ikisafiri bila posho.

www.shaffihdauda.co.tz: Asante sana mwalimu na nakutakia kila la heri katika kazi yako.

Amri Said: Asante sana, karibu tena wakati mweingine.

Mambo matatu yanayoweza kuwapa Mtibwa Sugar ubingwa msimu huu

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

ILI kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, mabingwa mara mbili wa zamani, timu ya Mtibwa Sugar FC wanapaswa kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi na kuendelea kushinda michezo yao inayofanyika katika uwanja wa nyumbani (Manungu Complex, Turiani.)

Mabingwa hao mara mbili mfululizo wa zamani (1999 na 2000) wameanza msimu huu vizuri wakiwa wameshinda michezo minne na kutoa sare mara tatu katika michezo saba ya mwanzo. Ikiwa nyuma kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya viongozi Simba SC kikosi hicho cha kocha Zubeiry Katwila kimeonyesha nia ya kutwaa taji msimu huu tangu walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho miaka takribani 16 iliyopita.

Licha ya ‘kubezwa’ na kuonekana ni ‘tabia’ yao-kuanza vizuri msimu na kumaliza katika nafasi za chini mwishoni mwa msimu, upande wangu naamini Mtibwa Sugar ni timu yenye uwezo wa kushindana kwa msimu mzima na kutwaa ubingwa kama watajipanga katika hilo.

Kushinda pointi 35+ Manungu Complex

Kabla ya kuanza kwa msimu wa 2016/17 nilipata kuandika makala kuhusu uzembe ambao umekuwa ukifanywa na timu hiyo ya Turiani, Morogoro kiasi cha kushindwa kuonyesha upinzani hadi mwishoni mwa msimu.

Kushindwa kizembe kupata matokeo katika uwanja wa Manungu Complex dhidi ya timu ambazo wangeweza kuzifunga kuliiangusha sana timu hiyo msimu wa 2012/13 licha ya kufanikiwa kukusanya alama kumi katika michezo minne dhidi ya vigogo Yanga SC na Simba.

Unapomaliza msimu pasipo kupoteza mechi dhidi ya Yanga na Simba huku ukizishinda timu hizo mara mbili na kutoa sare mbili inamaanisha ulikuwa na kikosi kikali. Katika misimu ya karibuni Mtibwa Sugar imekuwa ikiangusha sana pointi katika uwanja wa Manungu jambo ambalo limekuwa likiwaporomosha na kwa misimu saba sasa timu hiyo imekuwa nje ya nafasi tatu za juu huku mara moja tu wakifanikiwa kumaliza msimu ndani ya nafasi nne za juu.

Kushinda michezo mitatu mfululizo katika uwanja wa Manungu Complex mbele ya timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC na Mbao FC) kumewafanya mabingwa hao mara mbili wa kihistoria kukusanya alama zote 9 katika uwanja wa nyumbani.

Na wakiwa wametoka kupata sare tatu mfululizo katika michezo mikubwa ya ugenini (Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa, Yanga 0-0 Mtibwa, Simba 1-1 Mtibwa) ni wazi kikosi cha Katwila kimeonyesha mwanzo mzuri japo wengi wanachukulia ‘kuwa ni tabia yao.’ Tabia ya kuanza msimu vizuri na kumaliza vibaya.

Mchezo wao wa nne katika uwanja wa Manungu Jumamosi hii dhidi ya mabingwa mara moja wa zamani wa Tanzania, timu ya Tanzania Prisons umeonyesha picha halisi ya kile kinachotakiwa na timu hiyo kutoka mkoani Morogoro katika ligi ya msimu huu baada ya kupata ushindi mwingine kwenye uwanja wa nyumbani.

Katika michezo 15 ya nyumbani, Mtibwa haiwezi kupata alama zote 45 lakini wanaweza kupambana na kupata walau pointi 35 ambazo zinaweza kuwasogeza karibu na malengo ya ubingwa.

Ni lazima wapambane na kujitahidi kadri wawezavyo kushinda michezo kumi pale Manungu, sare tatu na kupoteza michezo miwili kunaweza kuwafanya kuwa juu katika msimamo siku ya mwisho ya msimu.

Pointi 20+ katika game 15 za ugenini

Si rahisi kupata alama 25 katika michezo 15 ya ugenini lakini Mtibwa Sugar ni lazima wajaribu kutafuta walau pointi 20 nje ya Manungu Complex kama kweli wanataka kurudisha ubingwa huo.

Kushinda walau michezo mitano ya ugenini kutawapa alama 15 na sare katika michezo mitano kutawapa ‘makumi mawili’ ya pointi muhimu katika game za ugenini. Wanaweza kupambana vizuri na kupata walau alama tano katika michezo mitatu ya ugenini vs Stand, Mwadui FC na Mbao FC ambazo walifanikiwa kuzifunga zote katika uwanja wa Manungu.

Kulazimisha matokeo dhidi ya timu kama Ndanda FC, Majimaji FC, Lipuli FC katika viwanja vyao vya nyumbani kunaweza kuwaongezea pointi muhimu timu hiyo yenye mseto mzuri wa wachezaji kiumri na kiuchezaji.

Naona wanaweza kupata alama zisizopungua 20 nje ya uwanja wao wa Manungu msimu huu huku tayari wakiwa wamechukua alama moja moja kwa kila mchezo kati ya game tatu za ugenini walizocheza dhidi ya Shooting na wababe Yanga na Simba. Bado pointi 17 katika michezo 12 iliyosalia ugenini kwa upande wao.

Kikosi kizuri wanacho

Golikipa mshindi mara mbili wa tuzo binafsi ya kipa bora wa VPL, Shaaban Kado, walinzi wazoefu kama Dickson Daud, Salum Kanoni, Issa Rashid, viungo wakongwe wenye ubora wakiongozwa na nahodha, Shaaban Nditti, Henry Joseph.

Hussein Javu katika safu ya mashambulizi wanaweza kuungana na vijana kama Kassian Ponela, Haruna Chanongo, Mohamed Issa ‘Banka’, Stamil Mbonde na wengineo kutengeneza timu kali ambayo inaweza kushinda ubingwa wakiweka malengo na kupambana ndani ya uwanja.  Huku uwanja wa Manungu wakiutumia kwa umakini na kuugeuza ‘karata dume’ yao ya kuwapa taji la tatu la VPL.

Uhuru Selemani kaiongoza klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi kuu Msumbji

$
0
0

Uniao Desportiva do Songo

Mtanzania Uhuru Selemani Mwambungu amefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Msumbiji (Mocambola) 2017/2018 akiwa na klabu ya União Desportiva do Songo ambayo imemaliza ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 30 katika ligi yenye timu 16.

UD Songo ilitangaza ubingwa ikiwa bado imesaliwa na mechi mbili mkonano baada ya kuwafunga wapinzani wao wa karibu Costa do Sol ambao wamemaliza katika ya pili wakiwa na pointi 56.

Uhuru Selemani amesema ligi hiyo ni ngumu pengine kuliko ligi zote ambazo amewahi kucheza hivyo kushinda ubingwa haikuwa kazi nyepesi.

“Timu yangu imechukua ubingwa wa ligi lakini tunaelekea kucheza fainali ya FA Cup wikiki ijayo tulitangaza ubingwa tukiwa na mechi mbili mkononi baada ya kuifunga 2-1 Costa do Sol ya mjini Maputo na wiki hii tumemaliza ligi kwa mechi zote ambazo zilikuwa zimebakia na tumesha kabidhiwa kombe, medali na zawadi nyingine.”

“Ligi haikuwa rahisi kama wengi wanavyodhani na kumzungumza kwamba ligi ya Msumbiji ni rahiri. Mazingira ya viwanja, safari za kwenda kucheza mechi za ugenini pamoja na ushindani ndani ya uwanja ni mkubwa sana kuliko ligi zote nilizowahi kucheza kwa hiyo haikuwa kazi rahisi.”

“Tutapambana kuhakikisha tunashinda fainali ya FA Cup ili kuwa na makombe mawili mkononi, Mungu akijalia mwakani tunaelekea kwenye klabu bingwa Afrika kwa sababu kila kitu kinawezekana.”

Mabingwa hao wamemaliza ligi baada ya kushinda mechi 19, sare saba na kupoteza michezo minne katika ligi wakiwa wamefunga magoli 38 na kuruhusu kufungwa magoli 15.

Uhuru aliwahi kucheza ligi kuu Tanzania bara alipokuwa akiichezea Simba kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, vilevile amewahi kuchezea timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Unayopaswa kujua kueleka The Best Fifa 2017 usiku wa leo, nani kuchukua na nani kukosa?

$
0
0

Usiku wa leo katika jiji la London kunaenda kufanyika tukio kubwa sana katika soka, shirikisho la soka duniani linakwenda kutoa tuzo kwa makocha na wachezaji waliofanya vizuri mwaka 2017.

Pamoja na kuwepo kwa tuzo nyingi lakini macho ya wengi yatakuwa katika kinyann’anyiro cha The Best Fifa Male awards ambapo Lioneil Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar Dos Santos wanawania tuzo hiyo.

Kwa mafanikio waliyopata katika msimu uliopita wa ligi Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa kubeba tuzo hii kutokana na msaada aliowapa Real Madrid katika Champions League pamoja na michuano ya La Liga.

Tuzo hizi za Fifa zimekuja baada ya Fifa kuacha ushirikiano wao na jarida la Ballon D’Or na Ronaldo De Lima na Zinedine Zidane ndio wamechukua tuzo hii mara nyingi (3) na kama Cr7 atachukua tuzo hii atakuwa amewafikia.

Mshindi katika tuzo hizi anapatikana kwa kupigiwa kura ambapo kura zinapigwa na mashabiki, makocha,waandishi wa habari za michezo na macaptain ambapo kila kundi limepewa 25%.

Katika tuzo hizi kuna mwanadada raia wa Venezuela Deyna Castellanos mwenye miaka 18 ambaye yeye sio mwanasoka katika klabu kubwa lakini goli alilofunga akikitumikia chuo chake cha Florida lilimfanya dunia imtambue na kupewa nafasi.

Deyna anasema hakuwahi kuwaza kuweponkwenye tuzo hizo na hata siku majina yanatangazwa alikosa nguvu aliposikia jina lake likiwepo katika majina ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kike.

Deyna Castellanos yupo katika kinyang’anyiro chake akigombea tuzo hiyo pamoja na Lieke Martens na Carli Lloyd ambaye anapewa nafasi kubwa kunyakua tuzo hiyo.

Deyna Castellanos pia bao alilofunga chuoni kwao limeingia kwenye kinyang’anyiro cha bao bora huku akikumbana na upinzani kutoka kwa Olivier Guroud bao lake la nge na Ocarine Masuruke bao dhidi ya Orlando Pirates.

Antonio Conte kombe la kwanza katika msimu wake wa kwanza Epl  linamuweka katika kinyang’anyiro cha kocha bora akipambana na Massimiliano Allegri na Zinedine Zidane.

Idris Elba muigizaji wa filamu kubwa kama vile The Jungle Booka na Thor atakuwa ndio host wa tuzo hizi kubwa katika soka, nani atachukua na na nani atakosa? Tuonane baadae.

Manchester City yaviburuza vigogo vya Epl katika You Tube, United watia aibu

$
0
0

Inaonekana huu ni mwaka wa Manchester City ndani na nje ya uwanja, wakati klabu yao ikiwa inaongoza katika ligi kuu ya Epl sasa vinara hao wameweka rekodi nyingine nje ya uwanja katika mtandao wa You Tube.

Manchester City wanakuwa klabu ya kwanza kufikisha subscribers milioni 1 katika You Tube, hii ina maana chaneli ya You Tube ya Man City imefikisha watu milion 1.

Hii leo Man City walionesha live tukio hilo la kubwa klabu ya kwanza kufikisha idadi hiyo ya subsctibers huku kiungo wao Yaya Toure alikuwa live kuwashukurumashabiki wao kwa jambo hilo.

Lakini suala la kushangaza wakati Manchester City wakifikisha idadi hiyo ya subscribers, wapinzani wao wakubwa Manchester United wao hawana chaneli maalum katika mtandao wa You Tube.

Kiujumla Man City wana subscribers milioni moja na elfu nne huku Arsenal wakifuatia na subscribers laki saba na elfu kumi, nafasi ya tatu imekwenda kwa Liverpool wenye subscribers laki sita na tisini na nane.

Chelsea wanashika nafasi ya nne wakiwa na subscribers laki sita na tisini na tatu elfu huku Tottenham wakiwa na subscribers laki mbili na kumi na mbili elfu huku United wakiwa hawana chaneli You Tube.

Wakati Manchester City wakiviburuza vigogo wengine katika You Tube, msimamo wa Epl unaonesha Manchester City wanajinafasi kileleni mwa ligi wakiwa na alama 25 zikiwa ni alama 5 mbele ya United na Tottenham.


Cristiano Ronaldo amkalisha tena Messi

$
0
0

Kwa mara ya pili Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya The Best Fifa awards baada ya kupata 43% ya kura zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi aliyepata 19%.

Msimu uliopita Cristiano Ronaldo alifunga mabao 12 katika Champions League huku akifunga mara mbili katika mchezo wa fainali na kuwasaidia Real Madrid kutetea kombe la Champions League.

Manahodha waliompigia kura Cristiano Ronaldo ni pamoja na Luca Modric, Sergio Ramos, na Marcelo huku Neymar, Iniesta na Suarez wakimpigia kura Lioneil Messi.

Wakati Ronaldo akitwaa Best Male awards kocha wake Zinedine Zidane aliwabwaga Massimiliano Allegri na Antonio Conte na kutwaa tuzo ya kocha bora wa FIFA.

Gianluigi Buffon alichukua tuzo ya golikipa bora akiwabwaga wapinzani wake golikipa wa Real Madrid Keylor Navas na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer.

Olivier Giroud alipata tuzo ya bao bora huku kikosi bora cha Fifa kikiundwa na Gianluigi Bufgon, Dani Alves,Leornardo Bonuccci, Sergio Ramos, Marcelo,Toni Kroos, Andres Iniesta, Luvca Modric, Cristiano Ronaldo, Lioneil Messi na Neymar.

Tuzo zingine zilizotolewa usiku wa leo ni tuzo ya mchezaji bora wa kike iliyokwenda kwa Lieke Mertenes, tuzo ya kocha bora wa kike ikienda kwa Sarina Wiegman na tuzo ya mashabiki ikienda kwa mashabiki wa Celtic.

Picha 8 jinsi wanasoka walivyotokelezea green carpet na vimwana wao usiku wa The Best Fifa awards 17

$
0
0

Usiku huu wa tarehe 23 kulikuwa na tuzo za The Best Fifa awards zilizofanyika nchini Uingereza, wanasoka baadhi walikuja na wapenzi wao kama picha zinavyoonesha.

Kuelekea Dar derby, vitu ambavyo Simba na Yanga zinafanana baada ya mechi saba VPL

$
0
0

Mjadala mkubwa kwa upande wa soka nchini ni kuhusu October 28, 2017 siku ambayo meci ya watani wa jadi itapigwa watoto wa mjini wanaiita ‘Kariakoo derby’ game ambayo itazikutanisha Yanga na Simba katika mchezo wa VPL mzungunguko wa kwanza

Kabla ya mchezo kuo kupigwa, kuna baadhi ya vitu timu hizi zinafanana kwa kiasi kikubwa sana, idadi ya mechi, pointi, idadi ya mechi za kushinda na sare pamoja na mambo mengine mengi.

Idadi ya mechi

Kila timu imeshacheza mechi saba hadi sasa sawa na timu nyingine za ligi kuu

Pointi

Simba na Yanga zina pointi sawa (15) ambazo kila timu imepata baada ya kucheza mechi saba. Simba ndio inaongoza ligi kutokana na wastani mzuri wa magoli, Simba imefunga jumla ya magoli 19 na huku Aishi Manula akiruhusu magoli manne kwa hiyo wastani wa magoli wa Simba ni 15 wakati Yanga wao wamefunga magoli 10 lakini wamefungwa matatu hivyo kufanya wastani wao wa magoli kuwa saba. Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi juu ya Mtibwa Sugar ambao pia wana pointi 15.

Mechi za kushinda

Simba

Wameshinda mechi nne kati ya Saba waizocheza, wameshinda michezo mitatu wakiwa uwanja wao wa nyumbani (Uhuru) na mchezo mmoja wakiwa uwanja wa ugenini, Simba wamecheza mechi tatu ugenini huku mechi nne wakizipiga nyumbani.

  • Simba 7-0 Ruvu Shooting
  • Simba 3-0 Mwadui
  • Stand United 1-2 Simba
  • Simba 4-0 Njombe Mji

Yanga

Kama ilivyo kwa Simba Yanga pia wameshinda mechi nne kati ya mechi saba walizocheza, katika mechi nne walizocheza ugenini Yanga wameshinda mechi tatu na kutoka sare mchezo mmoja huku wakishinda mechi moja kati ya tatu walizocheza uwanja wa nyumbani.

  • Njombe Mji 0-1 Yanga
  • Yanga 1-0 Ndanda
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga
  • Stand United 0-4 Yanga

Mechi za sare

Simba

Imetoka sare katika mechi tatu, kati ya hizo michezo miwili wakiwa ugenini na mchezo mmoja wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani

  • Azam 0-0 Simba
  • Mbao 2-2 Simba
  • Simba 1-1 Mtibwa Sugar

Yanga

Katika mechi tatu walizotoka sare, michezo miwili ni kwenye uwanja wao wa nyumbani huku mechi moja wakibanwa ugenini.

  • Yanga 1-1 Lipuli
  • Majimaji 1-1 Yanga
  • Yanga 0-0 Mtibwa Sugar

Samatta awatosa Lioneil Messi na Cr7 katika The Best 2017

$
0
0

Jana kulitolewa Fifa The Best 2017 pale mjini London Uingereza, katika utoaji wa tuzo hizo manahodha wa timu za taifa dunia nzima walipewa nafasi kupiga kura kumpata mchezaji bora.

Tanzania nao walikuwa moja ya wapiga kura huku nahodha wa timu yetu ya taifa Mbwana Alli Samatta kituwakilisha kufanya zoezi hilo, na tofauti ya matarajio ya wengi Samatta alifanya kitu tofauti kabisa.

Kwa sasa dunia nzima inawazungumzia Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo kama wachezaji wakubwa kuwahi kutokea duniani, lakini kwa Samata hali ilikuwa tofauti na inaonekana hawakubali wote wawili.

Samatta kwenye kura zake tatu hajamuweka Cristiano wala Messi badala yake amempigia kura Ngolo Kante kiungo wa Chelsea, pia akampigia mshambuliaji wa PSG Neymar na kisha akampigia Muafrika mwenzake Pierre Aubemayang.

Hata hivyo kati ya wachezaji wote ambao Samatta amewapigia kura ni Neymar pekee ndio amefanikiwa kuingia kwenye tatu bora ya tuzo za mchezaji bora wa kiume huku tuzo ikienda kwa Cr7.

Ona manahodha maarufu duniani walivyopiga kura zao, Cr7 na Messi wakwepana

$
0
0

Kura zimepigwa kumtafuta mshindi wa tuzo ya The Best Fifa, na manahodha walipewa nafasi kupiga kura kwa kuandika majina matatu matatu, wafuatao ni baadhi ya manahodha maarufu na jinsi walivyopiga kura.

Eden Hazard, Hazard hakuona sababu ya kumnyima nyota mwenzake wa Chelsea Ngolo Kante kura, huku kura ya pili akimpigia nyota wa Real Madrid Cr7 na kura ya tatu akimpigia Luca Modric.

Lioneil Messi, kwa upande wa Messi yeye kura yake ya kwanza alimpigia Luis Suarez na ya pili akampa kiungo wa Barcelona Andres Iniesta huku kura yake ya tatu na ya mwisho akimpigia nyota wa PSG Neymar.

Brazil kura yao ilipigwa na Dani Alves ambaye aliwaweka wachezaji wote watatu walioingia tatu bora akianza na Neymar kisha akampigia Lioneil Messi na kura yake ya tatu akampigia Cristiano Ronaldo.

James Rodriguez nahodha wa Colombia yeye hakumpigia kura Lioneil Messi alianza na Cr7 kisha akampigia Sergio Ramos na ya tatu akampigia Robert Lewandoski.

Gianluigi Buffon mlinda lango wa Italia naye hakumpigia kura Messi bali kura yake ya kwanza ilienda kwa Cr7 ya pili akampa Paulo Dyabala na ya tatu akampigia Luka Modric.

Obi John Mikel nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria yeye alianza na Lioneil Messi, ya pili akampigia Cristiano Ronaldo na ya tatu akampigia Gianluigi Buffon.

Sergio Ramos aliweka unazi pembeni lakini kama kawaida jina la Cr7 alianza nalo kisha likafuatia na Lioneil Messi na jina lake la tatu akampigia Luca Modric.

Cristiano Ronaldo yeye kwa upande wake aliwapigia wachezaji wenzake wa Real Madrid kura akianza Luka Modric jina la pili akaweka Sergio Ramos kisha akamaliza na Marcelo.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>